Wakuu
Naomba hii thread isiunganishwe na mods huu uzi ubaki hapahapa
Siasa ni ustahimilivu na kuvumiliana lakini kutumia maneno makali inategemeana na aina ya mtu
Niwatolee mfano tu mtu kama mwendazake mdude angemjibu hivi ingekua sawa kabisa maana bwana yule naye alikua na maneno ya kashfa na kejeli na lugha chafu haswa
Lakini kwa mama sidhani kama ilikua ni uungwana kumjibu namna hiyo kwasababu uhalisia wa SSH ni mstaarabu sana na ana busara na hekima pia ndani ya siku 100 tu katupa vitu vingi sana tulivyokosa wakati wa bwana yule
Uhuru wa vyombo vya habari, demokrasia na masuala ya kiuchumi kajitahidi si haba
Ila kauli ya ndugu yangu mdude imenifanya nitafakari sana, na kauli ya mbowe pia na hata lissu, waswahili wanasema "ukimkimbiza mjusi sana mwishowe hugeuka nyoka na kukuuma"
Mimi sitaki huyu mama abadilike, wakati mwingine utakayomfanyia mtu inaweza kumbadilisha akawa mtu wa tofauti sitaki huyu mama yetu abadilike awe dikteta naombeni sana tudai haki ila kuangalia ndimi zetu
Mwisho kabisa nimeamua kujitoa chadema kuanzia leo sio mwanachama wa CDM tena wala sio kwamba eti nitaenda CCM hilo kamwe halitotokea nitasimama kuendelea kutetea Haki,uhuru na demokrasia na maendeleo bila kuwa Chadema
Maneno ya mdude yamenifanya niichukie chadema kuanzia leo sitaki hata kuisikia masikioni mwangu
Sikutarajia kama cdm ingebariki kuwa na watu wa ajabu hivi na hili la mdude limewafanya watu wengi kuichukia Chadema na hili linaweza kupelekea kupoteza asilimia 80 ya wanachama wa chadema
Najuta kwanini nilitoa mchango wangu tu maana huyu angebaki tu jela hana adabu kabisa