inategemea vitu viwili ama vitatu, lakini vya muhimu kabisa ni; upatikanaji wa raslimali (resources) za ukuaji kama maji, virutubisho; na muda uliopo kati ya kupanda na kukomaa kwa hindi husika, na muda huu hutegemea moja kwa moja na hali ya hewa ya sehemu yalikopandwa mahindi. mfano, ukanda wa pwani, mahindi na mazao mengine huchukuwa muda mfupi hadi kukomaa (siku 75-100) tofauti na sehem kama nyanda za juu kusini (siku 120-150 au zaidi). Kwa hiyo uwezekano wa kupata mahindi mawili katika shina ni mkubwa maeneo ya uwanda wa juu na ni mdogo maeneo ya pwani, hapa nafikiria kuwa mimea ya mahindi husika imepata maji na virutubisho sawa. Sababu hapa ni kuwa mimea hupata muda mwing kuweza kutengeneza biomass na hivyo huhitaji sehemu kubwa ya kuhifahdia, ndio maana magunzi mawili au zaidi utayakuta kwa vile ni kwa ajili ya kuhifadhi biomass iliyozalishwa kwa wingi. Kwa mahindi ambayo uzalishaji wake wa biomass ni mdogo kutokana na hali ya hewa au ukosefu wa maji na virutubisho, kwa vile biomass si ya kutosha, basi hindi moja ndio litakaloweza kutumika kuhifadhia, na yale mengine hufa kwani hakuna biomass ya ziada kuhifadhi. Hata hivyo, waweza pata hindi moja kwa kila shina hata ukiwa ukanda wa juu endapo maji na mbolea au virutubisho ni vya wasi wasi, na waweza kupata mahindi mawili ukanda wa pwani endapo maji, virutubisho ni vya kutosha na magonjwa na wadudu vimedhibitiwa bar a' bara. Naweza kuelezea zaidi muda ukiniruhusu au mtu yeyote akihitaji ilmu hii. Asante