Nimeamini Maisha si kombolela, nimepata akiba ya Tsh. Milioni 14.7 mwaka huu

safi sana mkuu sio wote tunaoweza kujibana kama ulivyoweza wewe
 

Safi sana mkuu ingawa sijasoma mpaka mwisho,, nitarudi kusoma
 
Sasa hiyo nayo hela ya kuianzishia thread?
 
Sasa kazinywee pombe ustarehe (kula bata) na malaya wa nje uwawache mkeo na wanao hawali matunda ya kuteseka kwao.
Hapo kwenye kuzila na Malaya ndipo wanaume tunapokosea na kupiga mweleka halafu tunasingizia tumelogwa. 😂 😂 😂 😂
 
Duuu yani umevundika ela badala ya kuizalisha.byebye
 
Yaani unapata 2.5mil kwa mwaka kwa investment ya 25mil. Mwee sii bora ukanywe bia tuu
Kwa kweli tumeumbwa tofauti sana nashangaa niwekeze mil 25 nipate marejesho ya milion 2.5 kwa mwaka wakati kuna harakati kibao ukifanya serious hiyo ni pesa ya faida ya miezi miwili au mitatu tu tena kwa mtaji usiozidi milion 5.

Watu tunatengeneza 1mil per month kwenye uwekezaji wa vipesa vya kawaida kabisa , ishu za kuwekeza kwa taasisi zinapaswa kuwa za pesa ya ziada kabisa. Mwanao anapaswa kurithi assets not money in banks ambazo anaweza hata asijue namna ipi azitumie. ataishia kuzila
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…