Nimeachwa na mpenzi sababu anataka tuishi pasipo ndoa (sogea tuishi)

Nimeachwa na mpenzi sababu anataka tuishi pasipo ndoa (sogea tuishi)

Sema wazi tu kuwa unataka upate leseni rasmi ya kuzini au kwa kiswahili rahisi ni leseni ya kungonoka bila woga tena. Ati upate baraka za wazazi. Kwani sasa mnapo ngonoka huwa unaenda kuomba radhi kwao asubuhi au huwa unaenda tu kuoga na kubadili nguo??
Mambo ingine Tz ni kama kuivuruga akili tu.
Amua uende kwake haraka sana la sivyo usije hapa ukilia kuwa; Aliniacha jana tu leo ako na wawili
Acha hizo, kama huwezi shauri maneno ya busara bora unyamaze. Mambo ya ngono hayo ni yake binafsi, focus kwenye mada.
 
Acha hizo, kama huwezi shauri maneno ya busara bora unyamaze. Mambo ya ngono hayo ni yake binafsi, focus kwenye mada.
Sisemi na mjinga miye nasema na wanaojielewa. Unaenda kuomba ridhaa kwa wazazi ati ninatamani kwenda kungonoka?? We ni aje??
 
Mkuu wewe inaonekana una makomplication mengi,na hujui maana ya ndoa na harusi,ndoa ni muungano wa hiari kati ya Mwanamme na mwanamke kama mke Na mme,sasa sijui wewe unataka ndoa au unataka mke,maana ninyi wanawake mmekua watu wenye kupenda ufahali na hivyo kuwalazimisha wanaume waingie kwenye mambo ambayo hawa kutarajia matokeo yake ni kuwapoteza wale mnao wapenda

Tatizo lako hamjapatana ni kipi kifanyike,wewe unataka harusi,mwenzio anataka ndoa sasa hapa lazima hamtaelewana,mimi nakushauri uungane na mwenzako anayetaka ndoa,achana na mambo ya harusi

Mimi baada ya kutanguliza mahari ukweni nilimchukua wife bila hata hizo ndoa unazozisema na mke wangu licha ya elimu aliyekuwa nayo hakujali,lakini pia hata wazazi wako walicho Kali ikiwa kumwona binti yao anapata mwenzako

Mwisho be watchful, utakomalia nyumbani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh,pole sana...hapa wanaJF tunaweza kukomaza shingo muache...kumbe usiku mwazima taa mwalala..nachotaka kusema maamuzi ni juu yako…..kwangu mimi ndoa ni makaratasi tu..ila kwa wengine ina heshima ya kipekee....ila chunguza kama havumiliki kwa mengine ndio umuache...kumpenda mtu 100% na yeye akupende 100% ni nadharia ambayo haipo...wengi wanacompromize..so kigezo cha kukupenda sio sababu ya kumuacha and second ndoa sio kipimo cha upendo,mnaweza kufunga leo ndoa akakucheat next day....pengine he is hurt from previous relationship so ana trust issues......namtetea as if ananilipa humu... 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Habari Kaka, mimi ni Binti wa miaka 28, sijaolewa ila nina mchumba wangu. Huyu Kaka nilikaa naye kwenye mahusiano kwa miaka mittano. Lakini alianza kubadilika ghafla mpaka akampa mwanamke mwingine ujauzito wakawa wanaishi naye. Alishanitambulisha mpaka kwao lakini baada ya kumpa huyo dada ujauzito aliniambia kuwa wazazi wake hawanitaki kwakua hawana uhakika kama nina kizazi au la hivyo wamemuambia kuwa amuoe huyo mwanamke mwingine.

Nilimuambia nimbebe mimba yake akagoma na kuniambia tuendelee kuwa marafiki tu lakini suala la ndoa haliwezekanai. Niliumia sana akawa anakuja kwangu ila anaishi kwa ule mwanamke mpaka alipojifungua. Baada ya kuanza kukusoma niliona kama ananipotezea muda hivyo niliamua kuchana naye. kuna Kaka alikua ananitongoza nikaamua kumkubalia na tukaanza mahusiano, huyo Kaka alikua siriasi kwani baada ya miezi minne tu alikuja kujitambulisha kwetu, akatoa mahari na mipango ya ndoa ilianza.

Baada ya kuona kuwa naolewa X wangu alinitafuta, aliomba tuonane na mimi kwakukua nilikua na mtu wangu basi nilikubali. Huko alianza kunielezea matatizo na mwanamke wake, aliniambia kwanza ni mchafu, mchotyo, hapendi ndugu zake na anafikiria kumuacha kwani Mama yake hamtaki tena anatamania angenioa mimi. Tuliongea mengi sana lakini sikumsikiliza, ila alianza kuomba msamaha, akawa anatuma mpaka na rafiki zake.

Kwakua ni mtu ambaye nilikua nampenda nilijikuta kuwa narudi wkake, nikajikuta sina hamu tena na mchumba wangu na mwisho nikaamua kumuambia mchumba wangu mpya kuwa tuliharakisha lakini mimi simpendi hivyo nataka tuachane. Alilia sana akaumia kw2ani alidai nimemuaibisha kwao kwakua kila kitu kilishaandaliwa ila sikua na namna, niliona hakuna haja ya kuingia kwenye ndoa na mwanaume ambaye simpendi wakati mtu ninayempenda amerudi.

Ndugu zangu walinisihi sana nisimuache lakini nilishafanya maamuzi. Sababu ya kuja kwako Kaka ni hivi, baada ya kuchana na mchumba wangu huyu mwanaume alinishawishi kubeba mimba yake ili iwe rtahisi yeye kunitambulisha kwa wazazi wake kwani hawawezi kunikubali kama hawajui kuwa nazaa. Nilibeba mimba yake kweli na sasa hivi nina ujauzito wa miezi nane ila kuna mambo yamebadilika Kaka naomba unisaidie kwani nimechanganyikiwa.

Kwanza bado anaishi na X wake, mwanzo aliniambia kuwa wanaishi pamoja kwasababu ya mtoto ila yeye hana mapenzi naye kwani hata tendo la ndoa hawafanyi. Lakini Kaka mimi mimba yangu ina miezi nane nimechunguza nimegundua kuwa kumbe hata huyo mwanamke naye ana mimba ya mtoto wa pili. Kumbuka aliniambia wanalea tu mtoto, sasa Kaka namuuliza kwanini amempa ujauzito ananiambia ilikua ni bahati mbaya.

Anadai kuna siku alirudi nyumbani kalewa ndiyo mwanamke akammbaka na kumlazimisha kufanya naye mapenzi lakini yeye hamtaki. Tuligombana sana nikamuambia kuwa amuache huyo mwanamke, basi siku iliyofuata alichukua vitu vyake kwa huyo mwanamke na kuhamia kwangu. Aliniambia kuwa kaamua kumuacha mwanamke wake, lakini Kaka sio hivyo nimechunguza nimegundua kuwa kule kwa yule mwanamke kamuaga kuwa anasafiri kikazi na wala hajamuambia kuhusu mimi.

Nimemuambia si nina mimba basi anipeleke kwao kunitambulisha ananizungusha ananiambia kuwa Mama yake sasa hivi ana presha kwahiyo tutamchanganya tusubiri mpaka apone ndiyo anipeleke. Kaka naomba nisaidie, mwanuame kaja anaishi kwangu, ana kazi nzuri lakini hatoi chochote, kila kitu nahudumia mimi, yaani hata umeme ukikatika hawezi kununua. Kifurushi cha Azam kikiisha basi kama kuna mpira atanunua cha wiki nisiponunua ila ndiyo basi, naomba nisaidie kuna mapenzi kweli hapa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo sio mwanaume ni shetani katika umbo la mwanaume.
 
Wakuu kuna jambo linanitatiza.
Nimekuwa na mahusiano kwa miaka miwili sasa huyu mwenzangu anataka tuchukuane kimya kimya (sogea tuishi) pasipo ndoa rasmi. Anaeleza kuwa baada ya mimi kwenda kwake wazazi wake waende nyumbani kwetu kutoa taarifa kuwa nimeolewa!

Kwa upande wangu nimejaribu kumueleza kuwa siyo jambo la busara mimi kufanya hivyo nahofia wazazi wangu kusononeka (nitakosa baraka za wazazi)

Nimejaribu kumweleza tutambulishane rasmi tufunge ndoa simple tu isiyokuwa na shamrashamra ila amekuwa mgumu kuelewa.

Ameamua kuniacha kisa nimekataa kuolewa kimyakimya pasipo kuwaeleza wazazi kuwa nimepata mchumba.

Bado nampenda sana nifanyeje ili tuweze kufikia suluhu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanza kabisa umejishusha hadhi wewe mwenyewe. Hivi nyie vijana wa kisasa, nani aliwaambia ndoa hutanguliwa na kuchokonoana hovyo? Mwanamume atakuwakia tamaa pale tu anapokuwa hajakuonja, lakini baada ya hapo ni maamuzi binafsi tu, yaani ni kama hisani kwako, hafungwi na lolote.

Sasa umempa huduma kwa miaka miwili, anakujua kona zako zote, umahiri na udhaifu wako mpaka kitandani. Huoni hana kipya cha kumfanya awake tamaa juu yako? Na ili kukuthibitishia hilo, ameamua akudanganye umsogezee mzigo karibu wakati hajaamua kuoa bado, pia hajampata wa kumfanya mke!! Wewe ni kiburudisho tu, so acha kabisa kujitapa eti unampenda sana. Nani kakupa kupenda wewe!?

Siku akitaka kuoa huyo jamaa yako unayempa manufaa ya ndoa pasipo ndoa atamtafuta binti mwenye hadhi ya ndoa na kisha atafuata taratibu zote kama zilivyo mila na desturi. Kwa sasa wewe endelea tu kuwa kipozeo, anakuhitaji short term. Wakati unahesabu una mpenzi unayemtumainia aje kuwa mume, mwenzako anahesabu ana demu anayemtimizia tamaa zake kwa kipindi hiki hajajipanga kuoa.

1. Jifunze kwa nini hilo tendo la kujamiiana linaitwa TENDO LA NDOA.

2. Jifunze ujue ni kwa nini hata kabidhi wasii mkuu hafungishi ndoa bila ridhaa ya wazazi.

Jifunze kwa nini mwanamke hakuumbiwa kupenda.

Ikimbie zinaa binti, unakula majira yako bure. Mwanamke huna muda mrefu wa kutamba, ukija shituka utakuta umetoka nje ya chati na hakuna anayetaka kuoa mwanamke aliyekuwa demu wa mtu mwingine. Corona inatosha, maradhi ya moyo ya nini? Acha kujigeuza chombo cha kumstarehesha mwanamume mwingine wewe binti. Mwoaji haji kwa sura hiyo, hata kidogo!!!

Mwanamke anapendwa, sio kupenda. Wacha waje wenye nia wakutongoze japo kwa miezi sita ndipo unaweza kuwapa masharti ya kupitia home ili wakupate kihalali. Sasa wewe kujidai kupenda ni namna nyingine ya kujigeuza kahaba uliyejihalalisha. Mwanamke, SUBIRI UPENDWE MAMA, mwanamume hapendwi, anaheshimiwa tu.

Najua neno hili ni gumu kwako na laweza kukukwaza, lakini ukweli lazima usemwe. Namaliza na unabii kwako, kama hutobadilika watakutafuna sana tu kisha watakutosa. Tabia yako tu mpaka sasa inaashiria hufai kuwa mke wa ndoa, wewe ni wa kuwatunza wanaume wasioweza kujizua kabla hawajaamua kutafuta wa kufunga nao ndoa. Unafanya ukahaba kwa kisingizio cha mapenzi kwamba una mapenzi ya dhati.

Mapenzi yatatoka kwa mwanamume kuja kwa mwanamke, sio kinyume chake. Miaka miwili ilitosha kwa huyo shefa wako kuwa amekuoa kabisa kama kweli umemchanganya, lakini yaonekana jamaa hata wazo hana. Anayetakiwa kufanya taratibu za kuoa ni mwanamume na sio mwanamke, kama jamaa anataka uingie ndani mwake ndipo ajipange, ni kwa sababu amekuona wewe ni kahaba tu ila hujiuzi mojankwa moja. ANAKUTENDA KAMA KAHABA. Ukienda kwake atakutumia mpaka atakapo kuwa tayari kuoa kisha anaweza kukuambia wazazi wake wamekukataa.

NAKUTAKIA MAPENZI MEMA!!

WASALAAM,

Nyenyere

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Tunda ashawahi kulila?
Hapo ndipo penye nguvu pekee ya mwanamke, make up wengi tu wanaweza kupaka wakawa kama majini mahaba.
Kama amekuwa akikutafuna kuna nini tena kimebaki kwako ambacho kitamfanya akuhesabu mke? Tendo la ndoa tayari hata kabla ya ndoa. Basi subiri tu huruma yake.
Nina miaka 27 mwanaume 33 hatujawahi kukwaruzana katika mahusiano yetu. Ndiyo nimemaliza chuo GPA haina mashiko hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
Miaka 27 ni jioni sana, unatoka kwenye ulingo wa ndoa. Jamaa akitaka kuoa atashuka chini zaidi. Kwa nini kuuchezea wakati? Hao ndugu zako waliojua kwamba jamaa anakutumia kama kiburudisho hawakukulinda kabisa. Hili ni tatizo la kizazi hiki. Waweza hata kumwagiza kaka wa mtu akuitie dada yake aje gheto, stupid!!

Acha kulia lia, chukua hatua, BADILI MAISHA YAKO SASA. Hao wanaokushauri utafute mwingine wanakudanganya. Mwanamke wa kuolewa anatafutwa, sio yeye atafute.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Wakuu kuna jambo linanitatiza.
Nimekuwa na mahusiano kwa miaka miwili sasa huyu mwenzangu anataka tuchukuane kimya kimya (sogea tuishi) pasipo ndoa rasmi. Anaeleza kuwa baada ya mimi kwenda kwake wazazi wake waende nyumbani kwetu kutoa taarifa kuwa nimeolewa!

Kwa upande wangu nimejaribu kumueleza kuwa siyo jambo la busara mimi kufanya hivyo nahofia wazazi wangu kusononeka (nitakosa baraka za wazazi)

Nimejaribu kumweleza tutambulishane rasmi tufunge ndoa simple tu isiyokuwa na shamrashamra ila amekuwa mgumu kuelewa.

Ameamua kuniacha kisa nimekataa kuolewa kimyakimya pasipo kuwaeleza wazazi kuwa nimepata mchumba.

Bado nampenda sana nifanyeje ili tuweze kufikia suluhu?

Sent using Jamii Forums mobile app

Achana nae hakupendi huyo mwizi. Kama anakupenda atakwenda kwenu kujitambulisha, au ana mke/ndoa nyingine? kuwa makini.
 
hapa ni kama unapiga story kijiweni.....yapo yatakayo faa na yasiyo faaa.....yeye anakupenda kwa dhati?? na wewe wampenda kwa dhati???..yazungumzeni kwa weledi....ndoa ni maisha yenu sio ya wazazi......kumbuka mnaenda kujenga maisha yenu....jamaa ndio driver.....usinganganie tu kuwaridhisha watu....BINADAMU hawaridhiki kamwe..
 
Hapo ndipo penye nguvu pekee ya mwanamke, make up wengi tu wanaweza kupaka wakawa kama majini mahaba. Kama amekuwa akikutafuna kuna nini tena kimebaki kwako ambacho kitamfanya akuhesabu mke? Tendo la ndoa tayari hata kabla ya ndoa. Basi subiri tu huruma yake.Miaka 27 ni jioni sana, unatoka kwenye ulingo wa ndoa. Jamaa akitaka kuoa atashuka chini zaidi. Kwa nini kuuchezea wakati? Hao ndugu zako waliojua kwamba jamaa anakutumia kama kiburudisho hawakukulinda kabisa. Hili ni tatizo la kizazi hiki. Waweza hata kumwagiza kaka wa mtu akuitie dada yake aje gheto, stupid!!

Acha kulia lia, chukua hatua, BADILI MAISHA YAKO SASA. Hao wanaokushauri utafute mwingine wanakudanganya. Mwanamke wa kuolewa anatafutwa, sio yeye atafute.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
Nimekupata Bingwa......ajishushe wakae wayamalize.......huo anaojidai MSIMAMO....na hapa kijiweni wanampa kichwa...amesahau....hakuna mwanaume yuko tayari kununua gazeti jioni...LISHASOMWA SANA......na anaemkimbia ndie alimpa gazeti toka asubuhi....
 
Hapana mkuu bado nampenda mpenzi wangu

Sent using Jamii Forums mobile app

Ndio uzwazwa wa wengi kwenye mapenzi hamtumii akili zenu mnaruhusu mioyo yenu itawale akili zenu!!

Hii kauli “bado nampenda” huwa inanikera mimi!

Kwenye mapenzi hatuwi na mtu sababu tunampenda, ila sababu anakupa sababu za kuishi nae, akujali, akuheshimu, akuthamini na kukusikiliza.

Kwangu mimi ndoa ni stara kwa mwanamke, inampa mwanamke heshima yake, kitendo cha mwanaume kwenda kwenu kwa ajili yako ni heshima tosha! Sasa unavyohamia kwake kuna utofauti gani na yule muuza pap aliyeokotwa club usiku, hawezi kunyenyua mguu wake kwenda kwenu nawe usinyenyue wako kwenda kwake, wanawake wa siku hizi vipi mbona mnakuwa supu hivyo, mbona mnakuwa warahisi kiasi hicho, kwamba ndio wanaume tumekuwa adimu au, ungekuwa karibu yangu ningekuweka kerebu,

Nilitaka nichangie ila hii kauli “bado nampenda” imechafua hali ya hewa
Unakuta jitu mwanaume mwaka wa 6 ana tabia mbovu ama anakula kipigo kila siku ni kusuluhishwa kila siku kilio, mkilishauri linasema bado nampenda, jitu halioneshi hata kubadilika, kama hawezi kuacha maovu kwa ajili yako badi ujue humo hauna mwenzi wa maisha

Changanya zako na za kuambiwa! Uamuzi upo mikononi mwako.

[emoji1435]‍♂️[emoji1435]‍♂️[emoji1435]‍♂️
 
Nimekupata Bingwa......ajishushe wakae wayamalize.......huo anaojidai MSIMAMO....na hapa kijiweni wanampa kichwa...amesahau....hakuna mwanaume yuko tayari kununua gazeti jioni...LISHASOMWA SANA......na anaemkimbia ndie alimpa gazeti toka asubuhi....
Umemaliza mkuu

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
hapa ni kama unapiga story kijiweni.....yapo yatakayo faa na yasiyo faaa.....yeye anakupenda kwa dhati?? na wewe wampenda kwa dhati???..yazungumzeni kwa weledi....ndoa ni maisha yenu sio ya wazazi......kumbuka mnaenda kujenga maisha yenu....jamaa ndio driver.....usinganganie tu kuwaridhisha watu....BINADAMU hawaridhiki kamwe..
Mkuu wazazi sio WATU BAKI. Acha kumpotosha. Unadhani yatakapomshinda huko atarejea kwa nani? Kauli eti ndoa ni yenu wawili ni uongo mwingine uliopenyezwa kwa kizazi cha sasa. Na wengi wameumizwa kwa ajili hiyo. Huyo unayemwita driver wala sio wa kujenga maisha, keshajilia vyake karidhika, sasa anatafuta gia ya kutokea.

Habari za mwanamke kumpenda mwanamume kwa dhati ni kujipoteza tu. Mwanamke huongozwa kwa hisia, mwanamume kwa reasoning. Sasa ukitaka atumie hisia tu kumpenda mwanamume kwa dhati ataliwa sana tu. Asubiri kupendwa na si vinginevyo. Ndoa sio taasisi ya masikhara kama mnavyoichukulia, wakiingia kimzaha mzaha itaisha hivyo hivyo.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Mkuu wewe inaonekana una makomplication mengi,na hujui maana ya ndoa na harusi,ndoa ni muungano wa hiari kati ya Mwanamme na mwanamke kama mke Na mme,sasa sijui wewe unataka ndoa au unataka mke,maana ninyi wanawake mmekua watu wenye kupenda ufahali na hivyo kuwalazimisha wanaume waingie kwenye mambo ambayo hawa kutarajia matokeo yake ni kuwapoteza wale mnao wapenda

Tatizo lako hamjapatana ni kipi kifanyike,wewe unataka harusi,mwenzio anataka ndoa sasa hapa lazima hamtaelewana,mimi nakushauri uungane na mwenzako anayetaka ndoa,achana na mambo ya harusi

Mimi baada ya kutanguliza mahari ukweni nilimchukua wife bila hata hizo ndoa unazozisema na mke wangu licha ya elimu aliyekuwa nayo hakujali,lakini pia hata wazazi wako walicho Kali ikiwa kumwona binti yao anapata mwenzako

Mwisho be watchful, utakomalia nyumbani

Sent using Jamii Forums mobile app
Bora wewe uliyetanguliza mahari manake ulijitambulisha ukweni. Kuliko nijitangulize kwa mume alafu baada ya wiki wazazi wake waje kwetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom