Nimeamka asubuhi nimekuta shuka zina matone ya damu!! mpaka saizi najitafuta nilipoumia sipaoni?

Lazima kuwe na damu puani/mdomoni, lzm ataamka damu inapotoka.
 
Hauoni inapotokea unakuta damu tu ebwana km hauamini basi baki hivyo hivyo ni damu na majimaji huamini basi subiri mpaka zamu yako ifike
Damu inayotoka ndani kwenye mapafu/ Koo, itapitia puani au mdomoni.
Ikipita puani kama ni nyingi kiasi cha kuziba pumzi, mgonjwa lazima atashtuka kutoka usinguzini, kama itapita mdomoni, hiyo ni kutapika damu.
 
Mimi niliwahi kukuta damu matone mabichi bafuni kwangu.

Nilisali nikakemea na maisha yakaendelea
 
Karibu kwenye Mkesha usiosahaulika kwa Mtume Mwamposa tarehe 13/12 Kawe. Tatizo lako limekwishaa
 
Wasikutishe apo Mbu walikudunga wakashiba damu...ww ukawalalia wakapasuka.
Tatizo umewaza uchawi sana
 
Haujahumia popote jua ni kunguni hao wanafataga maskini na vijana wachafu
 
Inawezekana ni Mbu alikunyonya Damu baadaye akatapika, kama unaamini tofauti simama katika imani yako.
 
Usije ukafikiria kuna mambo ya kishirikina hapana, chunguza vizuri kutakuwa kuna mdudu ulimlalia.
Amesubiri sana kuona jibu hili maana amesema yuko Kigoma hapo tayari nilijua anawaza nini
Ila watu naona wanaanza kujielewa kuhusu ushirikina
Nimefurahi kuona wengi wanatoa majibu tofauti na uchawi hii inaashiria mema kwa nchi
 
Amesubiri sana kuona jibu hili maana amesema yuko Kigoma hapo tayari nilijua anawaza nini
Ila watu naona wanaanza kujielewa kuhusu ushirikina
Nimefurahi kuona wengi wanatoa majibu tofauti na uchawi hii inaashiria mema kwa nchi
Kweli kabisa, maana ukiamini sana ishu za ushirikina ata ukijikwaa unahisi umerogwa.
 
Kuna popo ambao huwa na tabia ya kunyonya damu wanyama au binadamu. Hivyo angalia kwamba hawapati nafasi ya kuingia unapolala! Tumia net.

Hao popo, wanaitwa vampire bats, wanapokunyonya damu wala hutajua. Na unaweza usipaone walipokunyonya damu, ila wanapokunyonya kuna damu itadondoka. Ni nadra sana kuwakuta sehemu zetu hizi lakini inawezekana. Na kama amekunyonya atarudi tena.

Fanya mpango kama unaweza kupata video yao, ili uwatarrifu watafiti uwepo wa vampire bats eneo lako.

Pia kuna panya wanaweza kukutafuna usiku, lakini ungeona kidonda.
 
hao popo nawajua ila hawapo tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…