Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

Ndio huko huko mkuu!nitazingatia maelekezo yako mkuu!una maanisha ndani ya siku 30 baada ya kupanda ni lazima nimuagilie tena mime regardless pana unyevu chini?au niko wrong mkuu?

maana yake ni kuwa katika siku 30 za mwanzo baada ya kupanda, ni lazima kuhakikisha kuna unyevu wa kutosha shambani. ni juu yako sasa kila uonapo unyevu umepungua, unaweka maji.

Njia rahisi kujuwa kuna unyevu au la ni kuzoa udongo wa juu kwenye kiganja na kufanya kama unakunja ngumi na kufeel unyevu kwa mikono yako.
 
maana yake ni kuwa katika siku 30 za mwanzo baada ya kupanda, ni lazima kuhakikisha kuna unyevu wa kutosha shambani. ni juu yako sasa kila uonapo unyevu umepungua, unaweka maji. njia rahisi kujuwa kuna unyevu au la ni kuzoa udongo wa juu kwenye kiganja na kufanya kama unakunja ngumi na kufeel unyevu kwa mikono yako.



Mungu akubariki sana mkuu!naomba nikusumbue na swali moja la mwisho!je ki utaalam ni mbegu itakayofaa kwa maeneo na mazingira hayo bado itakua ni STUKA (M1) ?ahsante sana mkuu
 
Mungu akubariki sana mkuu!naomba nikusumbue na swali moja la mwisho!je ki utaalam ni mbegu itakayofaa kwa maeneo na mazingira hayo bado itakua ni STUKA (M1) ?ahsante sana mkuu

Stuka ndiyo mbegu nzuri kwa kilimo cha kiangazi kwani haihitaji maji mengi na hutumia muda mfupi kufikia hatua ya kuvunwa (mahindi ya kuchoma). Pia hindi lake ni kubwa na lina utamu sana. Mbegu ambazo usithubutu kupanda ni mbegu ya kienyeji, hii utapata hasasra vibaya mno.

Karibu tena
 
Nilikua namshauri ndugu yangu mmoja awe ana attend seminar za entrprenuership aboreshe biashara zake akannijibu hivi

'' yaani mtu ambaye hajawahi kuuza hata karanga akanifundishe biashara?

Labda yuko sahihi kwa kiwango flani. Mimi nafikiri mtu kuwa na uzoefu lazima kwanza utende kitu na uone matatizo yake na ujuwe jinsi ya kutatua, hapo ndio unaanza kubobea kuliko mtu kasoma kwenye kitabu tu halafu anakusimulia nadharia ambayo yeye binafsi ana mashaka nayo maana hajawahiona kama ni kweli au la.
 
Stuka ndiyo mbegu nzuri kwa kilimo cha kiangazi kwani haihitaji maji mengi na hutumia muda mfupi kufikia hatua ya kuvunwa (mahindi ya kuchoma). Pia hindi lake ni kubwa na lina utamu sana. Mbegu ambazo usithubutu kupanda ni mbegu ya kienyeji, hii utapata hasasra vibaya mno.

Karibu tena

Ubarikiwe sana mkuu,kama nami shule nimepata ya kutosha hapa, kilichobaki ni utekelezaji tu,and let's hope for the best!usituchoke tu na wengine pale tutakapohitaji ushauri wa kitaalamu mkuu wangu!
 
Ubarikiwe sana mkuu,kama nami shule nimepata ya kutosha hapa, kilichobaki ni utekelezaji tu,and let's hope for the best!usituchoke tu na wengine pale tutakapohitaji ushauri wa kitaalamu mkuu wangu!

Karibu sana. Nimepata hii taaluma bure na nitaitoa bure kwa Watanzania wenzangu bila kujali kabila, kiwango cha elimu, anakofanyia kazi au jinsia.. hahaa. Karibu tena.
 
Stuka ndiyo mbegu nzuri kwa kilimo cha kiangazi kwani haihitaji maji mengi na hutumia muda mfupi kufikia hatua ya kuvunwa (mahindi ya kuchoma). Pia hindi lake ni kubwa na lina utamu sana. Mbegu ambazo usithubutu kupanda ni mbegu ya kienyeji, hii utapata hasasra vibaya mno.

Karibu tena

Mkuu ninachoweza kusema ni asante sana!nimepata kila kitu kupitia darasa lako,sasa natakiwa kufaulu mtihani tu,ahsante sana ndugu,nitarudi na mrejesho hapa
 
Mimi nina mbolea nzuri sana ya kuboost hayo mahindi na mazao mengine ni costless hakika tuwasiliane juu ya kuipata hii huduma yangu.Kilimo kwanza Oyeeeeeeeew
 
Asante mkuu kwa kunielimisha. hata hivyo ktk context ya ujasiriamali wa kisasa, si rahisi kuwa na uhakika wa 100%. hii inatokana kiwango cha uwekezaji na uzalishaji husika. maana yangu ni kuwa ukiwekeza sh 50 elfu na ukapata mahindi 200, soko siyo tatizo kwani mtu mmoja atayaninuwa mara moja.ila ukiwa na mahidi laki moja na umwekeza milion 5, then kuwa na soko ni kitu cha msingi sana. asante na karibu sana tuendelee kuelimishana.

Mkuu nami naomba kuuliza,hivi kwa mahindi kuzaa mawili au zaidi kwa shina moja inategemea na mbegu au upandaji tu?
 
Mkuu nami naomba kuuliza,hivi kwa mahindi kuzaa mawili au zaidi kwa shina moja inategemea na mbegu au upandaji tu?

inategemea vitu viwili ama vitatu, lakini vya muhimu kabisa ni; upatikanaji wa raslimali (resources) za ukuaji kama maji, virutubisho; na muda uliopo kati ya kupanda na kukomaa kwa hindi husika, na muda huu hutegemea moja kwa moja na hali ya hewa ya sehemu yalikopandwa mahindi. mfano, ukanda wa pwani, mahindi na mazao mengine huchukuwa muda mfupi hadi kukomaa (siku 75-100) tofauti na sehem kama nyanda za juu kusini (siku 120-150 au zaidi).

Kwa hiyo uwezekano wa kupata mahindi mawili katika shina ni mkubwa maeneo ya uwanda wa juu na ni mdogo maeneo ya pwani, hapa nafikiria kuwa mimea ya mahindi husika imepata maji na virutubisho sawa.

Sababu hapa ni kuwa mimea hupata muda mwing kuweza kutengeneza biomass na hivyo huhitaji sehemu kubwa ya kuhifahdia, ndio maana magunzi mawili au zaidi utayakuta kwa vile ni kwa ajili ya kuhifadhi biomass iliyozalishwa kwa wingi.

Kwa mahindi ambayo uzalishaji wake wa biomass ni mdogo kutokana na hali ya hewa au ukosefu wa maji na virutubisho, kwa vile biomass si ya kutosha, basi hindi moja ndio litakaloweza kutumika kuhifadhia, na yale mengine hufa kwani hakuna biomass ya ziada kuhifadhi.

Hata hivyo, waweza pata hindi moja kwa kila shina hata ukiwa ukanda wa juu endapo maji na mbolea au virutubisho ni vya wasi wasi, na waweza kupata mahindi mawili ukanda wa pwani endapo maji, virutubisho ni vya kutosha na magonjwa na wadudu vimedhibitiwa bar a' bara.

Naweza kuelezea zaidi muda ukiniruhusu au mtu yeyote akihitaji ilmu hii. Asante
 
Wakuu.
Ni mbegu ya aina gani ya mahindi nzuri inafaa kupanda ukanda wa kasikazini
 
Ok. Karibu. Hayo yote inategemea mahali shamba lilipo. Kama ni ukanda wa juu au wa chini, mfano mbeya, rukwa, ruvuma au mikoa ya pwani. Pili hutegemea na aina ya njia ya upatikanaji wa maji ikiwa ni ya mvua au unamwagilia. Kama mshauri, nitashindwa kukupa ushauri wa jumula kwani hautakusaidia. Ni vyema ueleze vema mahali shamba lilipo. Karibu tena
Nashukuru sana kaka kwa utaalam wako!
Swali langu ni kwamba kwa eneo kama la babati mkoa wa manyara ambapo huwa tunategemea mvua ni mbegu gani bora ya
1.Mahindi
2.Maharage
3.Mbaazi
4 Alizeti

Na ni kipindi gan ambacho ni sahihi kupanda haya mazao kwa mavuno mengi zaidi.
 
Nashukuru sana kaka kwa utaalam wako!
Swali langu ni kwamba kwa eneo kama la babati mkoa wa manyara ambapo huwa tunategemea mvua ni mbegu gani bora ya
1.Mahindi
2.Maharage
3.Mbaazi
4 Alizeti

Na ni kipindi gan ambacho ni sahihi kupanda haya mazao kwa mavuno mengi zaidi.

Nashukuru kwa swali nitarudi baadaye kidogo. Kwa vile mimi nimebobea katika mahindi, basi nitajibu point moja. nadhani wenzangu wa mazao mengine sasa ni wakati wao wa kutoa darsa muj'arab. Subiri kidogo nitarudi
 
inategemea vitu viwili ama vitatu, lakini vya muhimu kabisa ni; upatikanaji wa raslimali (resources) za ukuaji kama maji, virutubisho; na muda uliopo kati ya kupanda na kukomaa kwa hindi husika, na muda huu hutegemea moja kwa moja na hali ya hewa ya sehemu yalikopandwa mahindi. mfano, ukanda wa pwani, mahindi na mazao mengine huchukuwa muda mfupi hadi kukomaa (siku 75-100) tofauti na sehem kama nyanda za juu kusini (siku 120-150 au zaidi). Kwa hiyo uwezekano wa kupata mahindi mawili katika shina ni mkubwa maeneo ya uwanda wa juu na ni mdogo maeneo ya pwani, hapa nafikiria kuwa mimea ya mahindi husika imepata maji na virutubisho sawa. Sababu hapa ni kuwa mimea hupata muda mwing kuweza kutengeneza biomass na hivyo huhitaji sehemu kubwa ya kuhifahdia, ndio maana magunzi mawili au zaidi utayakuta kwa vile ni kwa ajili ya kuhifadhi biomass iliyozalishwa kwa wingi. Kwa mahindi ambayo uzalishaji wake wa biomass ni mdogo kutokana na hali ya hewa au ukosefu wa maji na virutubisho, kwa vile biomass si ya kutosha, basi hindi moja ndio litakaloweza kutumika kuhifadhia, na yale mengine hufa kwani hakuna biomass ya ziada kuhifadhi. Hata hivyo, waweza pata hindi moja kwa kila shina hata ukiwa ukanda wa juu endapo maji na mbolea au virutubisho ni vya wasi wasi, na waweza kupata mahindi mawili ukanda wa pwani endapo maji, virutubisho ni vya kutosha na magonjwa na wadudu vimedhibitiwa bar a' bara. Naweza kuelezea zaidi muda ukiniruhusu au mtu yeyote akihitaji ilmu hii. Asante

Asante sana mkuu kwa darasa ili lililoshiba!ubarikiwe sana na uendelee na moyo huo
 
El Nino naona makadirio ndio yalimuangusha mambo ya kulima hekari 50 kwa TZS 5M na hekari moja gunia 30 duh!

Wakati wataalam wanasema expenses inabidi tuziweke makadirio ya juu na kipato kadirio la chini kabisa.
 
mkuu naomba unisaidie, nafanyaje japo na mm nimiliki hata eka 20?

Nenda Vigwaza/Mkuranga kamata pori kisha endelea na uwekezaji. Mbona mipori iko mingi sana. Toka Moro mpaka Iringa ni pori tupu,Mkuranga hadi Mtwara ni pori tupu,wewe unataka wapi?
 
Nataka kufanya project ya majaribio,kwa mtaji wa 3M,kilimo cha ufuta na mahindi.Eneo ni Dodoma vijijini.
PLANI YANGU: Nataka kulima kwa umwagiliaji maana kuna bwawa kubwa,karibu yake ntatafuta eneo la acres zisizopungua 10,ili iwe rahisi kuvuta maji kwa mashine na kumwagilia kwenye shamba langu.
Kama kuna mtu mwenye ujuzi wowote unaohisiana na hii project naomba anisaidie,hasa kuhusu;

1. Mashine ya maji yenye uwezo gani inafaa,na bei yake.Pia kama ni vizur kutafuta mashine moja kubwa au kununua ndogo ndogo zaidi ya moja.

2. Bei ya mabomba ya kumwagilia,na kama kuna uhusiano wowote wa umbali toka maji yalipo na aina za mabomba au uwezo wa mashine.

3. Estimation za kias cha mahindi nachoweza kupata kwa acre moja

4. Ujuzi wowote wa mbolea za kukuzia+madawa incase kama yatahitajika.

5. Kama kuna site yoyote au kitabu chenye kuelezea vitu kuhusu hii project itakuwa poa pia kama utanambia.(Currently nnaresearch kuhusu hii kitu kwa kutumia google so usije ukianambia nigoogle)

6. Niko interested zaid na uwezo wa mashine ya maji in relation to distance toka bwawani coz nadhan hili ni hitaji lenye gharama kubwa ya mara moja.

7. Mwenye ujuzi pia wa mifereji anaweza akanimegea.
 
Sijakuelewa vizuri,ufuta haifai kw umwagiliaji,mahndi sawa
 
Elnino

Ulipost hii thread mwaka 2010, sasa huu ni mwaka 2014, vp ungependa kutupa feedback ili kuwainspire na wengine as watu wengi walikusupport na nina imani wanapenda kusikia kutoka kwako.
 
Back
Top Bottom