Nimeamini USA ni kubwa la Dunia, Tamko la Trump tayari limeonyesha effect kwenye familia Yangu

Nina mwanangu alikuwa kwenye mradi anavuna milioni 5 kwa mwei, mradi ukaisha hata hela ya gesi, hela ya vitu vidogo, msosi wa mtoto ikawa mbinde, nilimoa sana kampani kipindi hiki, kapata kazi tena kasahau kila kitu 😂🤣
Hajaanza kujiwekeza?
 
Umemaliza kila kitu mkuu.
 
Hii hali imewakumba jamaa zangu pia, vipato vyao ni above average ila baada ya hiyo notice watu wanachanganyikiwa.

Kadri kipato kinavyoongezeka, matumizi yanaongezeka, usishangae mtu anapata 5m+ kila mwezi na anapewa notice ila Bank hana mia, scary!
 
Hajaanza kujiwekeza
Sina hakika, sababu sasa hivi sio km zamani, inaweza kupita miez 6+ huko hajakucheki, hata salamu ngumu, sasa katukuta sisi maskini jeuri, hatusaidii ili na wao watusaidie kesho la hasha, huwa tunasaidia sababu tunaona watu wetu wa karibu wametingwa(wana shida kushinda shida zetu) tunasaidia sababu sisi mtu akikunyooshea mkono wa kuhitaji, huwezi kuficha mkono wako mgongoni, nawe unamnyooshea kumpa kile kidogo ulichonacho, na wala hatusaidii sababu tuna vipato vikubwa la hasha, ni upendo ma huruma tu.
 
Hongera sana kwa moyo huo. Ila kama ulimbeba kipindi hicho ni heri kumkumbusha kuwa history repeats itself, hivyo ajiandae.
 
Pole sana mkuu.
 
Yaani mtu akikukatia msaada ndio inakuwa masimango hivi
 
Huo ni ujinga tu watu hawaishi maisha ya stahili yao wanang'ang'ana kuishi maisha ya wengine. shida sana hii hasa ukiwa na mke mpùmbavu mtaishia huku or worse.
 
Ndugu yangu anafanya kazi na masharika ya ukimwi yanayofadhiliwa na USAID... aliacha hata kutusalimia..akifikiri tutamwomba pesa.. hashiriki shughuli yoyote ya mchango wa familia.. nimeshangaa jana usiku amenipigia.. nikamwambia umekosea namba.. alikuwa mpole
 
Asa mbn mlalamika kwan haya maisha si yapo toka mwanzo au? au mnazungumzia kazi za unauzoefu gani katika kazii hii plus kama ulipewa kwa bluetooth ndo kasheshe
 
Polee sana Kiukweli Ni kwamba Tamko la trump limeathiri Uchumi wa nchi na watu wa Afya wanasikitika sana
 
kuna Familia bongo naifahamu kote kuchungu marekani na bongo..Kaka yuko miradi ya USAID hapa Tz, Dada ana overstay ya muda mrefu marekani.akidakwa tu bongo..Mama yao yuko roho juu ana amani..
 
Acha kujifariji wewe, nani alietumbuliwa kwa vyeti feki alirudi na maisha bora zaidi ya kutaharuki na wengine pressure ziliwapanda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…