Nimeambukizwa virusi vya UKIMWI (H.I.V)

Nimeambukizwa virusi vya UKIMWI (H.I.V)

Sijatoa ushauri wa kuponywa,
Yeye amtafute Mungu kwa bidii
Kuna utofauti wa kutafuta uponyaji na kumtafuta Mungu .
Watu wengi wanakimbilia uponyaji badala ya kumtufata Mungu
Mara useme Mungu,mara useme Yesu,

Mbona hueleweki?
 
kama ulikuwa na ratiba ya kuloweka leo, ukisoma uzi lazima ughairi
Ngwengwe noma
 
Habari wanaJF, mim ni kijana niliyekuwa ninajichunga na kuijari sana afya yangu kiasi cha kuwa na mabox ya vipimo vya H.I.V rapid test ghetto, ikiwa kama nimejichanganya bas nawahi dawa za PrEP,

Dawa za PrEP nimemeza round mbili yaani 2017, 2020 baada ya kucheza rough.

nilikuwa napima maambukizi na mwenza wangu mara kwa mara, Ivi sasa mwenza wangu anamalizia masomo ili mwakani July tuanze kuishi pamoja. sasa mwez Agosti mwaka huu nimekutana na mwanamke ambae tunameet na kusekx na uwa tunacheki afya sasa mwez huo nikapuuza kwakuwa tulicheki afya mwez May nikamla then maisha yakaendelea,

Mwez Octoba juzi tu nikajaribu kupima peke yangu ghetto nikakutana na mistari miwili CONTROL na 1, nilipima zaid ya mara tano apo apo gheto inasoma mistari miwili. Dah pressure ikawa kubwa.

Nikaenda Hospital napo inaonesha nipo POSITIVE, wakanianzishia dawa za ARV's adi sasa ninamaliza wiki tangu nianze dozi za ARV's. next wiki wananianzishia na dozi ya miezi sita ya Anti-T.B...

Juzi nipo YouTube nakuta kuna shuhuda nyingi sana kwamba kuna Mtaalamu anaponesha ili janga from POSITIVE to NEGATIVE anaitwa TR. MSIGWA, jaman waungwana kuna yeyote mwenye hakika na ili jambo ata ndugu yake alipata kupona kwa uyu docta maana kichwa kinawaka saiz sielewi, nikapata mawasiliano yake akaniambia dozi ni shilling 280k ya siku 45 inaitwa (4A9).

Wajameni ivi ili suala linaukweli dawa iyo ya Asili inasaidia kwa yeyote aliyawahi pata experience hii ata kwa ndugu yake kuhusu uyu mtaalamu TR. MSIGWA na dawa yake ya 4A9 maana ninawiki tu tangu nianze kumeza ARV's lakin naihis hali ya kuzichoka tayar. .

nawasilisha:
Kupima mara kwa mara ni dalili ya umalaya (kutojiamini)


Mtu asiye malaya huwa haangaiki kupima mara kwa mara

Shida kubwa ni mbususu (kilicho manyoya)
 
Hakuna tangazo ila ninawasiwasi na pesa yangu maana mzungu alishasema hakuna dawa itakayokurudisha kuwa Negative tena. nipo mkoani nawaza kuagiza maana matapeli ni wengi. Ninahamu na kuicheza hii kamali lakin ninamashaka.
Meza arv zako hakuna dawa hapo kama kweli unazo kula arv kula healthy tafuta ma detox ya ku cleanse In Figo na mwili kiujumla.
 
Habari wanaJF, mimi ni kijana niliyekuwa ninajichunga na kuijali sana afya yangu kiasi cha kuwa na mabox ya vipimo vya H.I.V rapid test ghetto, ikiwa kama nimejichanganya basi nawahi dawa za PrEP.

Dawa za PrEP nimemeza round mbili yaani 2017, 2020 baada ya kucheza rough.

Nilikuwa napima maambukizi na mwenza wangu mara kwa mara, hivi sasa mwenza wangu anamalizia masomo ili mwakani July tuanze kuishi pamoja. Sasa mwezi Agosti mwaka huu nimekutana na mwanamke ambae tunameet na kusekx na huwa tunacheki afya, sasa mwezi huo nikapuuza kwakuwa tulicheki afya mwezi May nikamla then maisha yakaendelea.

Mwezi Octoba juzi tu nikajaribu kupima peke yangu ghetto nikakutana na mistari miwili CONTROL na 1, nilipima zaid ya mara tano hapo hapo gheto inasoma mistari miwili. Dah pressure ikawa kubwa.

Nikaenda Hospital napo inaonesha nipo POSITIVE, wakanianzishia dawa za ARV's hadi sasa ninamaliza wiki tangu nianze dozi za ARV's. Next wiki wananianzishia na dozi ya miezi sita ya Anti-T.B...

Juzi nipo YouTube nakuta kuna shuhuda nyingi sana kwamba kuna Mtaalamu anaponesha hili janga from POSITIVE to NEGATIVE anaitwa TR. MSIGWA, jamani waungwana kuna yeyote mwenye hakika na hili jambo hata ndugu yake alipata kupona kwa huyu docta maana kichwa kinawaka sahizi sielewi, nikapata mawasiliano yake akaniambia dozi ni shilling 280k ya siku 45 inaitwa (4A9).

Wajameni hivi ili suala lina ukweli dawa hiyo ya Asili inasaidia kwa yeyote aliyawahi pata experience hii hata kwa ndugu yake kuhusu uyu mtaalamu TR. MSIGWA na dawa yake ya 4A9 maana nina wiki tu tangu nianze kumeza ARV's lakini nahisi hali ya kuzichoka tayari.

Nawasilisha:
Ndio inapona na Nina namba ya mhusika ,yupo iringa ,njoo inbox tuelewane nikupe namba
 
Wakuu sio lazima awe MSIGWA, mwenye experience ya mponyaji yeyote wa uyu mdudu anijuze,

sometimes naWish kama siku zirudi nyuma ifike mwez wa saba nimeze PEP mapema ila ndio ivyo nimeshachelewa.

now ndio nameza kidonge cha ARV iki ni kidonge cha nane tangu nianze kumeza.

uzuri hazijaniletea side effects zozote zaid ya kuhis kizunguzungu tu cha muda mfupi but nahis ni pressure ya mapokeo
 
Mdogo Angu soma hapa ni muhimu USIACHE Nitaandika maelezo marefu kwa sababu inahitaji kuongea zaidi ili uweze kuelewa plz nitajaribu kufupisha kadri navyoweza !

Polee Sana!

Matatizo tumeumbiwa binadamu,Kikubwa ni kuamini kwamba kila linalotukuta lina sababu Japo si Rahisi kuijua sababu kwa mara moja!

Kwanza kabisa Unaonekana bado upo kwenye denial na bado huamini kama Kweli unaweza kuwa na maambukizi, tuliza akili Mdogo wangu huu wakati ulionao ni wakati ambao akili yako bado haiamini kila kitu na inaamini sana kuwa bado muda unao na unaweza kupona na kuondoa Virusi hivyo mwilini..

Huu ni wakati ambao akili yako inaamini kuwa HIV ni kifo na kumbe swala hilo si la kweli!

Kwenye wakati huu wengi sana hupotea na tunapoteza Wengi kwa kukosa washauri wenye uelewa mzuri wa maswala ya maambukizi na wengi huamini kila kitu wanachoambiwa na kuona mitandaoni, Na huku wengine wakitapeliwa Pesa nyingi sana huku tatizo lao likibaki pale pale..

Huu ni wakati ambao unapaswa kutulia na kufata ushauri wa Daktari na washauri wengine mahali ambapo umeanza huduma ya Tiba na matunzo nafikiri kuliko wakati wowote ule....

Mpaka Sasa Si WHO, CDC,CRO, Medspace wala NIMR waliotangaza Dawa ambayo huenda ni mbadala wa ART..
Japo bado baadhi ya reseaech na procedure zinaendelea....

Kwahiyo ukitoa pesa ili kupata suluhisho la hilo tatizo lako utakuwa unaibiwa....

Na mdogo wangu naomba nikushauri katu asije mtu yoyote kukudanganya kuhusu Kuacha kutumia Dawa za ART kwa kigezo utumie Dawa zake...

Kwa sasa katika mwili wako kuna High production ya Virus wanamultiply sana na ndo maana ni wakati mbaya sana kuacha kunywa dawa!
HIV virus Si kirusi kinacho attack nutrients za mwili kwamba utakunywa dawa yenye protein ili kuzidisha protein na kufanya Waondoke mwilini...

NGOJA NIKUPE SOMO KUHUSU HIV NA DAWA ZA ART ZINAVYOFANYA KAZI ILI UPATE UELEWA KUWA ART NI BORA KULIKO HIZO MITISHAMBA

HIV Ni ina kirusi cha RNA na kinafahamika kama Retrovirus kwa kuwa kina tabia ya kujibadili na kuwa DNA kwa Kujichanganya Na vinasaba vya Mwili wa binadamu na hapo ndo huweza kubadili baadhi ya commands kwenye mwili na ku alter information za kawaida za mwili na kuamrisha mwili kutengeneza Wadudu ama virusi wengi kadri iwezavyo...

Utengenezwaji huu na upangwaji wa Virusi (Virion)
Hufanyika kwa haraka sana ndani na nucleas na nje ya nucleas ya Cells za binadamu katika hali hiyo cells nyingi hushindwa kuhimili Hali hiyo na nyingi huwa weak na kuharibika...sana sana hizi Tcells aina ya CD4 Kwakuwa ndiyo attachment yake na receptor au kufuli l funguo yake ndipo lilipo...

Kuna hatua kadhaa hufanyika ili kirusi kiweze kutengenezwa na kuharibu cells hatua hizo ni...
  • Kufungamana au kujishikiza kwenye cells ambayo ni cells ya CD4 (CD4 receptors- CCR5) kwa lugha nyingine huitwa Binding au Attachements
  • Kuungana au Fusion kirusi huingia ndani ya cells na kutoa vitu vyake vilivyo ndani..
  • Kujibadilisha kwa lugha nyingine huitwa Reverse transcription--kwakuwa RNA ni vigumu kuweza kufanya transcription (Kutoa order katika miili yetu kumbuka order hutoka kwa DNA na hutumwa kwa mfumo wa mRNA) virusi hufanya reverse transcriPtion yaani hujibadili kutoka HIV-RNA na kuwa HIV DNA na hapa ndo shida huanza..
  • Hatua inayofuata ni kujizalisha kwa wingi inavyowezekana ili kupata virusi wengi hatua hii huitwa Replication..
  • Kwa kuwa Ndani ya cells katika replication ni utengezaji wa material tu hatua hii hufanyika Kupanga material zote zilizotengenezwa huitwa assembly
  • Hatua ya mwisho ni budding ni kutoka kwa ile ile virus zilizotengenzwa ili zikomae na kwenda kufanya hatua hizo kwenye cells nyingine....
Nafikir umeelewa kuhusu hizo hatua zote...
Hakuna dawa yoyote ya mitishamba itakayozuia hatua yoyote kufNyika....
Sasa ART ina kazi moja wapo ya kuzuia hatua hizo kufanyika ili kuzuia uharibifu wa cells zaid na kuongeza kinga kwa kufanya hivyo...

Kuna dawa za ART Zinazuia kufanyika kwa...
binding/attachments tunaziita CCR5 antagonist pia zipo Post attachment inhibitors
Pia zipo zinazuia hatua ya Fusion (Fusion inhibitors)
Hatua hizi za mwanzoni huwa ni ART za sindano na kwa Tanzania bado hatujawahi kuwa nazo kwa sababu ni ghali...
Na hatua zinazofuata zote huwa na inhibitors zake..
Lengo la kuzuia HIV kufanya hivyo vyote ni ili ishindwe kuzaliana na Mwili utashughulika na HIV zilizokuwa weak na hazieleweki through engalf system ya macrophages..

Sasa kwanini nimekuambia yote haya kwa sababu ya kukujengea Kujiamni mwenyewe kuwa bado Una nguvu na wala Usiwaze kuhusu hicho unachowaza uko sawa na kutumia dawa kutakuweka katika afya nzuri sana..

Ukiacha kutumia dawa kwa hali yoyote ile utasababisha usugu wa Dawa (Drugs Resistance) ambayo inaweza kupeleka kufail kwa matibabu ya ART (ART drugs Failure) na ukifika huku inakuwa ni hatari sana...kwa sababu ART tena haitaweza kufanya chochote kwwnye mwili wako..

Kwahiyo jitahidi unywe dawa kwa wakati na baada ya miezi sita Angalia hali ya virusi kama unatumia dawa na lishe bora unaweza kujikuta upo kundi la watu walio na kiasi kidogo sana cha HIV (TND for HIV in HVL- Target Not Detected for HIV in HIV VIRAL LOAD)..

Najua ni Safari ndefu lakini ni fupi kama utajiamini na kuondoa hofu yoyote..
Asante kwa muda wako..
Na kama una swali unaweza kuuliza

NB: hakuna mtu aliyepima HIV positive baada ya muda akawa negative unless kafanya Bone Marrow transplant na yenyewe huwa ina 5% ya curetage...
[emoji120]
 
Back
Top Bottom