Nimeacha rasmi kuweka status WhatsApp kwa sababu hii

Nimeacha rasmi kuweka status WhatsApp kwa sababu hii

Explainer

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2015
Posts
517
Reaction score
506
.........Kazi iendelee. Wadau mimi ni mfanyabiashara, kwenye simu yangu ya mkononi nimetunza namba takribani 300.

Kati ya hizo Kuna wateja zangu, ndugu zangu, jamaa na marafiki na bila kusahau wadau wa unywaji na michepuko kadhaa.

Hapo kwenye wateja zangu Kuna aina tofauti za watu. Mosi, Kuna namba za mabosi zangu, wahindi na wachina ambao nanunua bidhaa kwao. Pia Kuna wateja zangu watanzania, watu wa daraja la kati na huku chini kabisa kwa wale waogopa tozo.

Sasa baada ya kuwa na namba zote hizo nimegundua kitu kimoja makini sana. Aisee sisi masikini ndio tunaangaika na kuweka mastatus ya maisha yetu na mahangaiko yetu kila uchwao. Huu ni mwaka mmoja sasa bado sijaona wale wachina au wale maafsa, wahindi, na baadhi ya watu kadhaa wenye uhakika wa kula muda wowote wakiweka mistatus hata kwa bahati mbaya.

Sasa hawa michepuko, na wadau wengine walala hoi waliobaki Sasa😂😂😂 yaani ni kutwa mara tatu kama dose ya ukimwi. Utakuta status hata akiwa choo Cha public anapost.

Acha nimalizie kwa kusema watu werevu na matajiri wametuacha mbali kwa ustaarabu.... Nb Mapovu ruksa.
 
Status zimegawanyika;
Kuna mtu anapost biashara zake kwa nia ya kufanya matangazo kwa contacts yake,
Kuna mwingine anapost ili kuhimiza au kuhasa jambo fulani
Kuna mwingine anapost maisha yake ambapo hata akipanda daladala atataka watu wajue, au kupost hbd za watu. Naweza kusema huyu wa mwisho Ndio masikini wa akili na pesa
 
Ndugu zangu kuposti status au kutokuposti sio kiashiria wala tabia ya masikini wala tajiri ila ukweli ni kuwa kila mtu anaishi vile anawiwa .

Sikatai kuwa wanaojiposti mara nyingi ni wa uchumi wa chini ila pia nakushirikisha kuwa wapo wenye maisha yao na bado wanajiposti hivyo nipende kusema yote ni vile kila mtu anahitaji kuishi either kwa matakwa binafsi au kuendeshwa na jamii .

Hivyo mwisho tujue ya kuwa hapana sababu itakayokufanya kuitwa tajiri au masikini ila mpaka pale watu wakijidhibitishia kupitia mali ulizonazo na si vinginevyo .

Tuishi humo ishi maisha yako , tafuta pesa uwe huru wa fikra na uamuzi tunduizi katika maisha yako.
 
.........Kazi iendelee. Wadau mimi ni mfanyabiashara, kwenye simu yangu ya mkononi nimetunza namba takribani 300.

Kati ya hizo Kuna wateja zangu, ndugu zangu, jamaa na marafiki na bila kusahau wadau wa unywaji na michepuko kadhaa.

Hapo kwenye wateja zangu Kuna aina tofauti za watu. Mosi, Kuna namba za mabosi zangu, wahindi na wachina ambao nanunua bidhaa kwao. Pia Kuna wateja zangu watanzania, watu wa daraja la kati na huku chini kabisa kwa wale waogopa tozo.

Sasa baada ya kuwa na namba zote hizo nimegundua kitu kimoja makini sana. Aisee sisi masikini ndio tunaangaika na kuweka mastatus ya maisha yetu na mahangaiko yetu kila uchwao. Huu ni mwaka mmoja sasa bado sijaona wale wachina au wale maafsa, wahindi, na baadhi ya watu kadhaa wenye uhakika wa kula muda wowote wakiweka mistatus hata kwa bahati mbaya.

Sasa hawa michepuko, na wadau wengine walala hoi waliobaki Sasa[emoji23][emoji23][emoji23] yaani ni kutwa mara tatu kama dose ya ukimwi. Utakuta status hata akiwa choo Cha public anapost.

Acha nimalizie kwa kusema watu welevu na matajiri wametuacha mbali kwa ustaarabu.... Nb Mapovu ruksa.
Inategemea na mtu mwenyewe mtazamo wake ukoje, ila kutokuweka status sio kigezo cha kwamba mtu ni tajiri au ni mwerevu sana..Kuna watu ni matajiri wanaweka status na kuna maskini hawaweki status...Ishu ni kwamba maudhui ya Status za matajiri wengi hawapendi kuanika life style zao...wao ni kupost labda habari fulani,michezo au mambo ya kidini..ila maskini wengi status ni sehemu ya Majungu na vichambo na jukwaa la matangazo wakifanikiwa ki jambo kidogo ni siku nzima ni full show off...ila upande wa wanawake Status ni sehemu ya kujigamba akila kitu tu lazima apige picha aweke status..
 
Kwa wenye akili watakusoma akii yako kupitia status.
Hasa wanawake wanamegwa kirahisi kupitia post zao za status.
Mtu anajua fika anapitia kipindi flani...anaye anakujia kama malaika wa nuru...kumbe ni mzabzab tu🤣🤣🤣
Wewe bwana all men, mzabzab included want one thing from a woman. Fortunately for us, women want it too😝
 
Back
Top Bottom