Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

Mbona nasikia kuwa kuna ugomvi mkubwa sana kati ya wakulima na wafugaji,Je Kiteto itakuwa mahali salama pa kulima?.
 
Mtoto ya Tima hongera sana kilimo kinalipa. Haswa ukikodi hecre nyingi at least kwanzia 50 na kwendelea. Sasa mi shida yangu kiteto yiko kwenye kumwagilia
Hakuna kilimo cha umwagiliaji kiteto,wanategemea mvua pekee,hapo ni kuomba Mungu tu lakini pia jitahidi upate shamba ambalo bado linarutuba.

Mwaka juzi kulikua na migogoro ya wakulima na wafugaji,kwakweli kulitokea mauwaji yakutisha na wakulima wengi walishindwa kabisa kwenda kuvuna mazao yao mashambani,

Vita hii ilianzia eneo wanaita Multangosi na kusambaa eneo kubwa mpaka maeneo jirani na mkoa wa dodoma kwani kiteto imepaka na dodoma,baadhi ya maeneo kama Kibaigwa pia vita hii iliathiri.

Ila kwa kwa sasa hali ni shwari,
Kila la heri!
 
chardams nami naulizia kilimo cha umwagiliaji huko kiteto. Tunasubiria majibu. Alafu naona uko vizuri katika ufafanuzi wako. Mungu akuzidishie

Hapana tunategemea mvua

nilikuwa huko wiki iliyopita mvua ndio zinaanza, ila sishauri kulima wakati huu maana mvua za mwezi wa 12 haziaminiki.

mda mzuri wa kulima ni mwezi wa kwanza mwishoni.
 
Asante kwa ushauli wako mi nimesha anzaa. Ila bado kulima
 
Umepata michango ya kukupa moyo mkuu lakini mi nakukumbusha kuwa l hekta =l00m by l00m na sio 70m by 70m. Pili umelenga umwagiliaji au rehema za Mungu kama ni umwagiliji nakupa hongera na kama ni mvua za Mungu basi usijipe matumaini kupitiliza usijeukasema pekee yako barabarani. Kumbuka nguvu ya soko inategemea mahitaji hilo nalo jiandae nalo. Kuna wadudu wanyama na ndege waharibifu nalo pia jiandae.yapo na mengine wanzangu watanisaidia kujazia vinginevyo nakupa HONGERA SANA wasomi wanatakiwa sasa mashambani kuibadili TIIZEEDII YETU
100m kwa 100m ni hekta 1 ambayo ni sawa na ekari 2na nusu ekari ni vipimo vya british system wakati hekta ni metric system. maoni yako ni mazuri sana
 
Hakuna kilimo cha umwagiliaji kiteto,wanategemea mvua pekee,hapo ni kuomba Mungu tu lakini pia jitahidi upate shamba ambalo bado linarutuba.

Mwaka juzi kulikua na migogoro ya wakulima na wafugaji,kwakweli kulitokea mauwaji yakutisha na wakulima wengi walishindwa kabisa kwenda kuvuna mazao yao mashambani,

Vita hii ilianzia eneo wanaita Multangosi na kusambaa eneo kubwa mpaka maeneo jirani na mkoa wa dodoma kwani kiteto imepaka na dodoma,baadhi ya maeneo kama Kibaigwa pia vita hii iliathiri.

Ila kwa kwa sasa hali ni shwari,
Kila la heri!
Hivi cwezi ku drill maji kutoka chini kwakutumia motar
 
Nafikiri swali lako halijakaa sawa ila nitajibu kwa namna nafikiri umemaanisha;

Ku drill kisima yapo makampuni yanamitambo maalum,bei zao hu charge kwa mita,bei ya mita moja hutegemeana na mambo mengi kama ugumu wa mwamba wa eneo husika,umbali kutoka ulipo na huko utakapoitoa kampuni ya uchimbaji,

Mfano kwa ndani ya dar es salam yapo ma kampuni yanayochimba mita moja kwa 70,000 lakini kama ni maeneo ya mkoa wa pwani kama kibaha,chalinze,bagamoyo wanachimba kwa 100,000 mpaka 120,000.

Nje ya hapo zipo gharama za water saveying ambazo mara nyingi ni kati ya 400,000 hivi.

Wakimaliza kukuchimbia watakufungia water pump ambayo itahitaji umeme hivyo kama kisima kipo shamba na hakuna umeme basi itakuhitaji generator.

Natumai nimejibu swali lako,
thnx!
 
Umenijibu vizuri. Maana tulikua tunataka kuchimba kisima kabisa japo inaweza kukost pesa nyingi. Kwahyo kiteto wanaweza hawa jama kufanya kwashingapi
 
Nakushauri kama ni kiteto kampuni ya uchimbaji uchukulie dodoma kwani ni jirani sana na kiteto gharama inaweza kuwa 120000 kwa mita,

Kama lengo ni kilimo na wewe unaishi Dar es salaam nakushauri tafuta mashamba mkoa wa Tanga ama Morogoro napo kwakilimo ni kuzuri sana hivyo itakuwia rahisi kwenye usimamizi wa shughuli zako kwani ni jirani na Dar es salaam.
 
Shukurani sana. Nkija tena kiteto ntakutafta
 
Ok ni vema lakini ninamuda kidogo sipo huko kutokana na mambo ya kazi zangu zilivyo, ila ni mwenyeji sana kwani nimekua na kusoma huko ni nyumbani, hivyo naweza kushauri kwa kadiri ya kile nafahamu.

Kila heri.
 
Salaam wakuu.

Msimu huu nimeandaa shamba nataka kulima mahindi. Mnisaidie maswali yafuatayo:
1. Nini tofauti ya mbegu za muda mfupi na mrefu kuhusu kiasi cha magunia unayopata kwa eka?
2. Ni mbegu gani nzuri kupanda huku kwetu Iringa ili nipate mavuno makubwa.
3. Naitaji kg ngapi za mbegu kwa kila eka?.
4. Ni dawa gani zinafaa kupandia na bei zake zikoje?

Pia nakaribisha ushauri wowote kuhusu kilimo cha mahindi.

Asanteni
 
Habari wandugu, ashukuliwe Mungu kuwa tuwazima na anatupigania kwenye changamoto za maisha.
Kwa hali ya kiuchumi ilivyo kwa sasa inatubidi kutafuta miradi tofauti tofauti ili kumudu hali ya sasa. Kwa mtazamo wangu naona sasa ipo haja ya kuitumia ardhi tulio nayo kutuletea maendeleo na sio kukaa na kulalamikia hali ngumu ya maisha.
Katika hayo naombeni kujuzwa kuhusu kilimo. Cha;

1: maparachichi.
Kilimo hiki kipoje, kinahitaji hali ya hewa ya namna gani?
Ni maeneo yepi hapa nchini yanafaa kwa kilimo hiki.?
Vipi kuhusu masoko yapoje?

2:. Matikiti major:
Hapa pia naomba kujuzwa, nifanye nini ikiwa nataka kulima matikiti maji,
Changamoto zake zikoje?

3: Mahindi:
Kilimo hiki kinaonekana kudharaulika lakini kila uchao unga unapanda bei.
Hivi ni njia zipi Bora za kilimo cha mahindi?
Ni mbegu zipi ni bora zaidi kwa hapa nchini hasa kwa mkoa wa morogoro?

Kwa wale wataalamu wa kilimo naomba mnijuze hayo, naamini itasaidia wengi wenye nia kama yangu.
Natanguliza shukurani zangu kwenu.
 
Kwa Mvua Za Mwaka Huu Hazina Uhakika Sana, Labda Za Masika, Nakushauri Tengeneza Mashimo Makubwa Kiasi Yenye Kutuamisha Maji Kwenye Shina Ili Mvua Kidogo Utakayopata Ituamishe Maji Ya Kutosha
 
Salaam wakuu.

Msimu huu nimeandaa shamba nataka kulima mahindi. Mnisaidie maswali yafuatayo:
1. Nini tofauti ya mbegu za muda mfupi na mrefu kuhusu kiasi cha magunia unayopata kwa eka?
2. Ni mbegu gani nzuri kupanda huku kwetu Iringa ili nipate mavuno makubwa.
3. Naitaji kg ngapi za mbegu kwa kila eka?.
4. Ni dawa gani zinafaa kupandia na bei zake zikoje?

Pia nakaribisha ushauri wowote kuhusu kilimo cha mahindi.

Asanteni
Tafuta mbegu za hybrid ni nzuri sana zinazaa mahindi mawili mawili, panda mbegu ya muda mfupi ndugu
 
Back
Top Bottom