Nimeamua kuachana na masuala ya dini, sihitaji kero za ajabu

Nimeamua kuachana na masuala ya dini, sihitaji kero za ajabu

Intelligent businessman

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
31,913
Reaction score
65,514
Nimepiga hesabu nikaona dini ni urithi mmoja wa ajabu sana, ninaamini Mungu yupo ila nita mwabudu nje ya hilo box.

Yaani unazaliwa na kukabidhiwa kitu usichokielewa au kupewa nafasi ya kuchagua.

Na hizi dini ndio zimetengeneza viumbe wenye hulka ya mazombie au vampire, ambao wao kazi yao ni kufata wasemayo viongozi au maandishi wasiyoelewa asili yake.

Mara mtu ampige au amtukane mwenzie kisa dini, yaani unajiona bora kisa dini tena utasikia wewe huendi mbinguni!.

Kuanzia Leo nina Imani na sio dini nisizozielewa.
 
Nime piga hesabu nika ona dini ni urithi mmoja wa ajabu sana, nina amini Mungu yupo ila nita mwabudu nje ya hilo box.

yaani una zaliwa na kukabidhiwa kitu usicho kielewa au kupewa nafasi ya kuchagua.

na hizi dini ndio zime tengeneza viumbe wenye hulka ya mazombie au vampire, ambao wao kazi yao ni kufata wasemayo viongozi au maandishi wasiyo elewa asili yake.

Mara mtu ampige au amtukane mwenzie kisa dini, yaani una jiona bora kisa dini tena uta sikia wewe huendi mbinguni!.

Kuanzia Leo nina Imani na sio dini nisizo zielewa.
Mkuu,
Nini kimekukuta? Nini kime ishake Imani YAKO.
 
Dini inakupa hisia kwamba unamtumikia Mungu ilhali unawatumikia wamiliki wa hiyo dini.

Dini inakwambia nyoka anaongea na punda ana mabawa anapaa juu.

Na huruhusiwi kupinga huku ukweli unajulikana kwamba nyoka hawezi kuongea na wala punda hawezi kupaa
 
Nime piga hesabu nika ona dini ni urithi mmoja wa ajabu sana, nina amini Mungu yupo ila nita mwabudu nje ya hilo box.

yaani una zaliwa na kukabidhiwa kitu usicho kielewa au kupewa nafasi ya kuchagua.

na hizi dini ndio zime tengeneza viumbe wenye hulka ya mazombie au vampire, ambao wao kazi yao ni kufata wasemayo viongozi au maandishi wasiyo elewa asili yake.

Mara mtu ampige au amtukane mwenzie kisa dini, yaani una jiona bora kisa dini tena uta sikia wewe huendi mbinguni!.

Kuanzia Leo nina Imani na sio dini nisizo zielewa.
Mkuu, hata elimu ni urithi tuliokabidhiwa, na kama elimu umeipenda, lazima uielewe.

Kwa mkutadha huo, hata dini ni urithi ila hujaielewa kwa kuwa hujaipenda.

Maisha mema huko uendako.
 
Back
Top Bottom