Nimeamini jamani hakuna kitu kigumu kama wajasiriamali

Nimeamini jamani hakuna kitu kigumu kama wajasiriamali

Wewe wajua nimezunguka taasisi 3 ili nizibe kwenye lile tatizo jibu nalokutana nalo corona.
Hata wale wadhamini tu wa kawaida nao corona imewagusa kiasi cha kwamba hakuna kitu kinachotendeka.
Naijua ile changamoto, ila chamsingi umesema utarejea mchezoni Mungu akubariki.
 
Hakika ni kumuomba Mwenyezi Mungu hili balaa lisiendelee kuiathiri Nchi yetu. Maana hapa biashara zangu fulani zilizokua zinanipa pesa ya kula nje ya mshahara wangu muelekeo wake sio mzuri kama hapo mwanzo.

Ni kuendelea kupambana na kumuomba Mwenyezi Mungu,kwa upande wangu sitegemei kuifunga itaendelea hivyohivyo mpaka pale hali itakapotengemaa tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole Sana'a mamii,ngoja nikutumie bas kidogo walau
 
[emoji28][emoji28]
Nimecheka sana niliposoma ile habari ya watu wa uganda waliowekwa karantini hotelini. Jamaa wameanza kuchakatana humo humo hotelini wanaume wamehama vyumba wamehamia kwa wadada..!![emoji23][emoji23]
 
Eee Mungu tunaomba toba na rehema, wewe ni Mungu unaerehemu, ni Mungu unaeponya, ni Mungu unaesamehe. Samehe Baba, ponya Baba na uturehemu pale tulipokwenda kinyume na mapenzi yako, Baba tunaomba utuvushe kwenye janga hili, tunajua kuna magonjwa mengi yanayochukua uhai wa binadamu lakini katika hili tumeshindwa Baba, dunia imejaa hofu na woga, dunia inaomboleza, hatujui mwisho wetu utakuwaje, Mungu tunaomba maisha yetu yarudi kama tulivyokuwa tukiishi siku zote, tumekutenda dhambi lakini Baba kumbuka rehema na uondoe ghadhabu juu ya nchi, watu wanaangamia kwa njaa, maisha magumu kwa kuwa hakuna kazi, watoto wanatamani kwenda shule lkn hawewezi tena, kumbuka rehema sawa sawa na neno lako kutoka Habakuki 3:1-2..Amen!
Amina

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii thread imenigusa sana. Wajasiriamali ni watu yatima hasa hawa wanaochipukia . Kwa TZ hatuna Serikali. Rais naye yuko pale kama mwajiriwa tu.. anamtegemea Mungu ..yani he cant think, he cant take advice, he cant impliment any precautions, na alipuuzia hadi tumefika huku.
Shit!
Rais hapaswi kulaumiwa kwa hili tupambane sote kwa pamoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huku nilipokuja nilitaka niingiwie na tamaa nikicheki mkaa gunia buku 8k, limao mmoja shambani bei yake ni shilling 10 ya kitanzania. Kuku ni kama bei ya singida tu.

Nikawaza nikawazua nikajisemea nikomae ni kitu kimmoja tu kilichonitoa dar na si kingine bali 'mawe'

Maana nikitaka vyote nitarudi kulekule kwa mwanzo.


Kwaiyo kama usemavyo ni vizuri ku deal na kitu kimoja tu.
Niunganishe hapo kwenye limao sokoni zimekuwa deal
 
Kuna mzigo niliagiza nje , Siku napata bill of loading ndo korona nayo imeshachangamka, halafu kibaya nilikuwa nategemea kulipwa na kiwanda fulani ili nipate kuukomboa mzigo bandarini, kwa bahati mbaya hicho kiwanda kimefungwa na mchina karudi kwako kenya , yani nimechangamyikiwa had basi
Meli inaingia tarehe Kumi ila wala sioni dalili za kupata hiyo pesa , nahisi kupoteza mzigo kwa storage na kodi
Hata kama tukipona korona itatuacha na umasikini uliotopea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shogangu alikuwa anategemea Hotel kuuza kuku wake wa nyama.
Sasa wiki ya pili hakuna biashara kuku wameshakula faida na kiasi cha mtaji alichofanya ni kuwachinja baadhi kuwaweka kwenye friza wengine amewajza na mabarafu kwenye madeli anatembea nao kwenye gari ikitokea zali njiani kakuta kibanda vha chips anauza.
Nawaonea huruma waliowekeza hela zao kwa Mr Kuku eti baada ya miezi 6 zina double mara mbili.

Sasa kama hizo hotels zimefungwa hao kuku watawauzia wapi.
 
Hii mbaya sana.
Pole mkuu
Kuna mzigo niliagiza nje , Siku napata bill of loading ndo korona nayo imeshachangamka, halafu kibaya nilikuwa nategemea kulipwa na kiwanda fulani ili nipate kuukomboa mzigo bandarini, kwa bahati mbaya hicho kiwanda kimefungwa na mchina karudi kwako kenya , yani nimechangamyikiwa had basi
Meli inaingia tarehe Kumi ila wala sioni dalili za kupata hiyo pesa , nahisi kupoteza mzigo kwa storage na kodi
Hata kama tukipona korona itatuacha na umasikini uliotopea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom