Ndio huko huko mkuu!nitazingatia maelekezo yako mkuu!una maanisha ndani ya siku 30 baada ya kupanda ni lazima nimuagilie tena mime regardless pana unyevu chini?au niko wrong mkuu?
maana yake ni kuwa katika siku 30 za mwanzo baada ya kupanda, ni lazima kuhakikisha kuna unyevu wa kutosha shambani. ni juu yako sasa kila uonapo unyevu umepungua, unaweka maji. njia rahisi kujuwa kuna unyevu au la ni kuzoa udongo wa juu kwenye kiganja na kufanya kama unakunja ngumi na kufeel unyevu kwa mikono yako.
Mungu akubariki sana mkuu!naomba nikusumbue na swali moja la mwisho!je ki utaalam ni mbegu itakayofaa kwa maeneo na mazingira hayo bado itakua ni STUKA (M1) ?ahsante sana mkuu
Nilikua namshauri ndugu yangu mmoja awe ana attend seminar za entrprenuership aboreshe biashara zake akannijibu hivi
'' yaani mtu ambaye hajawahi kuuza hata karanga akanifundishe biashara?
Stuka ndiyo mbegu nzuri kwa kilimo cha kiangazi kwani haihitaji maji mengi na hutumia muda mfupi kufikia hatua ya kuvunwa (mahindi ya kuchoma). Pia hindi lake ni kubwa na lina utamu sana. Mbegu ambazo usithubutu kupanda ni mbegu ya kienyeji, hii utapata hasasra vibaya mno.
Karibu tena
Ubarikiwe sana mkuu,kama nami shule nimepata ya kutosha hapa, kilichobaki ni utekelezaji tu,and let's hope for the best!usituchoke tu na wengine pale tutakapohitaji ushauri wa kitaalamu mkuu wangu!
Stuka ndiyo mbegu nzuri kwa kilimo cha kiangazi kwani haihitaji maji mengi na hutumia muda mfupi kufikia hatua ya kuvunwa (mahindi ya kuchoma). Pia hindi lake ni kubwa na lina utamu sana. Mbegu ambazo usithubutu kupanda ni mbegu ya kienyeji, hii utapata hasasra vibaya mno.
Karibu tena
Asante mkuu kwa kunielimisha. hata hivyo ktk context ya ujasiriamali wa kisasa, si rahisi kuwa na uhakika wa 100%. hii inatokana kiwango cha uwekezaji na uzalishaji husika. maana yangu ni kuwa ukiwekeza sh 50 elfu na ukapata mahindi 200, soko siyo tatizo kwani mtu mmoja atayaninuwa mara moja.ila ukiwa na mahidi laki moja na umwekeza milion 5, then kuwa na soko ni kitu cha msingi sana. asante na karibu sana tuendelee kuelimishana.
Mkuu nami naomba kuuliza,hivi kwa mahindi kuzaa mawili au zaidi kwa shina moja inategemea na mbegu au upandaji tu?
Nashukuru sana kaka kwa utaalam wako!Ok. Karibu. Hayo yote inategemea mahali shamba lilipo. Kama ni ukanda wa juu au wa chini, mfano mbeya, rukwa, ruvuma au mikoa ya pwani. Pili hutegemea na aina ya njia ya upatikanaji wa maji ikiwa ni ya mvua au unamwagilia. Kama mshauri, nitashindwa kukupa ushauri wa jumula kwani hautakusaidia. Ni vyema ueleze vema mahali shamba lilipo. Karibu tena
Nashukuru sana kaka kwa utaalam wako!
Swali langu ni kwamba kwa eneo kama la babati mkoa wa manyara ambapo huwa tunategemea mvua ni mbegu gani bora ya
1.Mahindi
2.Maharage
3.Mbaazi
4 Alizeti
Na ni kipindi gan ambacho ni sahihi kupanda haya mazao kwa mavuno mengi zaidi.
inategemea vitu viwili ama vitatu, lakini vya muhimu kabisa ni; upatikanaji wa raslimali (resources) za ukuaji kama maji, virutubisho; na muda uliopo kati ya kupanda na kukomaa kwa hindi husika, na muda huu hutegemea moja kwa moja na hali ya hewa ya sehemu yalikopandwa mahindi. mfano, ukanda wa pwani, mahindi na mazao mengine huchukuwa muda mfupi hadi kukomaa (siku 75-100) tofauti na sehem kama nyanda za juu kusini (siku 120-150 au zaidi). Kwa hiyo uwezekano wa kupata mahindi mawili katika shina ni mkubwa maeneo ya uwanda wa juu na ni mdogo maeneo ya pwani, hapa nafikiria kuwa mimea ya mahindi husika imepata maji na virutubisho sawa. Sababu hapa ni kuwa mimea hupata muda mwing kuweza kutengeneza biomass na hivyo huhitaji sehemu kubwa ya kuhifahdia, ndio maana magunzi mawili au zaidi utayakuta kwa vile ni kwa ajili ya kuhifadhi biomass iliyozalishwa kwa wingi. Kwa mahindi ambayo uzalishaji wake wa biomass ni mdogo kutokana na hali ya hewa au ukosefu wa maji na virutubisho, kwa vile biomass si ya kutosha, basi hindi moja ndio litakaloweza kutumika kuhifadhia, na yale mengine hufa kwani hakuna biomass ya ziada kuhifadhi. Hata hivyo, waweza pata hindi moja kwa kila shina hata ukiwa ukanda wa juu endapo maji na mbolea au virutubisho ni vya wasi wasi, na waweza kupata mahindi mawili ukanda wa pwani endapo maji, virutubisho ni vya kutosha na magonjwa na wadudu vimedhibitiwa bar a' bara. Naweza kuelezea zaidi muda ukiniruhusu au mtu yeyote akihitaji ilmu hii. Asante
mkuu naomba unisaidie, nafanyaje japo na mm nimiliki hata eka 20?