Nimeamua 'kusilimu' je, kisheria na kiimani nitaruhusiwa kuongeza wake nikihitaji?

Anabakije kuwa mke wangu nakati siwezi tena kutekeleza masharti ya mkataba wetu wa kikristo?
 
Labda kwa wakristo ila katika uislam hiyo kitu hakunaga,kumbuka mtoa mada atakuwa tayari ni muislam kiimani ambapo uhusiano wake uliokuwa na mke wake pia uliunganishwa kiimani,sasa imani tofauti.
Pili hivyo vyeti vinauzwa,kwhiyo c kigezo cha kutoachana!
 
1&2 HAPANA.. Sheria ya mikataba hairuhusu.. Mkataba hauwezi vunjwa na pande moja bila ya maridhiano na pande nyingine.
3. NDIYO.. Kwa kuwa pande mbili zimebadilisha dini kwa ridhaa ina maana mkataba wa awali ni obsolete kwa hiyo mtatumia mkataba mpya wa sheria za ndoa za kiislam.
 
Uhuru wa kuabudu unakujaje sasa. Coz kuongeza wake ni suna na tena ni ibada (kwa imani ya kiislam, nadhani) kama utaamua kuoa mjane. Sasa iweje pawe na mkataba unaokupunguzia uhuru wako wa kuabudu coz mke/mume anaweza asiridhie kuvunja mkataba
 
1. Ndoa itakuwa imevunjika, kwa sababu utakuwa umevunja msingi mmojawapo wa ndoa ambao ni dini
2. Kama wewe umesilimu na yeye kabaki kwenye ukristo, mtakuwa mnazini. Endapo utaoa mke mwingine na hata kufika wanne itakuwa ni sahihi
3. Kama mtasilimu wote, na mlikuwa katika ndoa ambayo ilifungwa katika taratibu sahihi za dini mliyotoka au hata kimila, hakutakuwa na haja ya kufunga ndoa nyingine. Uislamu unatambua ndoa za dini nyingine
 
Kwa upande hio hakuna tatzo we oa tu utakavyo
 
Asante kwa maelezo mazuri mkuu
 
Usitoe majibu kwa jambo usilokuwa na elimu nalo
 
Namba 2 bado ina utata mkuu, unaizungumziaje aya ya Quran inayosema ".....mmeruhusiwa kuwaoa waliopewa kitabu...."??. Kumbuka nyakati za maswahaba wapo waliokuwa wanaishi na wanawake wa kiyahudi licha ya kuwa wanawake hao hawakuwa wamesilimu na mtume hakuwambia kuwa ndoa zao ni batili.
Maswali haya kwa sehemu kubwa ni ya kisharia yanatakiwa kujibiwa na wanazuoni. Kwa nilivopata elimu kidogo ni kuwa wote wakibadili dini ndoa inabaki ile ile ya awali. Ila mmoja akibadili kwakweli sifahamu.
 
Good, tupate ufafanuzi hapo
 
Ndoa zilikuwepo hata kabla ya Mtume Muhammad (saw). Mayahudi na Makureishi walikuwa na taratibu za ndoa, na Mtume (saw) alikuja kuhitimilisha, wala hakuja kutengua. Na elewa kuwa maswahaba wengi walisilimu wao na wake zao ukiondoa kina Sayyidna Ally (ra)
 
Good, tupate ufafanuzi hapo
Mtume Muhammad (saw) hakuwafungisha upya ndoa maswahaba walio silimu. Hiyo ya kuwaambia waoeni waliopewa kitabu ilikuwa ni kuwapa faraja wanawake waliosilimu, jambo ambalo mpaka leo linasisitizwa
 
Kama MMEOANA kikristo na ukabadili dini...ndoa hakuna,,,ila kama mlioana KIISLAM halafu mmoja akabadili kuwa mkristo ndoa ipo pale pale....na hata ukiongeza mke mwingine bado atabaki ni mkeo...
 

1. Ndio sheria itaendelea kumtambua mke wa kikristo kwani mwanaume muislam anaweza kuwa na ndoa na mtu ambae ni ahlul kitab.
2. Ndio
3. Hakuna haja ya kufunga ndoa upya kwani Uislamu inatambua ndoa ilimradi iwe imefata taratibu za kidini.
Uislamu unatambua ndoa yoyote ilimradi iwe imefata taratibu za kidini, muislam mwanaume ameruhusiwa kuoa mwanamke asiekuwa muislam, pia kama akimsilimisha ni vizuri zaidi, lakini kama mlioana kwa dini nyongine baadae mkasilimu basi hakuna haja ya kuoana upya, na kama mwanamke akiamua kubaki kule kule kwenye dini yake basi haibatilishi ndoa. Na bado huyo mwanamke atatambulika kama mke wako.
 
MKE atambuliki kama ataamua kubaki
Kwani mke hatambuliki wakati uislamu unaruhusu mwanaume kuoa mwanamke ambae ni ahlul kitab, ijapokuwa ni bora zaidi ukimsilimisha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…