Nimeambiwa na mpangaji mwenzangu kuwa tunatakiwa kuchangia kila mmoja Tsh. 30,000/-

Nimeambiwa na mpangaji mwenzangu kuwa tunatakiwa kuchangia kila mmoja Tsh. 30,000/-

Changisha alafu ununue wewe na uweke wewe uone kama utaisha huo umeme wa elfu 60 mimi nina AC na taa tisa na simalizi umeme wa elfu 50 unit 140.4 na pasi napiga nnavyotaka na friji linaunguruma halijawai kuzimwa
Tanzania hii hii ama? Kuna watu mnabahati sana aisee
 
Ndio maana napenda nyumba ambayo choo umeme maji vyote natumia peke yangu

Kweli 10k ni units 28 lakini kwa appliances ulizotaja mwenzako anakupiga changa

Kama unajimudu tafuta nyumba ambayo umeme choo maji unalipia mwenyewe sio Kushare
 
Hama hapo. Usipende kupanga na wanawake mkashare luku. Bora upange nyumba yenye masela wakuiume wengi au panga apartment ya luku yako tu. Wanawake kila kitu ni umeme, anaoga maji ya moto, fridge anawasha full time, akitoka kuoga anakausha nywele kwa mashine ya umeme, ukiwahi kuondoka asubuhi yeye azimi taa za nje anaacha on 24/7, kila nguo anapiga pasi, usisahau feni anaacha inapepea wakati huo hayupo nyumbani mwisho kama kunakisima hapo tegemea mda wote Pedrolo pump ipo on kujaza maji kwenye tank.

Umesahau kuwa na fimbo zikitembea sana usiku asubuhi lazima achemshe maji kukanda donda yaani kupanga na wadada zetu ni shidaaa na hasa kama huyu anakula na mwenye nyumba na ndio wakaja na suluhisho la kumkamua jamaa, hapa naona option zipo mbili tu moja kununua hicho kidudu cha kusoma units anazotumia yeye na kulipa accordingly/kuwa na luku yake separately au Kuhama nyumba na kumwachia mzigo huo kicheche wake ambaye ni mwenye nyumba
 
Nimeambiwa na mpangaji mwenzangu kuwa tunatakiwa kuchangia kila mmoja sh.30000/- kila mmoja yaani umeme wa sh.60,000/- ndiyo unatosha kumaliza mwezi eti kwa kuwa kila mmoja ana TV screen na kwamba kwa Siku TV moja inatumia units mbili,naomba anayeujua ukweli aijuze tafadhali!

raha ya kupanga bora ukute mita yako na choo chako.hivo vituko lazima vikukute
 
Umesahau kuwa na fimbo zikitembea sana usiku asubuhi lazima achemshe maji kukanda donda yaani kupanga na wadada zetu ni shidaaa na hasa kama huyu anakula na mwenye nyumba na ndio wakaja na suluhisho la kumkamua jamaa, hapa naona option zipo mbili tu moja kununua hicho kidudu cha kusoma units anazotumia yeye na kulipa accordingly/kuwa na luku yake separately au Kuhama nyumba na kumwachia mzigo huo kicheche wake ambaye ni mwenye nyumba
Asante kwa ushauri
 
Ndio maana napenda nyumba ambayo choo umeme maji vyote natumia peke yangu

Kweli 10k ni units 28 lakini kwa appliances ulizotaja mwenzako anakupiga changa

Kama unajimudu tafuta nyumba ambayo umeme choo maji unalipia mwenyewe sio Kushare
Asante sana!
 
Hahaha unataka kugeuzwa kuwa fursa shtuka aisee

Halafu waweza kukuta huyo jirani yako nae yupo hapa anachangia huu Uzi wako
 
Kipindi nakaa gheto (chuo) nilikua natambulika kwa ubishi. Bila ubishi watu watakutumia sana. Hata 10k kwa mwezi ni kubwa sana kuliko matumizi yako. Lipa elfu kumi tena ikiwezekana nunua mwenyewe weka umeme kwenye luku. Ukiishia njiani vunga mwenye shida ya umeme ataweka. Mimi nilikua nna pasi tu chuo. Ila majirani zangu walikua na rice cooker, jug la kuchemshia maji, fridge kuna mpuuzi mmoja alikua hadi na microwave alafu umeme ukiisha wananigongea eti hela ya umeme wote lazma tuchange sawa 😂😂😂. Niliweka mgomo mpaka mwenye nyumba akaweka personal meter. Ongea na mwenye nyumba awaekee au uweke mwenye ukate kwenye kodi. Sidhani kama inafika laki.
 
Mie natumia umeme wa tshs 50,000 ,vifaa vyangu,fridge masaa 24 kubwa la lts 240.taa za nje za sensor zipo 8,jug kuchemshia maji ya kunywa kila siku ndoo ya lts 20,pasi nguo nne kila siku,tv kuanzia saa 11 jioni mpaka saa tano usiku,rice kuka kwa wiki mara 5.simu na magari ya watoto yanayochajiwa.pump ya kisima dk 30 kila siku.
 
Asante sana kwa ushauri!Nadhani nitafute makazi mengine
...Uhame Kwa ajili ya Mpangaji mwenzio? Inaonekana na wewe hujiamini!
Labda ndio umetoka Kwa Wazazi ndio inaanza kupanga!
Unashindwa kuniambia Mpangaji Mwenzako atoe Alfu 10 na wewe Alfu 10 m nunue Umeme wa Alfu 20 Kwanza muone utawafikisha wapi!
Angekuwa ndio mwenye Nyumba je?
 
2020 sitii neno i hope mtoa mada alishahama hapo
 
Back
Top Bottom