Nimeamini Kinachopiganiwa Gaza Ni Mafuta Na Gas

Kwa sababu ni weupe, ndio maana nimeelezea kwa kirefu, kwa sababu wengi huu mgogoro hawaujui, unaandika hoja mtu anakuita mvaa kobazi, mvaa dera, kichwani mweupe, haelewi dunia inaendaje ye kashiba wali na maharagwe anaona aandike anachoona.
Baadhi ya wajumbe humu JF ukiigusa Israel anaona umeigusa imani yake. Mwengine ukiigusa Saudi Arabia anaona umeigusa imani yake pia. Ili kwake kujipoza ndipo atakutolea maneno ya kejeli/kebehi.

Bw. James Comey huwa anasema mada kama hizi ndipo utakapoona uwezo wa akili wa watanzania.
 
Swali zuri mkuu 😀
We mkuu unaonaje? Naona ni suala la kulijadili kwa kina kabisa..
 
Hivi ni maisha magumu au watu mmegoma kufikiri?
 
Kabisa mkuu.
Gas ilyopo pale Levant basin inahitajika sana pale Ulaya baada ya jaribio la kutumia gas ya Qatar kupitia Syria kuelekea Ulaya kushindikana.

Wachezaji wakubwa hapo ni Israel kiongozi wao, Cyprus na Egypt, hao ndio wanufaika wakuu wakianza ujenzi wa bomba kwenda Ulaya.
 
Mkuu unaamini Trump akirudi madarakani itakuwa nafuu kwa Wapalestina?...

Umesahau namna alivyoutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel mpaka kuhamishia ubalozi wa Marekani huko, jambo liliowakera Wapalestina?....

Au nafuu unayoiona wewe ni vita kusimama tu ?
 
Russia hawezi kukubali ujenzi wa bomba kutoka Levant mashariki ya kati ilipo Gaza, Egypt na Israel kwenda Ulaya kum challenge. Hivyo ujenzi wa hilo bomba ungesimama na vita ya Israel na Gaza ingesimama.

Yanaweza kutokea machafuko lakini sio huu ugaidi wa kuua watu karibu 40K.
Trump alikuwa nafuu zaidi.
 
Haina shida mkuu, nilikua najaribu kuelezea ni sababu kuu ya vita inayoendelea.
 
kaka

naona shambulio la oktoba 7 lilikuwa la kimkakati huenda kulikuwa na mamluki wa kiyahudi kuanzisha vita au shambulizi.

nchi za asia wanahasirika vibaya mno.
Inaelekea kwa sababu miezi miwili nyuma kabla ya Oct 7, USA ilianza ujenzi wa kambi pale Negev Israel.
Haya mambo ya ajabu sana mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…