Nimeambukizwa virusi vya UKIMWI (H.I.V)

Kaka wakishacheki viral load wakiona ipo chini na CD4 zimebalance vizuri unaweza ukasimama kumeza dawa au bado zoezi la dawa litaendelea kama kawaida..
 
Kaka huu ugonjwa nimeupata mwaka huu mwez wa saba, nimegundua mwez wa kumi baada ya kujipima, nimeanza ARV's wiki moja nyuma. Kwanin mnabeza
Wewe!

Ulianza kutumia ARV za nini kama tayari afya yako sio mgogoro!?

Yaani ungeishi kawaida hata usingeugua kabisa!!!
Aliekuambia upime kwa ajili ya Nini!?
 
Nyie walokole mna tabu sana,

Huu ushauri wako ndio utamponya muhusika? Haya nenda kwenye Mahospitali ukawaombee wagonjwa wote ili wapone na warudi majumbani mwao.
Sijatoa ushauri wa kuponywa,
Yeye amtafute Mungu kwa bidii
Kuna utofauti wa kutafuta uponyaji na kumtafuta Mungu .
Watu wengi wanakimbilia uponyaji badala ya kumtufata Mungu
 
Huu ni utaalamu wa wataalamu, sio rahisi mim na jamii inayonizunguka kulifahamu ili
Ndio uchunguze. Muda unao maana ni maisha yote so we kuwa mdadisi tu.

Hata kama sio kupona fanya tu kama uchunguzi maana udadisi ndo akili
 
Wewe!

Ulianza kutumia ARV za nini kama tayari afya yako sio mgogoro!?

Yaani ungeishi kawaida hata usingeugua kabisa!!!
Aliekuambia upime kwa ajili ya Nini!?
Nilivyofika hospital walivyonipima na wao pia wakagundua ilo tatizo wakanipa matumaini then wakaniambia inabid niwahi kuanza dawa ivyo kesho kutu uje tukuanzishie dawa ndio nikaanza dawa,

walinihasa sana kwamba ni vyema nianze dawa mapema kabla ya virusi havijazaliana kwa wingi mwilini
 
Kaka wakishacheki viral load wakiona ipo chini na CD4 zimebalance vizuri unaweza ukasimama kumeza dawa au bado zoezi la dawa litaendelea kama kawaida..
Zoezi la kumeza dawa ni zoezi endelevu kwa maisha yako yote kwa sasa..kwani..
Mpaka sasa bado hakuna dawa ya kutibu moja kwa moja kama zitapatikana huenda itakuwa heri zaidi....

Hata kama HVL itaonyesha kiasi kidgo Sana cha HIV kwenye Damu au kiasi cha chini sana ambacho ni undetectable (TND) Huruhusiwi kuacha dawa kwani iliyofanya mpaka kuonekana na kupata majibu hayo ni hiyo hiyo dawa..
Ukiacha dawa utasababisha kuibuka kwa Mutant viral Species ambazo ni Hatari sana kwa Afya yako kwani zinaweza kusababisha hata usugu wa dawa na mwisho kushindwa kwa matibabu..na mwisho wa siku unaweza kupata AIDS
 
Kama umeanza dawa ni vizuri uendelee usikatishwe na walimwengu maana maisha ni yako mwenyewe na wategemezi wako. Kuna jamaa kadhaa tuliwapoteza baada ya kukataa hizo dawa. Ikifikia umepata fangasi kwenye ubongo aisee ni ngumu sana tena sana kuinuka tena
 
Mkuu unapona kabisa na ata nikipima baada ya mwaka au miaka haisomi kitu. Kuna yeyote unayemfahamu aliyepona kwa muda mref still ni Negative
Najaribu kuitafuta namba yake hapa halafu nitaku PM
 
Wewe!

Ulianza kutumia ARV za nini kama tayari afya yako sio mgogoro!?

Yaani ungeishi kawaida hata usingeugua kabisa!!!
Aliekuambia upime kwa ajili ya Nini!?
Acha kupotosha umma mkuu!
Neno dogo unaweza kulisema likaleta athari kubwa sana ambayo Matokeo yake huwa ni Irreversible..

Na ndo maana Sera ya Sasa Tanzania ni TEST and TREAT na imesaidia sana kupunguza kiwango cha maambukizi nchini kwa asilimia kubwa sana tumetoka kwenye Prevalence ya 9%. Kwa mwaka jana tuna Prevalence ya 5.0% Hii njia imesaidia sana kupunguza maambukizi mapya ....kupitia 95 95 95 ambayo zamani ilikuwa 90 90 90
 
Najaribu kuitafuta namba yake hapa halafu nitaku PM
Nitashukuru mkuu, Nitajaribu njia za dawa mbadala lakin ARV's sitoacha kumeza adi nihakikishiwe na madaktari kuwa ni Negative again but bila ivyo nitaendelea na mfumo[emoji17]
 

Kujichunga ni ku abstain, then ndo hayo ma box, pole.

"mabox ya vipimo vya H.I.V rapid test ghetto"
 
mkuu inakuaje dozi ya PrEP iweze kuangamiza virusi vilivyoingia mwilini na wamesema havina dawa, au apo nimeshindwa kuelewa sawasawa
 
Nitashukuru mkuu, Nitajaribu njia za dawa mbadala lakin ARV's sitoacha kumeza adi nihakikishiwe na madaktari kuwa ni Negative again but bila ivyo nitaendelea na mfumo[emoji17]
Huyo Jamaa hataki hata kujitangaza hadharani lakini nikiipata namba ya ndugu yake nitakutumia.
 
Kujichunga ni ku abstain, then ndo hayo ma box, pole.

"mabox ya vipimo vya H.I.V rapid test ghetto"
ni ktk harakati ya kukikinga kitu ambacho saiz tayar kimeingia ndani ya mwili wangu tena kirahis kabisa
 
Imekaa kitapeli tapeli☹
 
Aliekuambia upime kwa ajili ya Nini!?
sasa shehe usipopima utajuaje hali ya afya yako?

ukipima ukajua hali yako ndo unaweza kujilinda we binafsi na kuwalinda wengine unaoshirikiana nao

nje ya hapo unaweza kuwa unaeneza hii shida kwa wengine bila kujua au unaleta mtoto duniani lakn ana maambukizi tayari sasa uo ni uchoyo na binafsi mkubwa hata mungu hapendi

linda kizazi hiki na cha baadae, acha kuishi gizani kapime ujue hali yako
 

Mkuu utaliwa hela zako?

Swali la kujiuliza kama kweli anaponya kwanini asiende CTC wapone watu.

Hizo Dawa zake zingekua zinaponya ungekua ushaona watu wanatoa ushuhuda! subir dawa walioifanyia utafiti huko ulaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…