Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

hongera kaka, watu wengi natumaini wamekushangaa kwa uamuzi wako lakini mimi naamin u have made a perfect choice......lakini tunaomba updates za huko ili tuweze kuoanisha mawazo na practical
 
Elnino ;

naweza kupata kibarua cha kuwalimia watu kwa trakta huko uliko ; gharama ya kulima kwa ekari ni kiasi gani nifanye mahesabu.

Kwa mnaotaka kulima mahindi karibuni wilayani Mpwapwa ama Kongwa.................ulimaji wake ni nafuu na hautajutia.
 

Mkuu ungeweka wazi sifa za hapo Kongwa na mpwapwa. Naomba unitafutie ile mbegu fupi ya mapapai, nasikia iko na inapatikana huko Mpwapwa.
 
Best of luck man! From the tone of your story and these posts it is very obvious that you know what it takes and are ready to do it. I cant wait to see what 2012 brings for you.

Go get em! We are all rooting for you.




 
Du poleni kwa kupotea,

Ok kwa wilaya za Kongwa , Mpwapwa na Chamwino ghrama za wastani za kukodi shamba kwa ekari (zinazopimwa kienyeji) ni shs 15000

Kulima kwa Trekta ni elfu 30000 na gharama ya kupanda ni 2000 na kupalilia ni 15000 kwa ekari.

mavuno waweza kupata wastani wa gunia 6 na kwa bei ya msimu mwaka huu ziliuzwa kwa 40,000 kwa kila gunia la madebe 7.
 
wadau mi natafuta mbegu za minaza zile mbegu fupi, kwa anayejua anisaidie mimi sijui nitazipata wapi?
 
Sina uhakika na hiyo selling price ya gunia la mahindi Tsh 60,000/- Je umefanya utafiti wa hali ya soko? Sera za nchi haziruhusu kuuza chakula nje ya nchi!
 
Kilimo bila kujipanga kinaweza kukufanya ukawa maskini zaidi -- Serikali ya Tanzania haijaweka mazingira ya kilimo cha kisasa bali wameweka usanii mtupu. Kilimo kwa sasa hakikwezi kukutoa -- sahau.

Mimi nitabakia mjini hapa hapo kukimbizana kimbizana tu na mgambo wa jiji mpaka kitaeleweka. mashambani siendi.
 
Maskini jeuri mzima kaka,

Hujajibu ombi langu la mbegu za mapapai mbegu fupi.

Kaka Elnino mie mzima ; nimehamia bonde la ruvu kufanya kibarua ndio maana sikuona mapema hii kitu

Nadhani huo utakuwa upande wa Mpwapwa kusini.........nitatuma ujumbe huko nipe muda ndg!
 
ndoto ka ya alinacha alipokuwa kabeba mayai akaishia kupasua.

Anyway kilimo kinatoa ila jiandae kucmama wewe kama wewe c unaijua sirikali yetu inatuongopea tangu tunapata uhuru mpk leo kuwa kilimo n uti wa mgongo na hakijawah hata siku moja kuboresha mazngra.

Mimi ni mkulima mzuri tu npo dabaga mufind iringa na songea magagura nalima mahindi karibu.
 

Ni kweli hata hizo process za Dirisha la Kilimo ni kizungumkuti kingine
 

Mkuu Elnino, asante kwa update hakika kuna mengi ya kujifunza. Nimefuatilia huu uzi tangu mwanzo na nafurahishwa na wazo la Agroprocessing. Pamoja na hasara uliyoipata kwenye msimu wa kwanza, mie nadhani ukipata suluhisho la tatizo la kwanza; ukosefu wa mvua!

Fani yangu mimi ni Rasilimali Maji, na huku ninapopiga boxi wakulima wengi wanahakikisha kuna maji endapo mvua hazikufanya vizuri; tena hawatumii gharama kubwa sana.

Tukapata suluhisho la kupata maji kunyweshea mnazao kila mvua zinapochelewa basi inaweza kututoa.

Vipi ukafikiria combination ya kulima na Agroprocessing? kununua kutoka kwa wakulima wengine iwe nyongeza lakini sehemu kubwa itoke shambani kwako?
 

Kulima na kusindika ni nzuri sana,tatizo lipo ktk vitendea kazi hasa umeme.

Mahali kwenye ushindani mdogo unakuta hakuna umeme wala barabara. Kuna jamaa wapo Iringa Vijijini, wanalima mahindi hadi raha, wamejenga milling plant yao kando ya barabara kuu ambapo kuna umeme. Kwa hiyo wanasafirisha mahindi umbali wa km 20, kisha wanarudisha pumba shambani umbali huo huo, kumbe umeme ungefikishwa ktk mji ule(sio kwa ajili yao tu,hapana, yaani vijiji vyote pale havina umeme) hizi gharama zingetoweka, pili kijiji kingenufaika na ajira,wangeuza mahindi yao bila gharama za usafirishaji.

Haya jamaa wengine,wana shamba la ng`ombe wa maziwa,kwa kukosa umeme inabidi jamaa apeleke maziwa mjini kila siku,lakini kungekuwepo na nishati hii, mjini angepeleka finished products tu, au wanunuzi wangemfuata pale shambani kwake.

Kwa hiyo, kama nishati/nguvu kazi ipo bora kuunganisha, yaani zalisha na kusindika. Kama haya mawili hakuna basi chagua moja la kufanya. Hicho ndio kilimo chetu.
 


Kwa mtizamo tu ni miundo mbinu ya gharama kiasi gani ukitaka kumwagilia shamba la ekari 45...........hii ikiwa ni pamoja na kuchimba kisima.........nahitaji vifaa gani na natakiwa kuwa na akiba ya maji kiasi gani kujihakiishia uzalishaji wa mwaka mzima?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…