Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Vipi January bei ikifika sh ngapi ya mazao?Inategemea upo mkoa. Gani hapa Tanzania , kama upo mkoani jaribu biasharavya Nafaka msimu huu Mahindi yameanza na Bei rafiki sana Gunia la KG 110 ni 38000/ Hadi. 40,000/.
Nunua Mahindi Gunia 500 Kwa Thamani ya Tshs 20milioni ,
Then nunua mpunga Gunia 200 za debe kumi kumi Kwa Thamani ya Tshs 10Millioni ,
Alizeti Gunia 300 KG 70 Kwa Thamani ya Tshs 15Milioni.
Hifadhi Kwa muda wa miezi Sita , hapo ni January 2025 Bei zotakuwa. Juu sana Kwani Mazao yanakuwa hamna mashambani.
Mahindi unaweza uza Hadi Tshs 80,000/ mara 500 Gunia = 40milioni.
Mpunga Gunia 200 Mara 140,000/ = 28milioni.
Alizeti Gunia 90000/ mara Gunia 300 = 27milioni
Jumla ya kipato Kwa kuwekeza 45milioni Kwa miezi Sita ni 95milioni.
Option ya pili kama upo Dar es salaam nenda maeneo ya pembeni yanauokuwa Kwa Kasi Nunua ekari tatu za ardhi katika maeneo matatu tofauti then unapima. Viwanja baada ya mwaka Moja Hadi miaka miwili. Ekari Moja inatoa wastani wa Viwanja 10 vya kuanzia 400sq Kila Kiwanja utauza zaidi ya Tshs 4Milioni, hapo mchawi ni kwenye kupoint maeneo Gani yarayokuwa Kwa Kasi.
Hongera sana kakaNow 100ml asante Mungu
Duh, Kama ni Kweli basi hii nchi ni maskini sanaNi 0.1% ya watanzania wenye kuwahi kumiliki 100m kwa cash ni 5% ya watanzania wana miliki assets ambazo zinaweza kuwapa 100m.......95% ya watanzania ni hand to mouth economy. Hi mada hapa sio mahara pake.
Sawa ngoja nifanye hivoNi commitment tu. Jiwekee nadhiri kila kipata hela 20% nitawekeza ili mbele ya safari niishi bila stress
Kwanini unatoka kwenye hisa??Nimehamia kwenye hisa UTT Nina 700k only
Ni shughuli gani hizo unazofanya za kuweza kushika Mil 100??Mungu anisaidie, aniwezeshe kupitia jitihada zangu mwaka huu 2025 nishike Milioni 100 za kwangu mwenyewe.
Mungu wewe ndio kimbilio letu, wewe ndio Mkuu, unamuua unalotaka liwe na linakuwa, usiniache kwa ombi langu hilo kwa mwaka huu!
Invest in your hobby.Ngojeni kwanza mnafanya biashara gani wazee naombeni mnisaidie mawazo umaskini laana natamani niwe nazi na ninaamini nitazipata
Endelea kujipa moyo wa kilofa, hela ni hela mzee.Pesa za kurithi hazina utamu kama za kujitafutia.
Acha Mambo yako bhana 😂 😂Kati ya watanzania 100 mwenye ana account bank yeye kiasi zaidi ya 2.5 millioni ni 3 au 2
hongera sanaMafanikio huanzia rohoni.
Inategemea biashara zako,kazi,kilimo na mifugo.
Mimi kuna nyakati nilikuwa 0 lakini huyu Mungu ni FUNDI sasa namiliki meli kubwa za mizigo.
wazee tupeane michongo ata ww uko vzr mm sijawahi shika ata hio mil 10Noma sana aisee,yaan wakati sisi wengine ml 10 unaitafuta ndani ya miezi sita/zaidi tena kwa kukomaa kwel kweli[emoji23][emoji23]...halafu mtu ndani ya siku tano kainyaka daa[emoji3]
Lipia tangazo la UTIHabari wakuu,
Kiukweli kwenye haya maisha sio lazima ufundishwe kila kitu. Kuna wakati unafika unajaribu kupambana na kulifanya jambo fulani ndipo unakuja kujua mtu mwenye mafanikio ni wa kumheshimu sana. Ml 100 kwa kuzitamka zinaweza kuonekana ni pesa kidogo sana but in reality kuna baadhi ya wafanyakazi wanastaafu na hawajawahi fikisha kiwango hichi cha pesa.
Nimepambana kuinvest kwa upande wangu nimeamini kuwa na kiwango hicho cha pesa yataka moyo. Now mimi nimefikisha 56ml as cash na nimeinvest UTT.
Je, wenzangu mliofikisha kiwango hicho cha pesa mlifanyeje, na kwa muda gani? Tupeane uzoefu