Andiko zuri sana, lakini wote humu tumeshihudia kilichotokea, tumeona kwa macho yetu, ni kweli dunia huwa inafake matukio ili kufanikisha tukio fulani, lakini kwa hili la Gaza tuachane na hadithi za kutunga uongo kuufanya ukweli, ukweli kuufanya uongo. Sababu inayofanywa vita iendelee huko Gaza ni 1. Dini 2. Iran. Kwa mazingira hayo Israel hana chaguo lingine mbali na kuhakikisha Gaza inarudi nyuma miaka 50 na kutoa funzo kwa Hamas. Israel alishasema siku hamas wakiachia mateka siku hiyo hiyo vita itasitishwa. Wao waendelee kushikilia hao mateka lakini wapalestina watalipa gharama kubwa sana, sasa hizi hadithi za mafuta hazina mashiko 1% . Shida ni moja Hamas wanataka kulazimisha Israel ikubali matakwa yao na wakati hawana uwezo wa kulinda eneo la Gaza.