babukijana
JF-Expert Member
- Jul 21, 2009
- 14,478
- 18,341
Dah hizi mada za usiku
Lakini shida yote hii ya nini? Yaani ni ubahili tuu wa kumtoa Dar labda mpaka Morogoro, Dodoma au Arusha wakati mwenyewe kaacha maelekezo? Labda itokee hakuna mwenye uwezo kabisa wa kuchangishana na kukodi gari.
Asikudanganye Mtu popote pale ulipo kuwa Kauli za Watu waliokufa namaanisha Marehemu wakizisema huwa hazitimii. Ni kwamba huwa hawatanii kabisa na wayasemayo hutokea na hutimia.
Mwaka jana nilihudhuria Msiba Mmoja ambapo kumbe Marehemu wakati anakata Roho alisema akifa azikwe Dar es Salaam na Ndugu wakampuuza wakamsafirisha wanafika tu Segera wakapata Ajali na wale wale waliolazimisha asafirishwe Wakafa na Msafara ukageuka na kuja Kuzikwa Dar kama ambavyo Marehemu aliagiza.
Mwaka huu Mwezi February kuna Marehemu alisema akifa tu asizikwe Dar es Salaam na akazikwe Kijiini Kwao na Ndugu walipolazimisha Kumzikia Dar es Salaam kwa Kigezo cha Kuokoa Gharama Jeneza lake liligoma Kubebeka ila baada ya muda tu Ndugu walipokubaliana asafirishwe kama alivyoagiza Jeneza lilikuwa jepesi mno Kubebeka na akasafirishwa Kijiini Kwake kwa Maziko.
Leo hii kwa wale Wakazi wa Chang'ombe Temeke nadhani Ajali mbaya iliyotokea Mataa na kusababisha Vifo na Majeruhi mmeisikia.
Ni kwamba Marehemu ambaye ndiyo alikuwa anasafirishwa kwenda Kuzikwa kabla ya Kufa kwa Hasira alisema kuna Watu Wawili katika Familia yake akifa hataki waende Kumzika kwani wakati anaumwa na Kalazwa Hospitali walishindwa kwenda Kumuona huku uwezo huo wakiwa nao isipokuwa Dharau na Kupuuza kuliwatawala.
Na katika Ajali hi ya leo ambayo ilikuwa na Msafara wa Gari kadhaa Gari ambayo imegongwa na Kuharibika vibaya ni ya Watu wale wale Walengwa Wawili ambapo wote Wamefariki huku Mmoja Viganja vyake vikikatika.
Hivyo basi baada ya Msiba huu kutokea Msafara wa kumsafirisha Marehemu umeendelea na wale Watu aliowakataa wasimzike nao Wanefariki hivyo Maiti zao zipo Mochwari kwa sasa ukisubiri Msafara ulio Safarini ukirejea ndiyo waanze Kuhangaika nao na Wawazike.
Hata hivyo kuna Mbinu moja nilipewa na Wabobezi wa Kusafirisha Maiti / Marehemu wenye Masharti magumu hasa ya Kusafirishwa kuwa mkianza tu Safari tafuta Jiwe Kubwa / Jiwe Dogo liweke juu ya Jeneza na Marehemu / Mwili hautowasumbueni hadi mnafika. Bado sijaiamini ila kama hapa JamiiForums kuna wenye kuijua zaidi watufafanulie tafadhali.
Jamani tujitahidi mno na sana Kuziheshimu Kauli za mwisho mwisho za Marehemu kwani nimeamini kuwa kwa 85% huwa zinatimia japo kwa 15% zinaweza zisitimie vile vile kama ilivyo kwa Chanjo ya UVIKO-19 ambapo kwa 15% inaweza isikusaidie na ikakuathiri ila kwa 85% huwa inasaidia Kukukinga.
Ulaya nako kuna vituko pia na mambo ya ajabu, ila kwa kuwa wao wametuacha kiuchumi tunaona km huu upuuzi hakuna.. Ni km huku mwenye nacho(tajiri) tunaamini kuna mambo hana, ukiambiwa anafanya utashangaa.. Au tajiri ana ruhusa ya kusema chochote na kuaminika kirahisi, sema wewe KAPUKJ sasaa[emoji23]Haya ndiyo mambo pekee waafrica tunayaweza
Huyu mtu wenu sijawahi na kamwe sitawahi mkumbuka,kwa lipi hasaa?Na nyingine akasema "Najua mtanikumbuka na tena mtanikumbuka kwa mema" kauli ya marehemu naona imetimia 100%
KumbeAkikataa kuzikwa eneo A, akang'ang'ania kuzikwa eneo B. Na ninyi ndugu kwa sababu za msingi sana mkaona azikwe eneo A msipate shida sana. Kukwepa hayo mabalaa tumeni ndugu mmoja wa Kiume eneo B akachukue udongo kidogo katika kisado aulete eneo A.
Mkichimba kaburi miminieni udongo mloleta kutoka eneo B, bakisheni kidogo. Jeneza likishawekwa chini kaburini ule muda wa kuweka udongo malizieni na ule mlobakisha.
Muhimu kukumbuka udongo ulioletwa ufike siku moja au zaidi kabla ya maiti kutolewa mortuary. Kwenyw udongo ule kuwe na mawe madogo madogo kadhaa. Chukueni jiwe moja miliweke kwenye gari itakayosafirisha maiti kutoka mortuary mpaka makaburini.
Baada ya shughuli yote kukamilika. Gari lililombeba marehemu lisiende nyumbani kabla halijaoshwa. Lioshwe na mtu/watu baki (wasio ndugu) prefferably kwenye Car Wash za mitaa jirani au mtoni. Yule ndugu aliefuata udongo eneo B asiende kwake moja kwa moja baada ya msiba, wengi hupitia Bar kuzuga zuga walau three hours hivi, ikiwezekana kulipia lodge akaoge huko kwanza itapendeza.
Kwa kauli hizi hata hizo mali zenu za urithi sitaki iwe ya baba au sijui nani sitaki natafuta zangu.Kifupi kauli zao hutimia.Nakumbuka nikiwa mdogo mama yangu mkubwa alikuwa na pesa na Mali zisizo hamishika lakini kea kuwa alikuwa na UGONJWA wa ajabu wa kujivua Gamba ( Kama mdudu) baadhi ya ndugu walimnyanyapaa. Sasa hivyo hivyo alisema endapo at ONDOKA duniani wasimsafirishe na watu fulani wasipewe chochote kutoka ktk Mali yake.
Kilicho tokea Alipofariki walilazimisha kusafirisha walipo Anza safari TU sanduku likatoka kwenye gari, mwili ukatoka kwenye sanduku ukaangukia mbalii! Naam toka SAA 3 asubuhi Hadi saa11:30 jioni hawawezi unyanyua hata kuusogeza Hadi pale walipo badili uamuzi wasimsafirishe ndo ukabebeka.
2. Wale waliokuwa wakimnyanyapaa kila aliye pewa Mali toka katika Mali zake alisepa hakuitumia hiyo Mali aliyopewa!
Juzi Kati nilienda kufuata maiti Mortuary sijui hili wala lile kumbe unaweza ambua makubwa.Kwanza nahisi kuumwa umwa hovyo since then.Uwekaji wa jiwe kubwa au dogo, hautengui maamuzi ya mwendazake. Ni vena kufuata maamuzi yake ili kuepusha maafa kwa wale wanaobatilisha maamuzi yake.
Jiwe huwekwa jirani na sanduku baada ya sanduku kupakiwa ndani ya gari, na huondolewa baada ya sanduku kushushwa toka garini. Kazi ya jiwe hili sio kuzuia ajali, bali ni kuiondoa nuksi au mkosi unaofuatana na mwili wa mfu.
Baada ya sanduku kushuswa ndipo jiwe huondolewa toka garini na kudondoshwa chini . Kwa kufanya hivyo, nuksi iliyofuatana na sanduku huondoka ndani gari pamoja na jiwe. Hivyo, gari litakuwa salama.
Hujawahi ona gari lililotoka kusafirisha maiti linapata ajali wakati linarudi toka safari?.
" Kalaga bahho."
Safi jamaa.tafuta CHAKO na wafundishe watoto wako kutafuta chao Mambo ya kusubiri kurithi tuwaachie wazawa wa uswahiliniKwa kauli hizi hata hizo mali zenu za urithi sitaki iwe ya baba au sijui nani sitaki natafuta zangu.
Kiufupi mambo ya Mila yana nguvu kuliko imani za dini za wazungu na waarabu .
Wakinga Zamani walikuwa wanatajirika fasta tuu kwa kutii imani zao lakini leo hii hakuna tofauti na watu wengine Kisa dharau za Mila na kukumbatia tamaduni za watu wengine.
Wanaondokaga na watu mkuu acha wenye watu was wakatafute we saidia kubeba tuJuzi Kati nilienda kufuata maiti Mortuary sijui hili wala lile kumbe unaweza ambua makubwa.Kwanza nahisi kuumwa umwa hovyo since then.
Sitokuja kwenda kufuata maiti zisizonihusu maana hii kitu nimefanya mara 2 kwa watu 2 tofauti nisiowafahamu ila tuu ni vifo vya mtaani kujifanya jirani mwema.
Acha UBINAFSI mkuu!!!!!Nikifa, mke wangu asiolewe (mbususu ibaki kama nilivyoiacha)
Hili utangoja sanaNikifa, mke wangu asiolewe (mbususu ibaki kama nilivyoiacha)
Nitarudi kama nsyuka kwa atakaye pinga.Hili utangoja sana
UshirikinaAkikataa kuzikwa eneo A, akang'ang'ania kuzikwa eneo B. Na ninyi ndugu kwa sababu za msingi sana mkaona azikwe eneo A msipate shida sana. Kukwepa hayo mabalaa tumeni ndugu mmoja wa Kiume eneo B akachukue udongo kidogo katika kisado aulete eneo A.
Mkichimba kaburi miminieni udongo mloleta kutoka eneo B, bakisheni kidogo. Jeneza likishawekwa chini kaburini ule muda wa kuweka udongo malizieni na ule mlobakisha.
Muhimu kukumbuka udongo ulioletwa ufike siku moja au zaidi kabla ya maiti kutolewa mortuary. Kwenyw udongo ule kuwe na mawe madogo madogo kadhaa. Chukueni jiwe moja miliweke kwenye gari itakayosafirisha maiti kutoka mortuary mpaka makaburini.
Baada ya shughuli yote kukamilika. Gari lililombeba marehemu lisiende nyumbani kabla halijaoshwa. Lioshwe na mtu/watu baki (wasio ndugu) prefferably kwenye Car Wash za mitaa jirani au mtoni. Yule ndugu aliefuata udongo eneo B asiende kwake moja kwa moja baada ya msiba, wengi hupitia Bar kuzuga zuga walau three hours hivi, ikiwezekana kulipia lodge akaoge huko kwanza itapendeza.