Kuna kisa kilitokea katika msiba wa mfanyakazi mwenzetu Tabora. Maeneo ya mirambo barracks kulikua na mochwari, tulipeleka nguo za marehemu kutoka kwake kwa ajili ya kumsitiri ili asafirishwe kwenda kuzikwa kwao kijijini, tulienda na timu ya staff hakuwepo ndugu yoyote
Tukaingiza jeneza ndani ya chumba cha mochwari, sasa ikafika wakati wa kumvalisha nguo marehemu, yule jamaa wa mochwari akaita staff wawili wanawake waingie na nguo kusaidiana kumvalisha marehemu, sisi tulibaki nje basi baada ya muda wale wenzetu wawili waliambiwa watoke nje sababu marehemu alikataa kuvaa nguo ikabidi sisi tuliokua nje kuingia na kusaidia kumvalisha marehemu na kumuandaa, yule jamaa wa mochwari akatuambia kuwa marehemu aligoma kabisa kuvaa walipoingia wale wadada.
Tulipoingia sisi tukamvalisha na akaandaliwa fasta ila tulikumbuka kuwa kati ya wale wafanyakazi wenzetu kuna mmoja alikuwa haelewani kabisa na marehemu ila ilibidi aingie sababu alikuwa ni kiongozi wetu.
Wakati tupo ndani tulikuwa tuna mdadisi mambo mengi yule jamaa anayefanya kazi mochwari akatuambia maiti zinakuaga na vituko vingi sana na pia kuna watu wanawapokea kama maiti mochwari na wanakuwa hawajafa ila jamaa alisema huwa anawamalizia au anawaacha wafe kiukweli kuepuka taharuki.
Alitupa stori ya bibi mmoja wa miaka zaidi ya themanini ambaye aliletwa mochwari kuhifadhiwa ila hakupoa na kuwa wabaridi na alikuwa akipumua kwa mbali na kila ndugu wakija kuchukua mwili kwa ajili ya kwenda kuzikwa ilibidi wawaambie ndugu wasubiri hadi waliposhirikisha wazee wa Mila ikagundulika kuwa kuna kipenzi cha huyo bibi alihitajika kumvalisha na kumsafisha bibi yake ndio mambo yawe sawa.