Nimeachwa na nimekubali, ingawa naumia moyoni

Nimeachwa na nimekubali, ingawa naumia moyoni

Mi naona ni jambo jema.
Rudi kwenye soko angaza mali mpya.

Bora mmemaliza hili mapema nisingeelewa mtu, mtuchangishe michango baada ya mwaka na robo, ndoa chali muanze visa, heshimuni sana michango yetu hata kama mnatupa kuku na bia.
Umenena vema mkuu. Ingawa umesimanga kwa sehemu [emoji28]...
 
mzee piga moyo konde amini kwangu utampata aliebora zaid ya huyo.

Kweli mapenzi yanauma ila usifadhaike zaidi ukaunyima moyo wako furaha kisa huyo mwanamke,kwanza shukuru san ulikuwa unaoa mwanamke asiekuwa na misimamo huyo inadhihirisha anaeza hata kuliwa na Ex wake...nimalizie neno TAFUTA PISI KALI ZAID YA HUYO WANAWAKE BILA KUWA NA AKILI YA ZIADA WATAKUCHEZEA AKILI
 
Sio vigari vya chini kama crown, naendesha Discovery 4 Hybrid, la juujuu.

Nikipanda au kushuka siwi nimechuchumaa, nasimama.
aise me hata hilo gari lenyewe silijui,hongera mkuu. ILA mapenzi ni kitu kingne kabisa, kuna funzo kwene shuhuda yako hii
 
Pole Mkuu Amicus Curiae huwa naelewa sana falsafa zifuatazo katika mahusiano.

1. Ni makosa makubwa mwanamke kufahamu kuwa bila yeye mambo yako yatakwqma, hakika mwanamke akilijua hilo lazima akusumbue tu.

2. Hii inabebana na iyo ya kwanza, kamwe mwanaume haupaswi kujishusha mbele ya mwanamke hasa mwanamke uliye naye kwenye mahusiano. Huna sababu ya kujieleza kwa jambo lolote kwake. Ila muhimu wewe muheshimu tu na mipaka izingatiwe.

3. Usimuombe mwanamke kumuoa wewe fanya mambo yako hadi siku yeye atakapoomba wewe umuoe na kamwe usikubali akuendeshe au kukulazimisha kumuoa

Sasa Mkuu huyu mwanamke alijua bila yeye mambo yako hayataenda, huyo usihangaike naye kabisa funga ukurasa focus kwenye mambo mengine.

Pole sana Mkuu Amicus Curiae
hapo no3 imekaa vyema zaid yan bora mwanamke alilie ndoa kuliko mwanaume ndio uforce ndoa oyaaa utakuja kuchapwa matukio mpk uwe chizi
 
Na pia nadhani ulijitoa sana kwake kwa kila kitu. Going forward be careful unapodeal na mwanadamu; na angalau uwe tayari kwa lo lote maana mwanadamu anaweza kubadilika wakati wo wote. Jitoe kwa upendo huku ukijua kuwa ni sadaka tu unatoa lakini siyo kwa kutegemea cho chote maana kusema kweli loyalty ya mtu huwezi kuinunua ama kwa material things wala upendo wako wa kweli. Mwanadamu anaweza kuwa kiumbe katili sana akiamua!

Lakini pia kama malengo yako yalikuwa safi kwa huyu binti (if your intentions were pure) basi ondoka na dhamira safi huku ukijua kuwa hukumpotezea muda wake...and the Universe will reward you handsomely. Mwache aende na mtakie mema ila usije ukashangaa huko mbele ya safari kama atataka kurudi tena.

Kwa sasa hakuna njia ya mkato. Kuumia ni lazima utaumia lakini utavuka. Kwa kadri muda unavyokwenda maumivu nayo polepole yatapungua; na nati hizo zinazokaza kwenye moyo zitaanza kuachia na furaha yako itarudi.

Na ni lazima uchukue tahadhari. Usije ukaishia kuchukia wanawake wote. Huyu hakuwa wako na imeonyesha hivyo. Hata kama ungelazimisha basi huko mbele ya safari ungeumia zaidi ya unavyoumia sasa. Angalia tu usije ukaenda huko ukilalama na kuita kila mwanamke ni laghai, mbwa na malaya. Hutakuwa sahihi. Na siku moja utakuja kumpata aliye wako ambaye atakuonyesha mwanamke mwema na waifu matirio yukoje. Endelea kumtafuta mwanamke huyo kwa roho njema, moyo safi na dhamira isiyo na mawaa na siku moja utampata tu.

Sasa umekua! 👏🏼👏🏼👏🏼💪💪
Aisee,, ushauri mzuri
 
🫡🫡🫡 make sure wewe ndiyo unapendwa kwenye mahusiano yatakayo fuata.Wewe ndiye provider,wewe ndiye unaye amua kuoa tena sio kinyonge. A woman should be begging you to marry her,hii Mungu amekuepushia zahama maana wewe ndiye ulikua the weak person kwenye mahusiano.

Mwalimu inaonekana kuna mwamba ambaye yeye anampenda sana na amememtingisha kwamba kuna stranger (wewe) anataka kwenda kutoa mahari. Mtu katingishika kweli mpaka imebidi uambiwe vuta handbrake wakati anayependwa akisubiriwa kutimiza ahadi yake . Hii inaitwa multi-dating,ungepewa ruhusa ya kwenda kutoa posa kama plan A yake ingefeli.
Hahaa sawa mkuu nimekuelewa sana.

This time around hakuna mzaha tena aisee.
 
Good! Mungu akusaidie ufute kila memory yake ndio utamsahau na kumove on!

Au waza mabaya yake kwasana ( Kama yapo) itasaidia kukuketea relief ya maumivu!
Nimependa hapo kwenye kuwaza mabaya yake, na alikuwa nayo kama mimi nilivyokuwa nayo. Sema nilichagua kumvumilia.
 
Back
Top Bottom