Nimeamua kujitoa CHADEMA rasmi kutokana na Mdude, najuta kumchangia

Nimeamua kujitoa CHADEMA rasmi kutokana na Mdude, najuta kumchangia

Unahaki ya kujitoa Mdude si ndio yele aliyemwambia mama yetu kipenzi kuwa ATAMNYOA KAMA ALIVYOMNYOA JPM

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa kwenye siasa kusema utamnyoa kunashida gani? Mama lazima apewe changamoto anaendesha taifa sio kigango cha mtakatf Teresa!

Atapewa lugha ngumu, atachorwa, atasifiwa, atazomewa na anapaswa kuyastahimili hii nchi tusilazimishane wooote tutumie busara moja zipo busara mbalimbali katika udai uwajibikaji!! Kunyolewa sio tusi inategemeana na akili za mtu
 
CHADEMA walijitoa watu wa muhimu sana na bado imebaki imara zaidi ya jana
[emoji16][emoji16][emoji16]chadema ya 2010 ukailinganishe na utumbo wa akina mdude!!!

kinachoniuma hakuna mtu timamu ndani ya chama aliyethubutu kukemea upumbavu wa huyu mlemavu wa akili, ili chama kibaki sehemu salama.
 
Wakuu

Naomba hii thread isiunganishwe na mods huu uzi ubaki hapahapa

Siasa ni ustahimilivu na kuvumiliana lakini kutumia maneno makali inategemeana na aina ya mtu

Niwatolee mfano tu mtu kama mwendazake mdude angemjibu hivi ingekua sawa kabisa maana bwana yule naye alikua na maneno ya kashfa na kejeli na lugha chafu haswa

Lakini kwa mama sidhani kama ilikua ni uungwana kumjibu namna hiyo kwasababu uhalisia wa SSH ni mstaarabu sana na ana busara na hekima pia ndani ya siku 100 tu katupa vitu vingi sana tulivyokosa wakati wa bwana yule

Uhuru wa vyombo vya habari, demokrasia na masuala ya kiuchumi kajitahidi si haba

Ila kauli ya ndugu yangu mdude imenifanya nitafakari sana, na kauli ya mbowe pia na hata lissu, waswahili wanasema "ukimkimbiza mjusi sana mwishowe hugeuka nyoka na kukuuma"

Mimi sitaki huyu mama abadilike, wakati mwingine utakayomfanyia mtu inaweza kumbadilisha akawa mtu wa tofauti sitaki huyu mama yetu abadilike awe dikteta naombeni sana tudai haki ila kuangalia ndimi zetu

Mwisho kabisa nimeamua kujitoa chadema kuanzia leo sio mwanachama wa CDM tena wala sio kwamba eti nitaenda CCM hilo kamwe halitotokea nitasimama kuendelea kutetea Haki,uhuru na demokrasia na maendeleo bila kuwa Chadema

Maneno ya mdude yamenifanya niichukie chadema kuanzia leo sitaki hata kuisikia masikioni mwangu

Sikutarajia kama cdm ingebariki kuwa na watu wa ajabu hivi na hili la mdude limewafanya watu wengi kuichukia Chadema na hili linaweza kupelekea kupoteza asilimia 80 ya wanachama wa chadema

Najuta kwanini nilitoa mchango wangu tu maana huyu angebaki tu jela hana adabu kabisa
Kimsboy:Vipi umeogopa kinyolewa na wewe.tulia unyolewe vizuri
 
Sasa kwenye siasa kusema utamnyoa kunashida gani? Mama lazima apewe changamoto anaendesha taifa sio kigango cha mtakatf Teresa!
Atapewa lugha ngumu,atachorwa,atasifiwa,atazomewa na anapaswa kuyastahimili hii nchi tusilazimishane wooote tutumie busara moja zipo busara mbalimbali katika udai uwajibikaji!! Kunyolewa sio tusi inategemeana na akili zamtu
mama ni mama, akianza kuongea lugha za mwendazake kwa vitendo msijetafuta mchawi.

ndio maana sisi huwa tunawaita nyinyi ni wanafiki, maana ukweli ni kwamba hamjui kipi mnataka.

sasa hivi nina uhakika mama anajutia maamuzi ya kumwachia huyo pangahewa.
 
[emoji16][emoji16][emoji16]chadema ya 2010 ukailinganishe na utumbo wa akina mdude!!!

kinachoniuma hakuna mtu timamu ndani ya chama aliyethubutu kukemea upumbavu wa huyu mlemavu wa akili,ili chama kibaki sehemu salama.

Tuonyeshe mahali ulipokemea Magufuli akisema watu wabaki na mavi yao nyumbani.
 
mama ni mama,akianza kuongea lugha za mwendazake kwa vitendo msijetafuta mchawi.

ndio maana sisi huwa tunawaita nyinyi ni wanafiki,maana ukweli ni kwamba hamjui kipi mnataka.

sasa hivi nina uhakika mama anajutia maamuzi ya kumwachia huyo pangahewa.

Kwahiyo mama anasikitishwa na mambo madogo ya lugha za kina Mdude, lakini hasikitishwi na waliojiunganishia bomba la mafuta? Badala ya kumtaka mama aonyeshe uwajibikaji kwa mambo ya msingi, mnamjaza ajikite kwenye lugha za wanaharakati waliohujumiwa.
 
Wakuu

Naomba hii thread isiunganishwe na mods huu uzi ubaki hapahapa

Siasa ni ustahimilivu na kuvumiliana lakini kutumia maneno makali inategemeana na aina ya mtu

Niwatolee mfano tu mtu kama mwendazake mdude angemjibu hivi ingekua sawa kabisa maana bwana yule naye alikua na maneno ya kashfa na kejeli na lugha chafu haswa

Lakini kwa mama sidhani kama ilikua ni uungwana kumjibu namna hiyo kwasababu uhalisia wa SSH ni mstaarabu sana na ana busara na hekima pia ndani ya siku 100 tu katupa vitu vingi sana tulivyokosa wakati wa bwana yule

Uhuru wa vyombo vya habari, demokrasia na masuala ya kiuchumi kajitahidi si haba

Ila kauli ya ndugu yangu mdude imenifanya nitafakari sana, na kauli ya mbowe pia na hata lissu, waswahili wanasema "ukimkimbiza mjusi sana mwishowe hugeuka nyoka na kukuuma"

Mimi sitaki huyu mama abadilike, wakati mwingine utakayomfanyia mtu inaweza kumbadilisha akawa mtu wa tofauti sitaki huyu mama yetu abadilike awe dikteta naombeni sana tudai haki ila kuangalia ndimi zetu

Mwisho kabisa nimeamua kujitoa chadema kuanzia leo sio mwanachama wa CDM tena wala sio kwamba eti nitaenda CCM hilo kamwe halitotokea nitasimama kuendelea kutetea Haki,uhuru na demokrasia na maendeleo bila kuwa Chadema

Maneno ya mdude yamenifanya niichukie chadema kuanzia leo sitaki hata kuisikia masikioni mwangu

Sikutarajia kama cdm ingebariki kuwa na watu wa ajabu hivi na hili la mdude limewafanya watu wengi kuichukia Chadema na hili linaweza kupelekea kupoteza asilimia 80 ya wanachama wa chadema

Najuta kwanini nilitoa mchango wangu tu maana huyu angebaki tu jela hana adabu kabisa
Kaazishe chama chako
 
Mama amejibu kwa maneno mazuri sana tena yenye matumaini lakini CHADEMA wameona kumbe Huyu tunaweza kumfanya lolote. Mama ana maneno yenye kuleta matumaini, wameshindwa kujiuliza kwamba, hivi Mafufuli angekuwa hai Mdude angekuwa uraiani? Akina Mbowe kesi kufutwa, tunashubudia mengi yasiyotarajiwa. Lakini CHADEMA sikio la kufa eti leo wamekuwa wababe wako tayari kwa lolote. Tunasubiri mwisho wa huo utayari, Mimi yangu macho.
 
Kwahiyo mama anasikitishwa na mambo madogo ya lugha za kina Mdude, lakini hasikitishwi na waliojiunganishia bomba la mafuta? Badala ya kumtaka mama aonyeshe uwajibikaji kwa mambo ya msingi, mnamjaza ajikite kwenye lugha za wanaharakati waliohujumiwa.

sisi tunadeal na mdude aache kichaa,maamuzi ya nini afanywe mdude kwa wakati upi anayo mama mwenyewe.
na tunafanya haya ili kuchukua tahadhali ili mama asijebadilika.

sasa kama alihujimiwa na bado anawashwa basi akitulize tu,asijezua mengine.
 
Jamani tuwe na ubinadamu. Kauli ya Mdude ina shida gani?

He has been through a lot. He is also a human. Hebu tupunguze chuki kwake.

Mimi ni team Magufuli, lakini kwa hili hapana. Tujiwekeni kwenye viatu vyake kabla ya kuhukumu, tusifuate mkumbo.
kama huoni shida ya mdude kwenye move zake basi nawewe una shida sehemu.
 
Kauli ya Mdude ni ya kipumbavu hakuna mwenye akili anaweza kukubaliana nayo. Watanzania tunahitaji katiba mpya tena sana! Ila tunaweza kutoa kauli za busara na tukaridhiana kupata hiyo katiba kwa amani tu!!

Sioni kama mama Samia ni mtu katili kwamba asitupatie tunachohitaji! Mama ni mwelewa na pengine hata yeye mwenyewe anaona umuhimu wake!

Tudai katiba mpya siyo kwa matusi ila kwa hekima! Hata watanzania watatuelewa! Ila tukianza kutukana na kejele wenye busara watawaona kama wehu,

Busara ni kitu kidogo, CDM kama wanamtaka sana mdude wamkalishe chini wamfunze namna ya kuongea!
Akitukana magufuli au kheri james unakuwa uzarendo
 
kama huoni shida ya mdude kwenye move zake basi nawewe una shida sehemu.
Ninafikiri shida ipo kwa wakatili, msiojali hisia za wengine na wenye roho mbaya na chuki kama wewe.
 
Ninafikiri shida ipo kwa wakatili, msiojali hisia za wengine na wenye roho mbaya na chuki kama wewe.
kila mtu akiheshimiwa kwa hisia zake,kuna wajinga watakuja kukutongoza na ndevu zako wakikwambia unavutia sana kama mtoto wa kike.

duniani kila jambo tunalifanya kwa kitu tunaita self control,huwezi amua fanya jambo lolote tu kisa una uwezo huo,hata kama hakuna wa kukufanya kitu.
 
Back
Top Bottom