Nimeambiwa nichague kituo cha kazi cha kudumu Tanga mjini au Singida mjini, Je nihamie wapi ?

Katika mikoa nchi hii ambayo niko tayari kuishi hata ukinikurupua leo kesho basi mmojawapo ni Tanga, binafsi hadi nakutamania kupangiwa huko maana kwa sasa nimepachoka Dar, na kuna mikoa ambayo ni kipaumbele changu baada ya Dar ikiwemo Tanga huko
 
Kama unaajira umesema nenda Tanga tu ila hao wanaokwambua Kuna fursa za kutosha, Ni uongo kama Boda Boda saa mbili wanaenda kulala na hiace zao.
Mkuu sijajua unazungumzia mitaa gani au mara ya mwisho wewe kuwepo Tanga Mjini ni lini, ila mimi wiki iliyopita nilikuwa huko na itoshe kusema baadhi ya maeneo mida ya usiku pamechangamka sana, kuna mahali nilienda kupata nyama choma na vinywaji hadi mida ya kama saa sita hivi na boda walikuwepo wa kutosha tu
 
Ta
 
Karibu kwetu Tanga mkuu.
Sisi ni wakarimu na tuliostaarabika.
Tumefunzwa adabu na heshima kwa wakubwa na wadogo.
Karibu pwani yetu.
Tutakupa ushirikiano.
 
Tanga Kuna fursa Gani potential za Muda wote? Kwanza sasa hivi ndio vyumba vimepanda Bei mpka elfu 80 Self, sababu ya Wageni wengi kwenye mradi wa BBN, tena hapo ni Sahare Raskazone, Hizo sehemu unazosema usafiri wa Hadi sa nane ni siku na siku kwenye Vishughuli, ni hapo bistro na likely, Gari za Tangabeach,Donge,Mikanjuni-Raskazone sa mbili na nusu zinaenda kulala, kadhalika na za kange ndio umeumia, Wadigo na wazigua kwenye biashara hawana haraka kabisa kukujibu sio riziki nenda kwingine, kawaida sana labda wasambaa,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…