Tetesi: Nimeambiwa ni bilioni 300 zilitumika kuweka mabango ya Rais Samia nchi nzima

Tetesi: Nimeambiwa ni bilioni 300 zilitumika kuweka mabango ya Rais Samia nchi nzima

Mnashinda salama mna raha gani humu jukwaani?

Haya ndugu zangu, nimepewa info kuwa yale mabango ya kumsifia boss kuwa anaupiga mwingi yaliyojaa kuanzia kila kona ya DSM na mikoani kila kona yamewekwa yamegharimu bilioni 300.

Tukiwaambia hafai tunaonekana hatuna adabu. Yaani unapeleka bilioni 300 kwenye mabango huku watu wako wananuka shida.

Yaani roho yangu inaniuma sana. Sijui niseme nini imefika mahali nimekua na chuki kali juu ya haya yanayoendelea kwa sasa.

Unatumia vipi bilioni 300 kuweka mabango ya kusifia ilhali watu wanakufa bila dawa hospitalini? Mungu tulikufanyia nini sisi? Daaaah!!
Akina makamba na mwigulu ndo waliofadhili huu ujinga ili mwanasesera aoneka mchapakazi kuliko mtangulizi wake
 
Ila hata mwendazake nae alikuwa amesambaza sana mabango,na kuna yale ya bwana Mwigulu
Ya magufuli yalikuwa ya uchaguzi yaliyowekwa na chamaa ndo ya kaendelea hadi huko, halafu yalikuwa ni ya kawaida sana huyu amewekewa hadi graphics za mabango kuonyesha utukufu wake sio sawa kabisa
 
Sasa mkuu umeambiwa tu na wewe pasipo kufanya tathmini yako unakurupuka kusema bilioni 300 kweli?

Hivi kweli bil 300 zitumike kwenye mabango?

Yes, mabango yanaweza kuwa na gharama lakini sio ya 300 bilioni.
Ww uafikiri lile bango ni shi 1m moja
 
MUNGU ameamua kuingilia Kati.
Kuna Kila dalili ukombozi utaanzia Mbeya Kwa Wanyakyusa.

Alianza Mwakyembe kujitokeza adharani Kupinga ushoga unaoenezwa Kwa kutumia fedha nyingi kutoka NDANI na nje ya nchi huku Serikali ikiwa imekaa kimya Kwa kuogopa kunyimwa misaada.

Lakini Kuna yule Askofu anayezunguka kwenye mikutano ya Kudai Katiba Mpya.
Kuna mwingine Anaitwa Mbarikiwa .

Mbeya watawaamsha waliolala SIO muda Mrefu.
Mungu anafanya kazi na watu jasiri.

Hata teknolojia na maarifa ni mafunuo ya kiroho Kwa watu jasiri wenye maono maakibwa ya kuubadilisha ulimwengu. Ni watu wachache lakini wasio na woga na hawakati tamaa.

Tukiamua tunaweza .
Jambo la kwanza ni kutafuta watu Milioni Tano Nchi Nzima na kuchangia elfu mbili mpaka Kumi Kwa mawakili na wanaharakati Ili kuwalinda na kuzitunza familia Zao.
Tukichelewa Mafisadi yataunda vikosi vya kuteka watu na vikundi vya kigaidi na kuwanyanganya mawakili leseni zao Ili wawe na woga kutokana na kuingia kwenye maisha magumu na Umaskini Wa kukosa vipato.

Tuwachangie Kwa hamasa kubwa kuokoa nchi Yetu kama wanachama Wa Yanga walivyoamua wakati Fulani kuiokoa timu yao.

Tayari nchi imeshavamiwa na Wezi Toka nje na wamefanikiwa kupenyeza fedha nyingi Ili kuhalalisha uvamizi Wao Kwa kuwatumia Waandishi Wa habari na wasanii na makada feki Wa CCM.
Tunajitahidi kuwashika mikono lkn suala la kuwadhuru kidogo ni ngumu sio rahisi na uhakika na nachokisema.

Ndani ya mfumo sio wote wanaofurahia huu uwizi unaoendelea hata kuvuja kwa mkataba wa serikali yetu na DPW ni wenye nia njema waliopo kwenye mfumo la sivyo tungeshaumia zamani, ko hata litakapotokea kundi la kutaka kuwadhuru mapema sana hyo mipango miovu itajulikana mapema
 
Wanaomshauri ndo tuwashukuru sana maana nimeona wazi kabisaa wanamshauri kimkakati kwa malengo wanayoyajua wao
Uwanja Wa Mkapa unakwenda kukarabatiwa Kwa Bil. 31.
Wakisha kuukarabati watawapa Wachina wachukue mapato mana watanzania ni Wezi.
 
Sasa mkuu umeambiwa tu na wewe pasipo kufanya tathmini yako unakurupuka kusema bilioni 300 kweli?

Hivi kweli bil 300 zitumike kwenye mabango?

Yes, mabango yanaweza kuwa na gharama lakini sio ya 300 bilioni.
Lisilowezekana kwa wengine kwa CCM linawezekana.ccm ni zaidi ya covid
 
Yesu....🙆‍♂️
Sema ni Bwana, muunge mkono shekhe mstaafu🤣🤣🤣
20230801_175333.jpg
 
Ila hata mwendazake nae alikuwa amesambaza sana mabango,na kuna yale ya bwana Mwigulu
Mabango ya jpm hayakuwa na budget hiyo, ni yale yale yalitumika kipindi cha uchaguzi. Hakuwa mtu wa kuunguza pesa namna hiyo.
 
Mnashinda salama mna raha gani humu jukwaani?

Haya ndugu zangu, nimepewa info kuwa yale mabango ya kumsifia boss kuwa anaupiga mwingi yaliyojaa kuanzia kila kona ya DSM na mikoani kila kona yamewekwa yamegharimu bilioni 300.

Tukiwaambia hafai tunaonekana hatuna adabu. Yaani unapeleka bilioni 300 kwenye mabango huku watu wako wananuka shida.

Yaani roho yangu inaniuma sana. Sijui niseme nini imefika mahali nimekua na chuki kali juu ya haya yanayoendelea kwa sasa.

Unatumia vipi bilioni 300 kuweka mabango ya kusifia ilhali watu wanakufa bila dawa hospitalini? Mungu tulikufanyia nini sisi? Daaaah!!
tuliza tako we mmbea na uzushi wako. Hata zimetumika ni za mamako? Kumpongeza rais wetu we unawashwa na nini.
 
Wezi haswaa
Wezi wanapaswa kufungwa gerezani .
Kwa nini hawakamatwi ?
Ina Maana Kuna mkubwa yupo upande Wa Wezi ?

Bil. 31 zinakwenda Kukarabati vyoo na Viti pale uwanjani ???
Wizi mtupu!!
Bil 7 zingetisha kabisa .

Vitu vidogo vimewashinda kutokana na kukosa MTU Wa kuchukua hatua na si vinginevyo.
 
Back
Top Bottom