Nimeamini wanaume hawaaminiki

Mimi naongea ukweli. Baba Cathe anampenda mkewe, wewe unavutiwa na mapenzi yao. Hivyo acha kwenda kwao Kila siku
Labda navutiwa bila mimi kujijua nisikubishie sana.
Sitoenda tena kwao.
 
πŸ˜πŸ˜„πŸ˜ƒπŸ˜€πŸ€£πŸ€£!
Mkuu hongera kwa msimamo, nimefurahishwa.

Nikuulize swali lenye mfano wa vitu labda utanielewa vizuri.

Ushaangalia documentary za wanyama, wale wakali kama nyati wenye pembe za kujihami, wakitakiwa na simba ushaona pembe hizo zinawasaidia?

Tuje kwenye miti, mfano wa mchungwa: una miba mikali, ushaona matunda yake yakashindikana kuchumwa?

Hizo 'big no' zako hizo mkuu kwa mwanaume ndiyo chachu ya kujitathimini na kujenga hoja, kukataa kushindwa pamoja na kutumia rasilimali zake awezavyo ili kulainisha.

Enzi zetu nikikutongoza ukanambia 'sitaki' basi lazima niibadilishe hiyo sitaki iwe 'nataka' kwa mbinu zozote zile ziwe halali ama haramu.

Yeyote aliyenambia 'sitaki', tayari nishampata, hata mke wangu alinileteaga hizo za sitaki tena na matusi juu, nilimwambia neno moja tu, 'tutaona', hadi leo ninaye nazeeshana naye.

Waliosalimika kwenye anga zangu ni wale wanawake watii na wajenga hoja ambao mimi ninawaheshimu sana.

Ninapomsimamisha mwanamke akanitii na kisha kujenga hoja ya kiakili kunitolea nje, hapo hapo uking'ang'anizi wangu huishia hapo.

Lakini kwangu wale watukanaji, wakimbiaji, wabaniaji wa namba za simu na wakali wenye nyodo wote nshapita nao, kwa sababu sanaa ya kutongoza huichukulia kama ligi ya Simba na Yanga kutafuta ushindi ambao hata goli la mkono hulitambua.
 
Mkuu umeongea points tupu lkn huwezi amini SijaelewaπŸ˜‚
Nitasoma tena baadae akili ikitulia
 
Ni kweli huwa mnawatongoza wenyewe wanawake
Mjifunze kuzuia tamaa zenu jamaniiiii
Wanawake ndio huanza kumtongoza mwanaume kwa mavazi sauti kujidai wako humble and care kuliko ulie nae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…