Nimeacha kuishabikia Arsenal

Nimeacha kuishabikia Arsenal

Wakuu nimeamua kwa hiyari yangu na pasipo kulazimishwa na mtu yoyote kuitosa club ya Arsenal.Nina sababu nyingi za kuitosa The Gunners.

[1] Kukwepa magonjwa ya moyo.

[2] Imeshindwa kutwaa kikombe chochote kwa muda mrefu sana.

[3] Arsenal imekuwa gulio la kuuza wachezaji wake mahiri kwa Club nyingine

Baada ya kutafakari kwa kinaa na bila kushawishiwa au kulazimishwa na mtu au kikundi chochote nimeamua kujiunga na Club ya Manchester United yenye kutumia uwanja Old Trafold.Zipo sababu kibao lakini nitazitaja chache.

[1] Manchester United inaongozwa na manager mwenye mafanikio makubwa kuliko makocha wote wa UK.

[2] Manchester United imechukua ubingwa wa ligi kuu ya UK mara 19,timu inayoikaribia ni Liverpool pekee yake imechukua ubingwa mar 18 tu.

[3] Manchester United inakaribia kuweka rekodi mpya kwa kuchukua ubingwa mara 20, mpaka leo hii inaongoza ligi kwa tofauti ya point 12.

[4] Ukiishabikia Mancheter United uwezekano wa kupatwa na magonjwa ya moyo na kisukari ni mdogo sana.Kila wakati una kuwa ni mtu wa kucheka na kufurahia maisha duniani.

[5] Mwaka 1999 iliweka historia kwa kuchukua vikombe vitatu.Ubingwa wa ulaya.ubingwa wa Uk na Kombe la ligi.

[6] Mashabiki wa Manchester United ni wakarimu, wapole na wenye kujua kuchambua soka. Sifa hizo zinanihakikishia kwamba nitapokelewa vizuri.

Wapenzi wa Arsenal mtanisamehe sana kuhama club ni jambo la kawaida kwa mashabiki kama ilivyo kawaida kwa wachezaji. Siwezi kuendelea kusononeka hapa duniania kisa kupenda Club mbovu.

Nakala: Wacha1 Idimi Belo Steve Dii Mphamvu Dark City gfsonwin The Boss BAK Rejao Viper mfarisayo MwafrikaHalisi Kibunango Maxence Melo EMT Balantanda Mwita Maranya
Kwani ulivyoanza kuishabikia ulituambia
 
ndoa ya kikristo hiyo kaka -- kaza moyo !!
 
Wewe ni shabiki wa man u kwnye ubora wako,japo unashindwa kujionesha wazi direct sabab ya nafasi,muda ukifika utaenda ata ndanda
 
Arsenal:
The new UEFA Champions League winners for the first time in the history of UCL
2016/17 EPL winners
Huu ni mwaka wa Arsenal tu
2fdadc5b86b5304e5e7845ee1bc634aa.jpg
 
Game hii lazima tungepigwa hata kabla ya kuingia uwanjani...mtu mpuuzi sana huyu wenga ni mbwa
 
Nilifikiri unaizungumzia Arsenal, kumbe unaizungumzia Marefa United. Hata mimi najua ina mafanikio sana, ndio klabu pekee yenye kusajili wachezaji na marefa pia.

Kuhusu Arsenal kutochukua vikombe miaka mingi, utakuwa unaumwa wazimu.

Chelsea walisubiri miaka 40

Manchester City miaka 35

Je washabiki wao wamekufa na hayo magonjwa?
Je ni Arsenal peke yake ndio haichukui? Vipi kuhusu West Ham, Everton n.k?
Kuna jamaa kaniambia hivi , ukipata demu ambaye ni shabiki wa Arsenal ni bora uoe kabisa , ni wavumilivu balaa !
 
Umelogwa wewe, sisi hatuondoki Arsenal mpaka Yesu atakaporudi.
 
Back
Top Bottom