Kwa mtizamo tu ni miundo mbinu ya gharama kiasi gani ukitaka kumwagilia shamba la ekari 45...........hii ikiwa ni pamoja na kuchimba kisima.........nahitaji vifaa gani na natakiwa kuwa na akiba ya maji kiasi gani kujihakiishia uzalishaji wa mwaka mzima?
Kwa mtizamo tu ni miundo mbinu ya gharama kiasi gani ukitaka kumwagilia shamba la ekari 45...........hii ikiwa ni pamoja na kuchimba kisima.........nahitaji vifaa gani na natakiwa kuwa na akiba ya maji kiasi gani kujihakiishia uzalishaji wa mwaka mzima?
Utahitaji kuchimba kisima kirefu (kadiria 5m), iwapo kuna mto karibu unaweza kuokoa gharama katika hili vilevile mashine (pampu) na mabomba ya plastic (low grade) kusambazia, inakuwa rahisi ukiwa na tanki sehemu ya mwinuko ili maji yaende kwa gravity (kadiria 3m - 5m), ukimpata fundi mchundo aliyekaribu na shamba lako anaweza kushauri vizuri kwa kutembelea eneo husika (ulizia Idara ya Maji wilayani utawapata).
Kumbuka lengo hapa ni kuziba pengo la kipindi kifupi ambapo mvua zinachelewa au kukatika katikati ya msimu, hivyo basi mtandao wa mabomba shambani si wa kudumu bali katika hali ambayo unaweza kuweka na kuhamisha. Kumbuka gharama za uendeshaji; umeme au diesel/petrol, hapa nilipo serikali yao inaweka ruzuku kwenye diesel ya mashambani.
Jamani nikitaka shamba la kukodisha napata wapi wanabodi? sehemu yenye rutuba ya kutosha na miundo mbinu, na je inagharimu kiasi gani kwa hekari moja?
Ungeweka wazi vitu vifuatavyo:Jamani nikitaka shamba la kukodisha napata wapi wanabodi? sehemu yenye rutuba ya kutosha na miundo mbinu, na je inagharimu kiasi gani kwa hekari moja?
Nao ni mpango kabambe pia.........swali nikuwa utakimbizana nao hadi utapofikisha miaka 60?
Ungeweka wazi vitu vifuatavyo:
1.Unatarajia kulima mazao gani?
2.Shamba liwe mkoa gani?
3.Unatarajia kulima ekari ngapi?
Kwa mkoa wa Dodoma rates za kukodi ni kuanzia elfu 15 mpaka 25 kwa ekari,
Mbeya eneo la mbarali naambiwa inafika hadi laki 2 kwa ekari
baadhi ya sehemu za mvomero ni elfu 45 kwa ekari...............wadau wengine watakupa bei kwa maeneo yao lakini hujasema unataka kulima nini
Hivyo ushauri wangu ungeanza na mazao kama ya viungo, mf. Tangawizi ambayo soko liko njenje ndani na nje ya nchi na halina siasa humo ndani.
JF
Hali ya uchumi ni ngumu sana kwa watu wote hasa tunategemea mwisho wa mwezi. Weekend nilijaribu kupiga hesabu za mishahara yangu in next 10 years....ooooooooooops hazikufika hata 500millions Tshs.
Kwa maneno mengine kama sintantafuta kitu mbadala mbali na mshahara wangu cha kufanya basi nishakufa maskini na sintakuwa na chochote cha kuwaachia wanangu.
Maisha ni magumu sana kadri siku zinavyoenda mbele, sasa nimeamua kuanza kilimo kwa mara ya pili, awamu hii natumia mshahara wangu kama mtaji, nimewaambia kwa mara ya pili sababu kilimo cha kwanza nilifanya pamoja na wazazi wangu hadi nilipomaliza form four miaka hiyo, hicho hakikuwa na manufaa yeyote sababu ya mtaji na ufahamu.
Kwa sasa nimeanza na heka 50 ( 70m by 70m), nipo morogoro - pale Tuliani. Heka zote zimeshalimwa sasa tunapanda - nita expand my project up to 1,000 in next 3 - 5 years.
Makadirioni kwamba kila hekari average ni gunia 30, nitategemea kupata gunia 1500 za mahindi kutokana na hekari zangu za sasa 50. Kila gunia average selling price ni Tshs 60,000. kwa hiyo nitapata average Tshs 90m by July this year.
Running cost itakuwa approx 5m, so super profit ni 85m by July 2010.
Sasa 85m kwa mtu anayepokea sh 1million kwa mwezi ni mshahara wake wa miaka 7 na ushee-- teh teh teh teh
By next year nitaexpand to 200 hektas, nitalipima shamba langu na nijaribu kutafuta mikopo katika mabenki - or mbia toka SA au Zimbabwe. by 2015 wakati Dr Slaa anakuwa Rais wa nchi nitakuwa millionea. Sasa ole wenu mseme nimefanya ufisadi.
This is a challenge to you JF - hasa mnaopata less than 5m per month - think twice and join me.
Kumbuka shairi la darasa la nne - Kama mkitaka mali mtayapata shambani - huu ni wosia.