Nimeamini wanaume hawaaminiki

Nimeamini wanaume hawaaminiki

Sijafurahia na sijategemea hili kutoka kwake!
Uhalisia ni kwamba kutongoza ni tendo la mwisho, kabla ya hapo kuna mambo ya kibiolojia huwa yanatumika kama ishara ya kumwambia mwanaume huyu sasa ni wa kutongozwa, hayo mambo huyafanya mwanamke kwa kujua au kutokujua.

Hapo kwake hamkuwahi hata kugonganisha macho na jamaa ukatabasamu? Sema kweli.
 
Mimi sikubali mpk nikakipige kiberiti kilinge cha ustaadhi hawezi kula pesa ya mkinga bure 🤣🤣🤣🤣
Na huyo kungwi ajiandae nampokonya gold zake zote kufidia pesa yangu..!!!

Ss hivi tumlete kungwi kutoka Oman dada sitaki kuachika tena kwa babe mupya.!! 😂😂😂
Ila mi baby mupya Sina radhi nae ujue kabisaaaaaa......Mimi na Wizzy mpaka ufe akuzike...
 
Tatizo kuna wanawake mnapenda sana kutongozwa. Hata kama mnaona kabisa haiwezekani kuwa wapenzi utatengeneza mazingira tu utongozwe useme nilikuwa nakuheshimu mno halafu wakati mwingine muhusika akikazana sana unaachia unajikuta tayari mshavuana nguo mambo yanavurugika, urafiki unakufa au mimba hiyo hapo unavuruga familia ya watu sababu tu mnapenda kutongozwa.
Na 80% ya mshusiano huanzishwa na wanawake kwa makusudi yaliyo kamili, asilia 10 bila ya wao kujua na 10% ni jitihada za wanaume
 
Sijawahi hata kumuwazia
Na yeye hakuwahi hata kuonyesha dalili
Haiwezekani. Yaani ww kuadmire tu huko kulishana lishana na mkewe ni kumkubali na yeye kama mwanaume lazima atanotice kuwa unamkubali, shida ni kutafsiri namna unavyomkubali.

Inawezekana kabisa hukujua ila tukio la kukutongoza lilianzia kwako, hata namna ulivyokuwa unamuaga tu.. Ulikuwa unasemaje? Sheeeem, usiku mwema. Huwa unamuagaje?
 
Ila mi baby mupya Sina radhi nae ujue kabisaaaaaa......Mimi na Wizzy mpaka ufe akuzike...
Utazoea tyuuu!! 😂😂😂
Halafu huyo hatukuwa wapenzi, ni marafiki sie sema nyie ndo mlikuwa mnaona vibaya dada!!
 
Haiwezekani. Yaani ww kuadmire tu huko kulishana lishana na mkewe ni kumkubali na yeye kama mwanaume lazima atanotice kuwa unamkubali, shida ni kutafsiri namna unavyomkubali.

Inawezekana kabisa hukujua ila tukio la kukutongoza lilianzia kwako, hata namna ulivyokuwa unamuaga tu.. Ulikuwa unasemaje? Sheeeem, usiku mwema. Huwa unamuagaje?
Eti alikuwa anaaga "sheeeeeeem usiku mwema"Ulikuwepo?😂
 
  • Kicheko
Reactions: Tsh
Na 80% ya mshusiano huanzishwa na wanawake kwa makusudi yaliyo kamili, asilia 10 bila ya wao kujua na 10% ni jitihada za wanaume
Kabisa. Mwanaume mtongozaji maranyingi ni victim. Exception ipo kwa wabakaji tu. Ila mtu mnaonana mara nyingi asikutongoze day 1 aje akutongoze day 100 halafu mtongozwaji usihusike? Haiwezekani.
 
Bora wewe umenifariji
Hawa wengine wanamtetea Baba Cathe😂
Mimi hata Mungu anafahamu nini nakuwazia wewe ephen na namna navyotamani siku Moja nifanye jambo kubwa la kuuufanya hata moyo wako ukabubujikwa na machozi ya furaha ,kusema kumbe japo Dunia ni uwanja wa fujo na watu hawaaminiki na wamepungua upendo na utu lakini kumbe alikuwepo na yupo Lucas Mwashambwa katikati ya hao walimwengu mwenye roho ya upendo wa jua.
 
Habari!
Nimekutana na mkasa ambao umenifanya niamini wanaume sio watu wa kuwaamini 100%

Mimi ni mtu ambae muda mwingi najifungia ndani, lakini ikitokea nimekua mpweke sana huwa napendelea kwenda kwa jirani mwenye nyumba inayofuata baada ya kwetu.

Tumeshakua ni washkaji japo yeye ni mtu mzima kiasi, ana mume na watoto watano. Ila mimi na yeye tunaongea lugha moja. Mshkaji wangu namwita Mama Cathe. Anapendana sana na mume wake familia yao ni bora yenye upendo, kuwaona wamekumbatiana na mume wake ni jambo la kawaida sana.

Nipo karibu nae nimejua baadhi ya mambo, mume wake huwa anarudi kila siku mchana kula, mama Cathe huwa anamsubiri mchana ili wale wote saa 9.

Kwa jinsi wanavyopendana usiku wanaweka msosi nje wanakula mume, mke na watoto kulishana ni jambo la kawaida. Siku zote ninavyowachora mume anampenda sana mkewe, nilikua naona hawezi hata kumsaliti, hata michepuko haijui. Nilikua naamini kuna wanaume ni waaminifu na huyu Baba Cathe nilimuweka kundi hilo kwa jinsi wanavyoishi.

Juzi asubuhi mama kanituma nikanunue mahitaji, natembea zangu kwenye uchochoro mpana nikasikia mtu ameniita 'Ephen!' nikageuka nyuma. Nakutana na Baba Cathe akaniambia 'Nilikuona wakati unatoka nikasema nikufate sababu kila siku navizia nafasi ya kuongea na wewe lakini siipati, kwani unaenda wapi?'

Mpaka hapo nikawa nimeshangaa sikutegemea hii kauli kutoka kwake, hapo anaongea kimahaba
Huyu mzee nilikua namuheshimu sana....Nikamwambia naelekea dukani.

Akasema 'basi naomba namba yako siku yoyote naweza kukupigia tukutane sehemu X, huwa unanivutia sana nahitaji tuongee zaidi' nikamjibu sina simu

Alarm ikalia kichwani kwangu kua ule uchochoro yeyote anaweza kutokea ikawa kesi, sikumjibu nikageuka nikaendelea na safari yangu. Mimi nipo mbele yeye nyuma hapo natembea chap niumalize uchochoro akawa anaongea maneno ambayo siwezi kuyaandika hapa.

Nikamaliza uchochoro na yeye nahisi huku nyuma aligeuza, muda wote nikawa najiuliza huyu mzee kapatwa na nini?

Kilichonishtua ni jana nimekaa kibarazani na mkewe mida ya mchana, karudi mke wake akasimama kumkumbatia, huyu mzee akanikonyeza. Namuona anakuja kwa kasi!

Wanaume wote kumbe wanacheat.....!
Nilijua amekula mzigo tyr kumbe maongezi tu sasa fanya hivi ww muite then mrekodi maneno yote then mpelekee mkewe
 
Point ni kwamba
Nilikua nina imani kuna wanaume watulivu
Jinsi baba Cathe anavyomtenda mke wake vizuri nikajua kweli wanaume watulivu wapo 100%

Kitendo alichokifanya kwangu kimenifanya nione mwanaume anaweza kua mwema kwa mkewe lkn ana makandokando kayaficha bila kuonesha dalili yoyote.
Huenda mke wake anajua kila kitu sema watu wa zamani wana vifua wameamua kuwaonesha upande mwema kwao
 
Mimi hata Mungu anafahamu nini nakuwazia wewe ephen na namna navyotamani siku Moja nifanye jambo kubwa la kuuufanya hata moyo wako ukabubujikwa na machozi ya furaha ,kusema kumbe japo Dunia ni uwanja wa fujo na watu hawaaminiki na wamepungua upendo na utu lakini kumbe alikuwepo na yupo Lucas Mwashambwa katikati ya hao walimwengu mwenye roho ya upendo wa jua.
Sijawahi kububujikwa na machozi ya furaha nasubiri hiyo siku😂
 
Sijawahi kumuita shem wao ni watu wazima kwangu
Huwa namuamkia 'Shikamoo baba Cathe'
Na huwa simuagi sababu nakaa kibarazani siingii ndani kwao
Hiyo shikamoo baba cathe embu jirikodi voice note tuisikie kama imekaa kutongozwa tongozwa tuone kama baba cathe kweli ni wa kulaumiwa.
 
Back
Top Bottom