Nimeamini wanaume hawaaminiki

Nimeamini wanaume hawaaminiki

Habari!
Nimekutana na mkasa ambao umenifanya niamini wanaume sio watu wa kuwaamini 100%

Mimi ni mtu ambae muda mwingi najifungia ndani, lakini ikitokea nimekua mpweke sana huwa napendelea kwenda kwa jirani mwenye nyumba inayofuata baada ya kwetu.

Tumeshakua ni washkaji japo yeye ni mtu mzima kiasi, ana mume na watoto watano. Ila mimi na yeye tunaongea lugha moja. Mshkaji wangu namwita Mama Cathe. Anapendana sana na mume wake familia yao ni bora yenye upendo, kuwaona wamekumbatiana na mume wake ni jambo la kawaida sana.

Nipo karibu nae nimejua baadhi ya mambo, mume wake huwa anarudi kila siku mchana kula, mama Cathe huwa anamsubiri mchana ili wale wote saa 9.

Kwa jinsi wanavyopendana usiku wanaweka msosi nje wanakula mume, mke na watoto kulishana ni jambo la kawaida. Siku zote ninavyowachora mume anampenda sana mkewe, nilikua naona hawezi hata kumsaliti, hata michepuko haijui. Nilikua naamini kuna wanaume ni waaminifu na huyu Baba Cathe nilimuweka kundi hilo kwa jinsi wanavyoishi.

Juzi asubuhi mama kanituma nikanunue mahitaji, natembea zangu kwenye uchochoro mpana nikasikia mtu ameniita 'Ephen!' nikageuka nyuma. Nakutana na Baba Cathe akaniambia 'Nilikuona wakati unatoka nikasema nikufate sababu kila siku navizia nafasi ya kuongea na wewe lakini siipati, kwani unaenda wapi?'

Mpaka hapo nikawa nimeshangaa sikutegemea hii kauli kutoka kwake, hapo anaongea kimahaba
Huyu mzee nilikua namuheshimu sana....Nikamwambia naelekea dukani.

Akasema 'basi naomba namba yako siku yoyote naweza kukupigia tukutane sehemu X, huwa unanivutia sana nahitaji tuongee zaidi' nikamjibu sina simu

Alarm ikalia kichwani kwangu kua ule uchochoro yeyote anaweza kutokea ikawa kesi, sikumjibu nikageuka nikaendelea na safari yangu. Mimi nipo mbele yeye nyuma hapo natembea chap niumalize uchochoro akawa anaongea maneno ambayo siwezi kuyaandika hapa.

Nikamaliza uchochoro na yeye nahisi huku nyuma aligeuza, muda wote nikawa najiuliza huyu mzee kapatwa na nini?

Kilichonishtua ni jana nimekaa kibarazani na mkewe mida ya mchana, karudi mke wake akasimama kumkumbatia, huyu mzee akanikonyeza. Namuona anakuja kwa kasi!

Wanaume wote kumbe wanacheat.....!
Sifa ya moyo Tamaa Mkuu, Moyo sifa yake kutamani
 
Ninayo ndio lakini sio kama ya kwenu, unaenda kabisa kumtongoza mwanamke mwingine

Kaba mliyopewa niyakumeza mate unapomtamani mwingine bila kumtongoza sababu tayari unaye wa kwako!!!!!!!
Ujue hata wewe unayo tamaa
 
Ninayo ndio lakini sio kama ya kwenu, unaenda kabisa kumtongoza mwanamke mwingine

Kaba mliyopewa niyakumeza mate unapomtamani mwingine bila kumtongoza sababu tayari unaye wa kwako!!!!!!!
Key word hapo ni tamaa eph, matokeo ya tamaa ni kitu kingine, kuhusu kutongoza muhukumu yeye maana sisi wengine hata kutongoza hatuwezi
 
Key word hapo ni tamaa eph, matokeo ya tamaa ni kitu kingine, kuhusu kutongoza muhukumu yeye maana sisi wengine hata kutongoza hatuwezi
Yes! Nimeelewa kua sio wanaume wote

Lkn hapana mwanzo niliamini sio wote ila Baba Cathe kanivunja moyo😎
 
Primary ilikua moja tu, sikuhesabu secondary ila ni nyinginyingi kiasi kwamba inabidi tukubali matokeo.

Ehhhh...kumbe dawa yenu ni njaa tu ehhh???[emoji16]

Asante kwakunipa mbinu. From now on hashibi mtu kwa Dr!![emoji38]
Tukiwa na njaa hatuwazi kabisa hayo majambo, lakini wengine hata kutongoza hawajui that's make a study kuwa na fake conclusion
 
Wanawake bhana,siku nyingine ukimwona na mwanamke mwingine tofauti ndo utamkubali,sasa hivi hapo unamheshimu tu kwa vile hujawahi kumwona na hizo tabia,baada ya mda utamvulia tu pichu
 
Tukiwa na njaa hatuwazi kabisa hayo majambo, lakini wengine hata kutongoza hawajui that's make a study kuwa na fake conclusion
Nimeshachukua notes!😁

Sasa Cole...fake conclusion inatokea wapi na wahusika wamesupport findings za research ya mtoa mada bila kulazimishwa?

Inawezekana wewe ni exceptional ndio maana huelewi tumefikafikaje kwenye conclusion.
 
Back
Top Bottom