Nimeacha Rasmi Kutazama Mechi za Yanga NBC PL

unataka sema hata mwaka jana kimataifa walikuwa na hofu

ama hii hofu ni mechi za ndani tu

nan mwaka jana ajafungwa na yanga
 
Nimesoma kote ila ulivyoleta story kuwa hizo timu nyingne sijui wakikutana na Simba basi wanawakazi, kiukweli sijaendelea kusoma tena.
Ww mechi za Simba huwa unaangalia kweli? Magoli ya penalt za mchongo alafu unasema wanawakazia!!
 
Nimeamini kweli uelewa Tz umeshuka sana. Yaani hawa walopokaji wa timu akilopoka jambo hata liwe la kutunga tu kwa ufikiri wake tu lakini atapata kiwango kikubwa cha wafuasi wake kwa lugha zake tu. Hasa mashabiki wa mikia wanaamini sana kwa wasemaji wao.

Nakumbuka hata kipindi cha manara yuko simba ilikuwa wakisikia tu usemi fulani kutoka kwa manara kesho yake mitaani utawakuta mashabiki wa Simba wanapita na ile lugha yake.

Hawawezi kujifikiria na kuchanganua jinsi waonavyo wao. Wanaamini sana kutoka kinywani kwa walopokaji wao
Huyu kajitahidi anajaribu kuona kama ni ya kwake,lakini yote kwa yote anafuata mle mle kwa mlopokaji wao.

Hapo ujue bado zitakuja tred nyingi za mlengo ule ule wa lugha ya ahemed.

Kwenye mihemko ya kufuata usemi wa msemaji wa timu nawasifu sana mashabiki wa YANGA,hawana hiyo sana. Na ni wavumilivu sana mashabiki wa YANGA
 
Ni changamoto kubwa sana kama watashindwa kutofautisha kati ya mapenzi na kazi. Hii inapelekea bias na kuua falsafa yetu ya fairness katika mchezo wetu pendwa.

Maybe ni quality, maybe not. Umeangalia vizuri mechi tajwa hapo juu?
Nimetazama mechi zote
Ni matokeo ya kimchezo na Yanga anapata mechi ngumu na kufungwa.
Kama ingekuwa ivo kwanini Yanga anafungwa
Wapinzani wanapata on target
Yanga anataka card
Yanga wachezaji wanaumia
Si angekuwa anafika na kushinda
 
Tunazungumzia mechi za NBC. Kuhusu kama ni hofu, kuhongwa au sababu nyingine, hakuna anayejua....
tangu mwaka jana ni azam pekee aliye mfunga yanga

maana yake timu 13 zina muhofia yanga
 
haina shida kiongozi,tupo tutakaondelea kuangalia,i love you yanga
 
tangu mwaka jana ni azam pekee aliye mfunga yanga

maana yake timu 13 zina muhofia yanga
Mbona unang'ang'ania kuhofia tu wakati nimetoa sababu za kufungwa zaidi ya hiyo? Mimi na nadhani na mleta mada hatujatoa jibu la moja kwa moja la kwa nini hizi timu zinafungwa na Yanga katika mazingira yanayoonekana ni ya kizembe.

Au labda sijaelewa hoja yako ni ipi hasa.
 
Mada umeiwasilisha kistaarabu kuwafumba watu kwamba hujasema Yanga inahonga direct ila ulicho andika kina maana hiyo. Ukisema unasubiri uangalie mechi kati ya Yanga na Simba au Azam maana yake hao ndio hawahongwi unaamini kuna usawa. Lakini hizo hizo timu zimefungwa mara ngapi na Yanga akiwa anasemwa anahonga.? Sawa tujadili polepole.

Ubora huu wa Yanga sidhani kama unahitaji timu pinzani uanze kuihonga. Kama kweli ni shabiki wa mpira na unaangalia mpira bila fikra za kishabiki nikikuuliza kwanini hapa katikati Yanga alifungwa mechi mfululizo na hata alizoshinda alikua anashinda kwa mbinde sana lazima majibu yatakua fitness ilishuka hata kocha alilisema hili, wachezaji muhimu kupata majeraha na kadi nyekundu ya Bacca.

Kwasasa Yanga inavyocheza unaona kabisa fitness imerudi ari na morali ya wachezaji inarudi tofauti na hapo nyuma. Sasa Yanga kushinda kwa idadi hiyo inakushtua nini wewe kama sio chuki za kishabiki tu. Fikiria hili kwa kina usiruhusu moyo wako kukuendesha kwa kufuata hisia tu.
 
Mkuu naona umejikita kwenye ushabiki zaidi na sio uhalisia....hapa Tanzania timu zilizofanya uwekezaji mkubwa ni pamoja na yanga,,,,,kwa ninavyoziona timu za zote ni simba na azam tu ndio zenye uwezo wa kufunguka na kuweza kupata matokeo mbele ya yanga....zilizobaki ni lazima plan yao ya kwanza iwe ni kuwazuia yanga na kufanya mashambulizi ya kushtukiza.
 
J
Chandimu soka mara magori yafungwe na vidole yaani taabu tu jamaa kasema!
 
wale wanawivu na kinachowatisha sasahivi walijua kushindwa zile mechi kadhaa basi tutapoteana!, mambo si yameanza kukaa sawa tena mapema mno basi wameanza kuchanganyikiwa!
 
Kama Yanga Kila mchezaji akiweza kutoa uwezo wake kwa 80% hakuna timu itakayo fungwa Chini ya Goli 5.

Yanga Wana kikosi chenye wachezaji wenye vipaji vya hali yajuu akitofautiana na timu Nyingi za Ligi kuu.
 
Mbumbumbu kazi mnayo, niliwai kusema mda si mrefu mtatoka kwenye mashimo yenu Mmoja baada ya mwingine,, wakati yanga anafungwa mechi tatu mfululizo ulikuwa unampenda kuziangalia hizo mechi lakini yanga karudi kwenye makali yake ghafla unatoa milio kwamba utaki kuwaangalia TenaπŸ€”πŸ€”πŸ€”
Kwaiyo yanga wangeendelea kufungwa ungeendelea kuangalia mechi zao na ingekuwa burudani kwako?
 
Umezunguka kweli mseeπŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„.kataa hofu,hofu inaua🀣🀣🀣🀣 YANGA BINGWAπŸ˜„
 
Uliona mbali Mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…