Nimeamini masharti ya marehemu wakiyasema kabla ya kukata roho

Nimeamini masharti ya marehemu wakiyasema kabla ya kukata roho

Akikataa kuzikwa eneo A, akang'ang'ania kuzikwa eneo B. Na ninyi ndugu kwa sababu za msingi sana mkaona azikwe eneo A msipate shida sana. Kukwepa hayo mabalaa tumeni ndugu mmoja wa Kiume eneo B akachukue udongo kidogo katika kisado aulete eneo A.
Duuh kwann iwe yote haya??

Vip mmoja akikosea?
 
Akikataa kuzikwa eneo A, akang'ang'ania kuzikwa eneo B. Na ninyi ndugu kwa sababu za msingi sana mkaona azikwe eneo A msipate shida sana. Kukwepa hayo mabalaa tumeni ndugu mmoja wa Kiume eneo B akachukue udongo kidogo katika kisado aulete eneo A.
Ndugu popote pale ulipo pokea Saluti yangu ya Kipekee kabisa Kwako kwa Elimu hii nzuri na Kubwa ambayo nakuhakikishia nimeipokea vyema na naamini Watu wengi pia wamefaidika nayo.

Ubarikiwe mno na Asante sana sasa Marehemu wetu Wabishi na wenye Masharti ya Kukomoana watatukoma kwani tumeshapata sasa Dawa yao ya Kuwatuliza Udongoni bila Kututesa na Kutusumbua pia.
 
Ulaya nako kuna vituko pia na mambo ya ajabu, ila kwa kuwa wao wametuacha kiuchumi tunaona km huu upuuzi hakuna.. Ni km huku mwenye nacho(tajiri) tunaamini kuna mambo hana, ukiambiwa anafanya utashangaa.. Au tajiri ana ruhusa ya kusema chochote na kuaminika kirahisi, sema wewe KAPUKJ sasaa[emoji23]

New Zealand wana mchawi wa taifa
Benfica wana laana ya kocha wao aliwaapiza jinsi walivyomkosea adabu hawatabeba kombe la ulaya miaka 100.. Mpaka sasa waishapoteza fainali km 5 hivi..
Kuna wachezaji ulayA wana imani za kiwaki, sikumbuki vizurii, km sikosei JT yeye alikuwa lazima wa mwisho kuvaa, ikitokea kavaa halafu mtu hajavaa atavua na kuvaa upya.

NOTE. sisemi naamini hizi imani, ila nasema zipo duniani koote. Si mzungu, muafrika, muhindi, wala mchina.
Kocha wa zamani wa Italia Marcello Lippi alikuwa anapanga kikosi kwa nyota zao za siku hiyo.

Hata uwe mchezaji mzuri vipi unaweza kushangaa siku 1 anakuweka benchi kisa nyota ysko siku hiyo haijang'aa

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
 
Uwekaji wa jiwe kubwa au dogo, hautengui maamuzi ya mwendazake. Ni vena kufuata maamuzi yake ili kuepusha maafa kwa wale wanaobatilisha maamuzi yake.
Jiwe huwekwa jirani na sanduku baada ya sanduku kupakiwa ndani ya gari, na huondolewa baada ya sanduku kushushwa toka garini. Kazi ya jiwe hili sio kuzuia ajali, bali ni kuiondoa nuksi au mkosi unaofuatana na mwili wa mfu.
Baada ya sanduku kushuswa ndipo jiwe huondolewa toka garini na kudondoshwa chini . Kwa kufanya hivyo, nuksi iliyofuatana na sanduku huondoka ndani gari pamoja na jiwe. Hivyo, gari litakuwa salama.
Hujawahi ona gari lililotoka kusafirisha maiti linapata ajali wakati linarudi toka safari?.
" Kalaga bahho."
Sasa hapa Unanielimisha vyema kama alivyofanya Mbobezi Puppy au Unanisuta? Miswahili bhana....!!!
 
Akikataa kuzikwa eneo A, akang'ang'ania kuzikwa eneo B. Na ninyi ndugu kwa sababu za msingi sana mkaona azikwe eneo A msipate shida sana. Kukwepa hayo mabalaa tumeni ndugu mmoja wa Kiume eneo B akachukue udongo kidogo katika kisado aulete eneo A.

Mkichimba kaburi miminieni udongo mloleta kutoka eneo B, bakisheni kidogo. Jeneza likishawekwa chini kaburini ule muda wa kuweka udongo malizieni na ule mlobakisha.

Muhimu kukumbuka udongo ulioletwa ufike siku moja au zaidi kabla ya maiti kutolewa mortuary. Kwenyw udongo ule kuwe na mawe madogo madogo kadhaa. Chukueni jiwe moja miliweke kwenye gari itakayosafirisha maiti kutoka mortuary mpaka makaburini.

Baada ya shughuli yote kukamilika. Gari lililombeba marehemu lisiende nyumbani kabla halijaoshwa. Lioshwe na mtu/watu baki (wasio ndugu) prefferably kwenye Car Wash za mitaa jirani au mtoni. Yule ndugu aliefuata udongo eneo B asiende kwake moja kwa moja baada ya msiba, wengi hupitia Bar kuzuga zuga walau three hours hivi, ikiwezekana kulipia lodge akaoge huko kwanza itapendeza.
Dooh!
Shida yoote hiyo, si bora tu kutekeleza maelekezo!
 
Kwa kauli hizi hata hizo mali zenu za urithi sitaki iwe ya baba au sijui nani sitaki natafuta zangu.

Kiufupi mambo ya Mila yana nguvu kuliko imani za dini za wazungu na waarabu .

Wakinga Zamani walikuwa wanatajirika fasta tuu kwa kutii imani zao lakini leo hii hakuna tofauti na watu wengine Kisa dharau za Mila na kukumbatia tamaduni za watu wengine.

Dunia ya Leo unakuta kijana anakomaa na mali za Urithi, what a shame
 
Haya ndiyo mambo pekee waafrica tunayaweza
Nani kakudanganya kuwa Wazungu nao hawana Tamaduni zao au Dhania kama hizi? Umewahi Kuishi nao huko Ulaya / Marekani?

Hapo ulipo Umezaliwa Tandale na sasa Unazeekea hapo hapo Tandale leo hii unataka Kutudanganya hapa mambo na Tamaduni za Wazungu wakati umeota kwenda Kutembelea na Kuishi huko huu mwaka wa 40 sasa hujafanikiwa.

Hopeless mkubwa Wewe!!
 
Back
Top Bottom