Habari Kaka, mimi ni Binti wa miaka 28, sijaolewa ila nina mchumba wangu. Huyu Kaka nilikaa naye kwenye mahusiano kwa miaka mittano. Lakini alianza kubadilika ghafla mpaka akampa mwanamke mwingine ujauzito wakawa wanaishi naye. Alishanitambulisha mpaka kwao lakini baada ya kumpa huyo dada ujauzito aliniambia kuwa wazazi wake hawanitaki kwakua hawana uhakika kama nina kizazi au la hivyo wamemuambia kuwa amuoe huyo mwanamke mwingine.
Nilimuambia nimbebe mimba yake akagoma na kuniambia tuendelee kuwa marafiki tu lakini suala la ndoa haliwezekanai. Niliumia sana akawa anakuja kwangu ila anaishi kwa ule mwanamke mpaka alipojifungua. Baada ya kuanza kukusoma niliona kama ananipotezea muda hivyo niliamua kuchana naye. kuna Kaka alikua ananitongoza nikaamua kumkubalia na tukaanza mahusiano, huyo Kaka alikua siriasi kwani baada ya miezi minne tu alikuja kujitambulisha kwetu, akatoa mahari na mipango ya ndoa ilianza.
Baada ya kuona kuwa naolewa X wangu alinitafuta, aliomba tuonane na mimi kwakukua nilikua na mtu wangu basi nilikubali. Huko alianza kunielezea matatizo na mwanamke wake, aliniambia kwanza ni mchafu, mchotyo, hapendi ndugu zake na anafikiria kumuacha kwani Mama yake hamtaki tena anatamania angenioa mimi. Tuliongea mengi sana lakini sikumsikiliza, ila alianza kuomba msamaha, akawa anatuma mpaka na rafiki zake.
Kwakua ni mtu ambaye nilikua nampenda nilijikuta kuwa narudi wkake, nikajikuta sina hamu tena na mchumba wangu na mwisho nikaamua kumuambia mchumba wangu mpya kuwa tuliharakisha lakini mimi simpendi hivyo nataka tuachane. Alilia sana akaumia kw2ani alidai nimemuaibisha kwao kwakua kila kitu kilishaandaliwa ila sikua na namna, niliona hakuna haja ya kuingia kwenye ndoa na mwanaume ambaye simpendi wakati mtu ninayempenda amerudi.
Ndugu zangu walinisihi sana nisimuache lakini nilishafanya maamuzi. Sababu ya kuja kwako Kaka ni hivi, baada ya kuchana na mchumba wangu huyu mwanaume alinishawishi kubeba mimba yake ili iwe rtahisi yeye kunitambulisha kwa wazazi wake kwani hawawezi kunikubali kama hawajui kuwa nazaa. Nilibeba mimba yake kweli na sasa hivi nina ujauzito wa miezi nane ila kuna mambo yamebadilika Kaka naomba unisaidie kwani nimechanganyikiwa.
Kwanza bado anaishi na X wake, mwanzo aliniambia kuwa wanaishi pamoja kwasababu ya mtoto ila yeye hana mapenzi naye kwani hata tendo la ndoa hawafanyi. Lakini Kaka mimi mimba yangu ina miezi nane nimechunguza nimegundua kuwa kumbe hata huyo mwanamke naye ana mimba ya mtoto wa pili. Kumbuka aliniambia wanalea tu mtoto, sasa Kaka namuuliza kwanini amempa ujauzito ananiambia ilikua ni bahati mbaya.
Anadai kuna siku alirudi nyumbani kalewa ndiyo mwanamke akammbaka na kumlazimisha kufanya naye mapenzi lakini yeye hamtaki. Tuligombana sana nikamuambia kuwa amuache huyo mwanamke, basi siku iliyofuata alichukua vitu vyake kwa huyo mwanamke na kuhamia kwangu. Aliniambia kuwa kaamua kumuacha mwanamke wake, lakini Kaka sio hivyo nimechunguza nimegundua kuwa kule kwa yule mwanamke kamuaga kuwa anasafiri kikazi na wala hajamuambia kuhusu mimi.
Nimemuambia si nina mimba basi anipeleke kwao kunitambulisha ananizungusha ananiambia kuwa Mama yake sasa hivi ana presha kwahiyo tutamchanganya tusubiri mpaka apone ndiyo anipeleke. Kaka naomba nisaidie, mwanuame kaja anaishi kwangu, ana kazi nzuri lakini hatoi chochote, kila kitu nahudumia mimi, yaani hata umeme ukikatika hawezi kununua. Kifurushi cha Azam kikiisha basi kama kuna mpira atanunua cha wiki nisiponunua ila ndiyo basi, naomba nisaidie kuna mapenzi kweli hapa?
Sent using
Jamii Forums mobile app