Nimeamini masharti ya marehemu wakiyasema kabla ya kukata roho

Nimeamini masharti ya marehemu wakiyasema kabla ya kukata roho

Safi jamaa.tafuta CHAKO na wafundishe watoro wako kutafuta chao Mambo ya kusubiri kurithi tuwaachie wazawa wa uswahilini
Mada hapa ni Marehemu na Masharti yao hii Mada yako sijui ya Wazawa na Urithi hapa imekujaje? Kuna Watu ni Wapumbavu hapa hadi mnakera na nashangaa kwanini UVIKO-19 imewachelewesha Kuwapeleka tu Udongoni.
 
Kifupi kauli zao hutimia.Nakumbuka nikiwa mdogo mama yangu mkubwa alikuwa na pesa na Mali zisizo hamishika lakini kea kuwa alikuwa na UGONJWA wa ajabu wa kujivua Gamba (Kama mdudu) baadhi ya ndugu walimnyanyapaa. Sasa hivyo hivyo alisema endapo at ONDOKA duniani wasimsafirishe na watu fulani wasipewe chochote kutoka ktk Mali yake...
Duh!!!. Wakatoliki tukizungumza habari za wafu na kusema kuwa wafu bado wanaishi ktk Ulimwengu wa roho kuna watu huwa wanabisha na kutuona sisi washamba tusiojua Maandiko lkn ukweli ndo huo kifupi yapo mengi tusiyoyajua kuhusu wafu.
 
Nani kakudanganya kuwa Wazungu nao hawana Tamaduni zao au Dhania kama hizi? Umewahi Kuishi nao huko Ulaya / Marekani?

Hapo ulipo Umezaliwa Tandale na sasa Unazeekea hapo hapo Tandale leo hii unataka Kutudanganya hapa mambo na Tamaduni za Wazungu wakati umeota kwenda Kutembelea na Kuishi huko huu mwaka wa 40 sasa hujafanikiwa.

Hopeless mkubwa Wewe!!
Unajua we ni lijinga?
 
Juzi Kati nilienda kufuata maiti Mortuary sijui hili wala lile kumbe unaweza ambua makubwa.Kwanza nahisi kuumwa umwa hovyo since then.

Sitokuja kwenda kufuata maiti zisizonihusu maana hii kitu nimefanya mara 2 kwa watu 2 tofauti nisiowafahamu ila tuu ni vifo vya mtaani kujifanya jirani mwema.
Usikate tamaa, endelea kuwa mwema.
 
Akikataa kuzikwa eneo A, akang'ang'ania kuzikwa eneo B. Na ninyi ndugu kwa sababu za msingi sana mkaona azikwe eneo A msipate shida sana. Kukwepa hayo mabalaa tumeni ndugu mmoja wa Kiume eneo B akachukue udongo kidogo katika kisado aulete eneo A...
Hii ni sayansi au ni imani
 
Lakini shida yote hii ya nini? Yaani ni ubahili tuu wa kumtoa Dar labda mpaka Morogoro, Dodoma au Arusha wakati mwenyewe kaacha maelekezo? Labda itokee hakuna mwenye uwezo kabisa wa kuchangishana na kukodi gari.
Ukiamua kutaka mbwembwe na masharti mengi basi ni vyema uache na bajeti husika (mfano fedha za kutosha kusafirisha mwili wako) siyo kusumbua watu na kuwalazimisha kukusafirisha kwa gharama.
 
Hiyo ya 'sitaki fulani afike siku nikifa' nimeshuhudia matukio mawili maeneo tofauti.

La kwanza ilikuwa mke alikula njama kumwua mumewe kwa sumu. Alihangaika kwa matibabu ilishindikana. Kabla hajafa akasema mkewe asisogee msibani. Kwa jeuri ya pesa alikodi polisi wakamsindikiza kijijini kumzika mumewe wakati muda wote wa kuumwa hakujali. Aliposogelea jeneza aiangalie maiti, marehemu alifungua macho live.

La pili ni ndugu waligombana. Mmoja akasema hata nife mdogo wangu asisogee kunizika.Siku ilipofika dogo akajitosa kwenda msibani. Kiangazi mvua ilinyesha na ilipiga radi ya kutisha. Bahati nzuri haikuleta madhara. Dogo akaondolewa eneo la tukio na mvua ikaisha jua likawaka.
 
Hiyo ya 'sitaki fulani afike siku nikifa' nimeshuhudia matukio mawili maeneo tofauti.

La kwanza ilikuwa mke alikula njama kumwua mumewe kwa sumu. Alihangaika kwa matibabu ilishindikana. Kabla hajafa akasema mkewe asisogee msibani. Kwa jeuri ya pesa alikodi polisi wakamsindikiza kijijini kumzika mumewe wakati muda wote wa kuumwa hakujali...
Duh! Noma aisee.
 
Ninayoikumbuka kuna mzee alisema sitaki siku ya kunizika mfanye mbwembwe kama sherehe kutokana na uwezo wa kifedha wa ile familia. Alisema anataka azikwe simple sio mambo ya vyakula, pombe n.k.

Sasa alipifariki watoto ni kama walifanya sherehe.. kitaa watu walihamia pale ni kula na kunywa. Siku ya maziko vivyo hivyo wakazika fresh.

Baada ya siku moja wakaja polisi wana kibali kwamba mtu aliyezikwa sio huyo. Kaburi likafukuliwa kuangalia kweli marehem sio wa familia husika. Ikabid waende tena mortuary kuchukua maiti yao na kuja kuzika kimya kimya bila mbwembwe.
 
Ninayoikumbuka kuna mzee alisema sitaki siku ya kunizika mfanye mbwembwe kama sherehe kutokana na uwezo wa kifedha wa ile familia. Alisema anataka azikwe simple sio mambo ya vyakula, pombe n.k. Sasa alipifariki watoto ni kama walifanya sherehe.. kitaa watu walihamia pale ni kula na kunywa. Siku ya maziko vivyo hivyo wakazika fresh...
Inamaana hawakumuangalia na kumkagua marehemu wao??
 
Back
Top Bottom