Nimeamua kujitoa CHADEMA rasmi kutokana na Mdude, najuta kumchangia

Nimeamua kujitoa CHADEMA rasmi kutokana na Mdude, najuta kumchangia

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
9,846
Reaction score
20,319
Wakuu,

Siasa ni ustahimilivu na kuvumiliana lakini kutumia maneno makali inategemeana na aina ya mtu.

Niwatolee mfano tu mtu kama mwendazake Mdude angemjibu hivi ingekuwa sawa kabisa maana bwana yule naye alikuwa na maneno ya kashfa na kejeli na lugha chafu haswa.

Lakini kwa mama sidhani kama ilikuwa ni uungwana kumjibu namna hiyo kwasababu uhalisia wa SSH ni mstaarabu sana na ana busara na hekima pia ndani ya siku 100 tu katupa vitu vingi sana tulivyokosa wakati wa bwana yule.

Uhuru wa vyombo vya habari, demokrasia na masuala ya kiuchumi kajitahidi si haba.

Ila kauli ya ndugu yangu Mdude imenifanya nitafakari sana, na kauli ya Mbowe pia na hata Lissu, waswahili wanasema "ukimkimbiza mjusi sana mwishowe hugeuka nyoka na kukuuma"

Mimi sitaki huyu mama abadilike maana miaka 6 ya mwendazake tumeteseka sana, wakati mwingine utakayomfanyia mtu inaweza kumbadilisha akawa mtu wa tofauti sitaki huyu mama yetu abadilike awe dikteta naombeni sana tudai haki ila kuangalia ndimi zetu.

Mwisho kabisa nimeamua kujitoa Chadema kuanzia leo sio mwanachama wa CDM tena wala sio kwamba eti nitaenda CCM hilo kamwe halitotokea nitasimama kuendelea kutetea Haki, uhuru na demokrasia na maendeleo bila kuwa Chadema.

Maneno ya Mdude yamenifanya niichukie chadema kuanzia leo sitaki hata kuisikia masikioni mwangu.

Sikutarajia kama Chadema ingebariki kuwa na watu wa ajabu hivi na hili la Mdude limewafanya watu wengi kuichukia Chadema na hili linaweza kupelekea kupoteza asilimia 80 ya wanachama wa Chadema.

Najuta kwanini nilitoa mchango wangu tu maana huyu angebaki tu jela hana adabu kabisa.
 
Uliingia chadema kumfata Mdude?

Pole unautoto ubongoni! Kimsingi kukatalia katiba ni dharau kubwa sana kwa watz, watu wameteswa, wamepotea, wameumia kwa katiba kushindwa kuweka misingi bora ya kistaarabu katika taifa! MTU yeyote anayezuia katiba hastahili heshima kabisa.
 
... CCM IS MESSING UP WITH THE WRONG GENERATION!
... ANOTHER ESWATINI COOKING!
😅
1625394571379.png
 
Kauli ya Mdude ni ya kipumbavu hakuna mwenye akili anaweza kukubaliana nayo. Watanzania tunahitaji katiba mpya tena sana! Ila tunaweza kutoa kauli za busara na tukaridhiana kupata hiyo katiba kwa amani tu!

Sioni kama mama Samia ni mtu katili kwamba asitupatie tunachohitaji. Mama ni mwelewa na pengine hata yeye mwenyewe anaona umuhimu wake.

Tudai katiba mpya siyo kwa matusi ila kwa hekima! Hata watanzania watatuelewa! Ila tukianza kutukana na kejele wenye busara watawaona kama wehu.

Busara ni kitu kidogo, CDM kama wanamtaka sana mdude wamkalishe chini wamfunze namna ya kuongea!
 
Back
Top Bottom