Nimeamini wanaume hawaaminiki

Nimeamini wanaume hawaaminiki

Habari!
Nimekutana na mkasa ambao umenifanya niamini wanaume sio watu wa kuwaamini 100%

Mimi ni mtu ambae muda mwingi najifungia ndani, lakini ikitokea nimekua mpweke sana huwa napendelea kwenda kwa jirani mwenye nyumba inayofuata baada ya kwetu.

Tumeshakua ni washkaji japo yeye ni mtu mzima kiasi, ana mume na watoto watano. Ila mimi na yeye tunaongea lugha moja. Mshkaji wangu namwita Mama Cathe. Anapendana sana na mume wake familia yao ni bora yenye upendo, kuwaona wamekumbatiana na mume wake ni jambo la kawaida sana.

Nipo karibu nae nimejua baadhi ya mambo, mume wake huwa anarudi kila siku mchana kula, mama Cathe huwa anamsubiri mchana ili wale wote saa 9.

Kwa jinsi wanavyopendana usiku wanaweka msosi nje wanakula mume, mke na watoto kulishana ni jambo la kawaida. Siku zote ninavyowachora mume anampenda sana mkewe, nilikua naona hawezi hata kumsaliti, hata michepuko haijui. Nilikua naamini kuna wanaume ni waaminifu na huyu Baba Cathe nilimuweka kundi hilo kwa jinsi wanavyoishi.

Juzi asubuhi mama kanituma nikanunue mahitaji, natembea zangu kwenye uchochoro mpana nikasikia mtu ameniita 'Ephen!' nikageuka nyuma. Nakutana na Baba Cathe akaniambia 'Nilikuona wakati unatoka nikasema nikufate sababu kila siku navizia nafasi ya kuongea na wewe lakini siipati, kwani unaenda wapi?'

Mpaka hapo nikawa nimeshangaa sikutegemea hii kauli kutoka kwake, hapo anaongea kimahaba
Huyu mzee nilikua namuheshimu sana....Nikamwambia naelekea dukani.

Akasema 'basi naomba namba yako siku yoyote naweza kukupigia tukutane sehemu X, huwa unanivutia sana nahitaji tuongee zaidi' nikamjibu sina simu

Alarm ikalia kichwani kwangu kua ule uchochoro yeyote anaweza kutokea ikawa kesi, sikumjibu nikageuka nikaendelea na safari yangu. Mimi nipo mbele yeye nyuma hapo natembea chap niumalize uchochoro akawa anaongea maneno ambayo siwezi kuyaandika hapa.

Nikamaliza uchochoro na yeye nahisi huku nyuma aligeuza, muda wote nikawa najiuliza huyu mzee kapatwa na nini?

Kilichonishtua ni jana nimekaa kibarazani na mkewe mida ya mchana, karudi mke wake akasimama kumkumbatia, huyu mzee akanikonyeza. Namuona anakuja kwa kasi!

Wanaume wote kumbe wanacheat.....!
Pole kuna vingi utazid kujifunza mdogo angu.
 
Mbona cha ajabu sijaona hapo mimi, kwani kutongozwa si kawaida tu hapo ulitakiwa useme yes au hapana.
 
Cha ajabu hapo ni mwanaume ana mke wake ila bado anataka michepuko
Iyo si ajabu best iyo ni nature kwa kiumbe anaitwa mwanaume, ni kawaida sana kuona mwanaume anampenda kupitiliza mke wake cha ajabu akakufata akakutongoza kutaka mapenzi iyo tunaita nature vizazi na vizazi, kibaya kutelekeza familia ndio mbaya zaidi.
 
Huyo mwanaume ni mwamimifu na anampenda sana mkewe.....anachokifanya anamlinda mkewe hataki awe karibu na wewe, anaogopa usije kumharibu mkewe🤣🤣🤣🤣......si unajua akufukuzae?

Angekuwa muhuni angefanyia mbali huko na angepata sababu ya kuchelewa kurudi as mkewe ana kampani nyumbani.....angewapisha Yani🤣🤣🤣
Huyo hakutaki na hataki kukuona karibu na mkewe ndo anawagombanisha......Ila ukijichanganya anakulamba kweli mgombane vizuri🤣🤣🤣

Halafu mashosti mpunguze kutembelea walioolewa, wanaume wengine washazoea wakirudi kazini wanapokelewa kikubwa, nyumba imefukizwa udi, mke ana kanga moja....ni kujishindia tu.....sa anarudi anakuta mke anafumuana nywele na shost, ni ukatili mnafanya huo🤣🤣🤣 Tulia kwenu mdogo angu.
 
Chumba chao sijawahi kuingia hata sebule yao sijui inafanana vipi, nyumba zetu zipo karibu kiasi kwamba sioni shida kukaa kibarazani kwao na yeye huwa anakuja kibarazani kwetu kukaa

Tunakaa na watoto wake tunapiga story tunacheka sasa kama ananihofia mimi kazi kwake
Na sio kwamba mimi ndo best wa mama cathe nop! Ana marafiki zake mtaani ila akiwa peke yake ndo naenda kwa wiki hata mara 3 haifiki cz mimi mwenyewe nakua busy na mambo yangu
 
Nakushauri usiende kwake, hawa wanaume kadri tunavyoishi nao ndo wivu unaongezeka.......akimaliza kukutongoza atakwambia unamfundisha umalaya mke wake.
 
Mama Cathe ni mtu naelewana nae hata mama angu ni rwfiki yake mkubwa
Sema Mumewe ndo anataka kuleta mambo ya kiwaki...
Kama upo single na upo serious nichek private tujenge maisha.
Achana na huyo mume wa mtu
 
Back
Top Bottom