Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Status
Not open for further replies.
Dah... Mkuu pole aisee Dah so sad.. nimehisi mwili umelegea na kuishiwa nguvu katika hili Dah!! Pole R.i.p Folk
 
Mkuu ndugu mbona haujafa au miezi hiyo minne haijafika tu?
 
Tuliowahi kukumbwa na hali kama hii ndio tunajua maumivu yake. Mimi mgonjwa wangu nilikataa kumtoa mpaka alipofariki hapo hapo hospital.

 
Nimesioma thread hii very late sana; ikanikumbusha kwa uchungu sana ndugu yangu aliyekutwa na aina fulani ya kansa, daktari akatuambia kuwa ana masaa 36 tu. Hata hivyo jamaa alikuwa na amani tele na mchangamfu daima na akaishi kama wiki nzima ila siku za mwisho zikawa za mateso sana kwani alikuwa hawezi hata kuongea na ilipofika siku ya saba tangu dakari atupe masaa 36 amri ya bwana ikatimia.

Nimesoma kwa machungu sana, lakini ndiyo hivyo; kama ni kweli, basi RIP Folk wetu.

Itakuwa ni vizuri pia iwapo modereta atabadilisha classification kuwa RIP kusudi watu wasimtag tena. Nimemkumbuka tena dada Regia Mtema aliyekuwa active sana hapa akafariki kwa ajali ya gari.
 
Dah, inauma sana. Mwenzetu kapitia mateso makubwa ila kaufaham mwisho wake na najua alijinyenyekeza kwa mola wake. Mpaka kupata mda wa kuaga watu ni dhahiri kua ni mtu mwenye bahati sana ya kutubia dhambi zake.
Wengi wanakosa hiyo nafasi kwani mauti yamekua yakiibuka ghafla bila kujiandaa.

Bwana akurehemu na akupe maisha ya milele ya amani.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…