Nimeamua Kukisanua: Hii ndiyo sababu ya Jezi za Simba SC kutozinduliwa hadi leo

Hapa tumeshafeli kwa jinsi walivyoniudhi hata Simba day siendi hata wakitoa sababu milioni moja mimi siwezi kuwaelewa kwenye suala la jezi hapa tukubali Simba mwaka huu kwenye jezi tumefeli vibaya sana inaniuma sana wangekuwa karibu ningepiga makofi viongozi wote tunafanyaje mambo kienyeji kama utopolo?
 
Ha ha ha Tangu lini TPA wakawa wakusanya kodi? Ungesema TRA ningekuelewa. TPA hawaiingii kabisa huko. Endelea kuwajaza mashudu wajinga
 
Umefua nguo yako ya ndani?
 
Yaani watu wengine hawana hata hela ya kununua jezi lakini wanalazimika jezi hakuna
Mashabiki wa UTO nao wanalazimika jezi za Simba hakuna
 
Anaandika Shafii Dauda

Kuna dunia ambayo Simba wanaishi, ni dunia ambayo wanaamini hakuna makosa, wanaamini ni wakubwa, wanaamini kila kitu kinachofanyika ni sahihi sana

Hata pale ambapo wameharibu watahitaji kupamba na kuonekana hawajaharibu, hata pale watapopaswa kuambiwa maneno machungu ya ukweli watahitaji nyimbo za mapambio

Siku chache zimesalia kuelekea Ngao ya Jamii hawana jezi mpya, masaa yamesalia kuelekea Simba Day hawana jezi mpya, lakini ndio klabu hii ambayo tunalazimishana kuiita kubwa, klabu yenye weledi? Excuse me

CEO kama Mtendaji wa klabu you are in for this, suala la jezi sio option ni lazima, suala la merchandise ni compulsory na linafahamika, inatia ukakasi kwa namna mnavyoyaendea mambo, inafikirisha sana

DIGALA siwezi kukubali kuwa kwenye dunia ya praise and worship, sio dunia nzuri ya kuficha makosa na kuonekana mema, sio dunia nzuri mambo yakienda mrama watu wasake namna ya kujificha sio sawa na hii ni AIBU

Kwa Shabiki wa Simba anayejua mpira na kuelewa maana ya biashara anafahamu kuwa hili mmeharibu, lakini kwa Shabiki yule oya oya tu ataona DIGALA nachonga, ataona Digala ana nongwa ila in details nawapa dawa ya kuwaponya

Kwakuwa hili mmeshaharibu sio vyema msimu wa 2023/24 mkarudia tena makosa, hakuna excuse kwa matukio ambayo yana time frame, hakuna excuse ya Mdhamini wala usafiri, jezi sio suala la bahati mbaya

Hakuna wimbo wa maana utakaotungwa kuepusha aibu hii, hakuna wimbo utatungwa kuepusha kadhia hii, ndio ni klabu maarufu sasa pambaneni kuusaka UKUBWA, ukubwa una details zake, ukubwa una indicators zake, BADILIKENI

DIGALA naamini mpira ni darasa kubwa, utawala ni darasa kubwa, muda wa kuendelea kujifunza upo na naamini tukae darasani kama Wanafunzi watiifu na sio Walimu wakorofi

DIGALA
 
Na wewe ukaamua umtukane😂😂
Sisi yetu macho, tumekatazwa kuingilia mambo ya msimbazi.
 
Kwahiyo jezi zipo ila ziko bandarini,Fredy anakwa wapi kuchonga na akina Kasimu Majaliwa zikaachiwa
 
Chupli chupli fc watapita kimya kimya hapa.
 
"uongo hauna miguu ila scendo zinapaa"by Fid q
 
Ifike mda serikali ilete tozo za kuongea naona wamna mnaongea ongea tu pumba siku hz
 
HV Kat ya tra na tpa Nani mwenye nguvu ya kuzuia mzigo usitoke bandarini mnk inaonesha ujui lolote kuhusu bamdari na tarattibu zake wa kuclear mzigo hujui nakumbiaa na Kama unajuwa toa jinsi ganu ya kuckear mzigo utoke

Acah kudanganya ummma kuwaboss mpy wa tpa kagoma kutoa mzigo
 
Procedure za kutowa mzigo ni hizi.
• Bill of loading
• C& F
• Tax
• Shipping line
• Port chargers
 
Mkataba wa sportpesa umeisha katambo sana kabla ligi haija isha Barbra alidhibitisha hilo na ilikua inafahamika kua hautoongezwa labda kama kuna issue nyingine ila sio mdhamini
Hivi nyie mazuzu nani aliewaloga?

Unakataa tatizo sio mdhamini halafu unasema labda kama kuna issue nyingine, sasa kama unaijua hiyo issue nyingine si uitaje?

Wafuasi wa popoma ni shida sana.
 
Procedure za kutowa mzigo ni hizi.
• Bill of loading
• C& F
• Tax
• Shipping line
• Port chargers
Mbona hapo TPA kama anahusika tena wamwisho . Au waliosoma mambo ya shipping hamtueleweshi vizur
 
Sikuachi hata kama ukiwa certified popoma.

Lazima utambue, mazungumzo ya mkataba yanafanyika wakati wowote na mtu yeyote anayetaka kuidhamini klabu, hata kama Ahmed Ally alisema hawataongeza mkataba na Sportpesa.

Hiyo haikuwa sababu ya Simba SC kuwafungia milango Sportpesa, bado walikaribishwa wakati wowote kama wangeongeza mzigo, na mazungumzo yakawepo; popoma haya mambo yako nje ya uwezo wako wa kufikiri, una mikelele tu kama chizi mlevi.

Hiyo sababu yako ya kipuuzi kwamba Vunjabei alitaka kukwepa kodi unajitungia tu, kwasababu unajua hao wajinga wako 115 uliowafungasha akili hawatakuuliza.

Ni mjinga tu atakaeamini taasisi kubwa kama Simba SC, yenye watu kila mahali, ishindwe kukomboa mzigo wake bandarini zaidi ya mwezi kisa inadaiwa kodi.

Haya tuambie, hiyo kodi anayodaiwa Vunjabei ni kiasi gani utupe na ushahidi sio ujitungie namba tu kama kawaida ya upopoma wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…