Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

JF

Hali ya uchumi ni ngumu sana kwa watu wote hasa tunategemea mwisho wa mwezi. Weekend nilijaribu kupiga hesabu za mishahara yangu in next 10 years....ooooooooooops hazikufika hata 500millions Tshs.

Kwa maneno mengine kama sintantafuta kitu mbadala mbali na mshahara wangu cha kufanya basi nishakufa maskini na sintakuwa na chochote cha kuwaachia wanangu.

Maisha ni magumu sana kadri siku zinavyoenda mbele, sasa nimeamua kuanza kilimo kwa mara ya pili, awamu hii natumia mshahara wangu kama mtaji, nimewaambia kwa mara ya pili sababu kilimo cha kwanza nilifanya pamoja na wazazi wangu hadi nilipomaliza form four miaka hiyo, hicho hakikuwa na manufaa yeyote sababu ya mtaji na ufahamu.

Kwa sasa nimeanza na heka 50 ( 70m by 70m), nipo morogoro - pale Tuliani. Heka zote zimeshalimwa sasa tunapanda - nita expand my project up to 1,000 in next 3 - 5 years.

Makadirioni kwamba kila hekari average ni gunia 30, nitategemea kupata gunia 1500 za mahindi kutokana na hekari zangu za sasa 50. Kila gunia average selling price ni Tshs 60,000. kwa hiyo nitapata average Tshs 90m by July this year.

Running cost itakuwa approx 5m, so super profit ni 85m by July 2010.

Sasa 85m kwa mtu anayepokea sh 1million kwa mwezi ni mshahara wake wa miaka 7 na ushee-- teh teh teh teh

By next year nitaexpand to 200 hektas, nitalipima shamba langu na nijaribu kutafuta mikopo katika mabenki - or mbia toka SA au Zimbabwe. by 2015 wakati Dr Slaa anakuwa Rais wa nchi nitakuwa millionea. Sasa ole wenu mseme nimefanya ufisadi.

This is a challenge to you JF - hasa mnaopata less than 5m per month - think twice and join me.

Kumbuka shairi la darasa la nne - Kama mkitaka mali mtayapata shambani - huu ni wosia.




bosi tunaomba matokeo. Mana na sisi wengne twataka kuingia kwenye kilimo. je ulifanikiwa. na kama hukufanikiwa je changamoto gani zilikuzuia. Mana ni mda tangu 2010.
 
Wakuu salaam,
Wakuu ninaomba kujulishwa kutoka kwa wataalu nikiwa na imani JF ni kila kitu.

Ninashamba langu heka tatu nimefikiri nilime mahindi kisasa zaidi.

Nimehamamisika kwani shamba limefikiwa na maji ya serikali ambayo lita eflu moja yanauzwa wastani tsh 1500.

Mahindi hukomaa kwa meizi mitatu lakini nikiwa na imani hayohitaji maji kila siku pia kama nitapata muongozo kutoka kwa wataalu ni vema.

Naomba kujuzwa heka moja ya mahindi kwa mfumo huu wa umwagiliaji kwa njia ya drip nitahitaji lita ngapi za maji kwa heka moja kwa mwezi. Nimevutwa kuuliza hili kwani ninapopitia ushuri wa watu mbalimbali humu mfumo huu wa umwagiliaji kwa njia ya drip huhitaji maji kidogo sana.

Lengo ni kufahamu ili niweze kufanya tathmini ya gharama nitakazozitumia nilinganishe na mavuno ili nifaham kama kutakua na faida nijitose.
 
Haya sasa wataalamu wetu wa kilimo Sua na wengine mje kutoa nondo mdau amejipanga kukiendeleza kilimo kwa kilimo cha kisasa msijifanye hamuuoni uzi huu.
 
Daa wataalamu naona wana view kisha wanapita kimya mkuu,ngoja tuendelee vuta subira huenda kwenye viewers wa sasa nao wanasubiri mtaalam@nasemanao
 
Mkuu unataka kulima mahindi ya aina gani? Yaan yafike stage gani?
 
Kuhusu stage mkuu naweza vuma yakiwa mabichi ama makavu kutegemeana na option ipi yenye faida zaidi@yonga
 
makavu yatakuwa hayana faida sana, mabichi unaweza pata faida vizuri, mahindi kwa drip inawezekana vizuri,faida itakuwepo baada ya miaka kadhaa sababu cost kubwa itakuwa kutandaza mabomba shamba zima na kuweka matundu kwenye hilo bomba ambapo zinakaa emmiters
 
1. Unatakiwa uwe na chanzo kizuri cha maji ikiwa mto au bwawa au kisima ambacho vizuri ukawa na tank la kuhifadhia maji

2. Unatakiwa uwe na pressure regulator maana ili maji yatoke kwa matone inatakiwa pressure isizidi 20 psi inategemea na urefu wa bomba zako zinakoenda na vilevile chanzo chako cha maji
 
Asante mkuu japo bado hujakata kiu yangu, Lengo langu ni kufaham heka moja ya mahindi itahitaji lita ngapi za maji tangu kupanda mpaka kukomaa.
Kumbuka chanzo changu cha maji ni majibya serikali ambayo nitayanunua kwa 1500 kwa lita 1000.

Kama sitopata majibu ya kiasi cha maji nitakayoyatumia huenda nikajikua natumia maji mengi na gharama ikawa kubwa@yonga
 
Wakuu nimekuwa nikipata tetesi kuhusu huu mradi na faida zake! Najua kuna watu humu ni wazoefu naomba tushirikishane kwasababu mwezi wa saba nataka niingie shambani!

Asanteni
 
Mahindi kwa drip? Mkuu naona unataka tu kupoteza hela bure, kama shamba linafikiwa na maji kwa urahisi bora unyweshe tu kwa kutumia mirereji inakua nzuri zaidi kwa kilimo cha mahindi.

Drip ni nzuri kama wataka lima mbogamboga na matunda.
 
Asante mkuu kwa ushauri,lakini drip irrigation sio kwaajili ya mbogamboga pekee.Drip irrigation ni mfumbo ambao nchi nyingi duniani hutumia kwa sasa kwenye kilimo cha mahindi.

Unaweza tizama mto kama ruvu ukaona yale maji ni mengi sana ila kama kutatokea wakulima wakubwa na wakafanya irrigation kwakutumia mitaro hayo maji hayatotosha.

Niko na utube video za wakulima wakubwa wa mahindi ulaya wanafanya drip irrigation ila cm ninayotumia nashindwa kiweka hapa@dudupori
 
nilichojifunza kwenye kilimo ni kuwa wengi huingia wakitzama faida zaidi bila ya kufikiri labda changamoto ambazo huenda watakutana nazo.

So mtu anapokuwa katizama faida zaidi kasheshe huja pale anapokuwa kaingia kwenye kilimo. Hukutana na changamoto kibao ambazo huenda hakuzitarajia.

Ukweli ni kwamba mambo si raisi hivyo.
Lazima utizame faida na changamoto ambazo zinaweza kujitokeza. Kilimo huwa hivi Mwaka ambao mavuno huwa mazuri,changamoyo huamia kwenye upande wa soko. Kwani mazao huwa mengi na kusababisha bei kushuka.

Mwaka mavuno yakiwa hafifu. soko nalo huwa zuri sana.

Nimepanga kujiingiza kwenye kilimo.
Ukweli ni kuwa JF imenisaidia kugundua mambo mengi sana kabla sijajiingiza kwenye kilimo na ufugaji.

Nitajitosa tu hivo hivo lakini nikitarajia kukutana na changamoto kadha wa kadha.
 
Asante mkuu kwa ushauri,lakini drip irrigation sio kwaajili ya mbogamboga pekee.Drip irrigation ni mfumbo ambao nchi nyingi duniani hutumia kwa sasa kwenye kilimo cha mahindi.
Unaweza tizama mto kama ruvu ukaona yale maji ni mengi sana ila kama kutatokea wakulima wakubwa na wakafanya irrigation kwakutumia mitaro hayo maji hayatotosha.
Niko na utube video za wakulima wakubwa wa mahindi ulaya wanafanya drip irrigation ila cm ninayotumia nashindwa kiweka hapa@dudupori
Mkuu hata mimi nina wazo la kufanya hiki kilimo na nimeanzisha uzi hapa kabla sijauona huu uzi wako kwani maudhui yanafanana kabisa, ingawa mimi nataka kujua gharama za kutandaza mabomba kwa shamba la ekari moja, kama unajua gharama za mabomba naomba nisaidie mkuu.
 
Bwana kateka ukitaka kupata namba za mafundi wanao tandaza mabomba kwaajili ya drip irrigation ingia kwenye thread za green house zipo humu jamvini nyingi tu ni rahisi kuwapata.

Jaribu kufungua moja baada ya nyingine
 
09e33ae8f62873cdf7816cc3292eb107.jpg


Inawezekana hiyo hapo mie nafanya mkuu na inalipa
 
Mahindi mabichi ya lipa lakini kwa kutumia drip illigation ni Kama nguvu kubwa inatumika hivyo ushauri wangu Kama unaweza kunywesha ni vizuri zaidi na bado utakua umelima kisasa na hiyo drip system ukaitafutia zao ambalo lita ku conducive mfano nyanya, hoho, tikiti, vitunguu swaumu, au hata ginger.
 
Mahindi kwa drip? Mkuu naona unataka tu kupoteza hela bure, kama shamba linafikiwa na maji kwa urahisi bora unyweshe tu kwa kutumia mirereji inakua nzuri zaidi kwa kilimo cha mahindi. Drip ni nzuri kama wataka lima mbogamboga na matunda.....
Inabidi tubadilike kulingana na technology inapoelekea enzi za jembe na bifu za kupigania maji ya miferegi Inabidi kama mtu una uwezo udeal na teknolojia zaidi.
 
Back
Top Bottom