Nimeachwa na mpenzi sababu anataka tuishi pasipo ndoa (sogea tuishi)

Nimeachwa na mpenzi sababu anataka tuishi pasipo ndoa (sogea tuishi)

Mkuu wazazi sio WATU BAKI. Acha kumpotosha. Unadhani yatakapomshinda huko atarejea kwa nani? Kauli eti ndoa ni yenu wawili ni uongo mwingine uliopenyezwa kwa kizazi cha sasa. Na wengi wameumizwa kwa ajili hiyo. Huyo unayemwita driver wala sio wa kujenga maisha, keshajilia vyake karidhika, sasa anatafuta gia ya kutokea.

Habari za mwanamke kumpenda mwanamume kwa dhati ni kujipoteza tu. Mwanamke huongozwa kwa hisia, mwanamume kwa reasoning. Sasa ukitaka atumie hisia tu kumpenda mwanamume kwa dhati ataliwa sana tu. Asubiri kupendwa na si vinginevyo. Ndoa sio taasisi ya masikhara kama mnavyoichukulia, wakiingia kimzaha mzaha itaisha hivyo hivyo.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
Ww utakuwa una watt wengi wa kike

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu kuna jambo linanitatiza.
Nimekuwa na mahusiano kwa miaka miwili sasa huyu mwenzangu anataka tuchukuane kimya kimya (sogea tuishi) pasipo ndoa rasmi. Anaeleza kuwa baada ya mimi kwenda kwake wazazi wake waende nyumbani kwetu kutoa taarifa kuwa nimeolewa!

Kwa upande wangu nimejaribu kumueleza kuwa siyo jambo la busara mimi kufanya hivyo nahofia wazazi wangu kusononeka (nitakosa baraka za wazazi)

Nimejaribu kumweleza tutambulishane rasmi tufunge ndoa simple tu isiyokuwa na shamrashamra ila amekuwa mgumu kuelewa.

Ameamua kuniacha kisa nimekataa kuolewa kimyakimya pasipo kuwaeleza wazazi kuwa nimepata mchumba.

Bado nampenda sana nifanyeje ili tuweze kufikia suluhu?

Sent using Jamii Forums mobile app

"...Hata yusufu alijaribu kumuacha kwa siri mwana mwali bikira....."

Endelea kudumu katka maombi....👣👣👣👣👣👣👣👣👣👣🍺
 
Acha ujinga. NEVER compromise your values kwa ajili ya ujinga wa aina hiyo hata siku moja.
Huyo most likely anataka kukutumia tuu (naongea hivi kwa experience binafsi kama mwanaume). Mwanaume anaekupenda from the bottom of his heart, hawezi kufanya hicho anachofanya jamaa yako.
Stick to your values, do not degrade yourself kisa tu kuolewa (tena bila utaratibu).
Upendo iswa
Mwanaume hawezi kumuweka ndani mmwanamke asiye mpenda hata siku moja
 
Mwanaume hawezi kumuweka ndani mmwanamke asiye mpenda hata siku moja
Well, ni kutofautiana perspectives tu.
Mimi my perspective is, anaweza kumuweka ndani mwanamke aliemtamani (sio aliempemda) kwa matumizi ya muda mfupi ili kukidhi mahitaji yake kwa muda huo. Na hapo hutumia mbinu mbalimbali kufanikisha hilo.
Econometrician
 
Mwambie aende akajitambulishe kwenu,mambo mengine mtafanya taratibu;kukaa na mtu bila ndugu zake kujua ni bomu linaloweza kulipuka muda wowote (akikufia hapo ni balaa lingine).
 
Uamuzi uliochukua ni mzuri sana mkuu... Us I ones he upo desperate na ndoa kwa kujirahisisha kwenda kuishi nae maana ukienda tu utakuwa ndo umeolewa hata mahari wanaweza wasitoe....

Good choice, inaonekana upo smart upstairs kama ndoa ipo ipo tu Mungu ataileta kama haipo huwezi ilazimisha iwepo by the way kuwa some great men wapo bado so utapata mkuu Mungu akusimamie .....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom