Nimeamua 'kusilimu' je, kisheria na kiimani nitaruhusiwa kuongeza wake nikihitaji?

Nimeamua 'kusilimu' je, kisheria na kiimani nitaruhusiwa kuongeza wake nikihitaji?

1. Ndio sheria itaendelea kumtambua mke wa kikristo kwani mwanaume muislam anaweza kuwa na ndoa na mtu ambae ni ahlul kitab.
2. Ndio
3. Hakuna haja ya kufunga ndoa upya kwani Uislamu inatambua ndoa ilimradi iwe imefata taratibu za kidini.
Uislamu unatambua ndoa yoyote ilimradi iwe imefata taratibu za kidini, muislam mwanaume ameruhusiwa kuoa mwanamke asiekuwa muislam, pia kama akimsilimisha ni vizuri zaidi, lakini kama mlioana kwa dini nyongine baadae mkasilimu basi hakuna haja ya kuoana upya, na kama mwanamke akiamua kubaki kule kule kwenye dini yake basi haibatilishi ndoa. Na bado huyo mwanamke atatambulika kama mke wako.
Haya ndio majibu sahihi...kuna watu humu wanatoa majibu kwa hisia na bila kuwa na ilmu ya mada husika..jambo ambalo ni kosa kisheria.
 
Mwenyezi MUNGU asingewataja kwenye Quran kama hawapo. Kumbuka hata waislam wamebadilika sana, zama za mtume hakukuwa na madhehebu ktk uislam but siku hizi yapo. Kuna shia, sunni, suffi, ahmadiyya n.k. Ukiulizwa waislam wa zama za mtume wapo? Utajibu nn ikiwa zama za mtume hakukuwa na madhehebu?. Maswala haya hata wanazuoni huwa wanaamua kujiepusha kutoa hukumu ya moja kwa moja. Kwa maana hiyo watu wa kitabu wapo isipokuwa nao wamegawanyika kama ilivotokea kwa waislam.
Uwepo wao upo ndio maana wametajw katika kitabu tukufu ila kwa zama hizi sidhani, allah anajua zaidi, na kama watakuwepo watakuwepo kwa uchache mnoo, usikute ni mmoja katika watu milion 100... Kuwepo kwa madhehebu hakufanyia kukosekana kwa waislama wa ukweli, katika huko huko kugawanyika kuna wale waliothabiti.
 
Kutokana na mabadiliko ya kimapokeo hadi kufika sasa na kuendelea, katika ulimwengu huu watu wa kitabu hakuna, kwani kila utakayemgusa tayari ni mshirikina [thalithu thalatha]
Hiki ndio nikimaanishacho ndugu alibakari
 
Umebadilisha dini ilii Uongezee Wakeee...haa ha ha..
 
Kasome tena
Soma hapo, usijitie uhayawani.
Kufunga ndoa na mwanamke Myahudi au Mkristo inaruhusiwa kutokana na rai ya Maulamaa wengi.

Ibn Qudaamah (Allaah Amrehemu) alisema katika [Al-Mughni 7/99]: "Hakuna tofauti ya rai za maulamaa kuhusu kuruhusiwa kuwaoa wanawake wa Kitabu. Na miongoni mwa walio na rai hii ambayo ilisimuliwa kutoka kwao ni 'Umar, 'Uthmaan, Talhah, Hudhayfah, Salmaan, Jaabir na wengineo".



Ibn Al-Mundhir kasema: "Hakuna usimulizi ulio sahihi kutoka kizazi cha mwanzo kusema kwamba hivyo ni haraam. Al-Khallaal amesimulia katika Isnaad yake kwamba Hudhayfah, Talhah, Al-Jaaruud ibn Al-Mu'alla na Udhaynah Al-'Abdi wote walioa wanawake wa Ahlul-Kitaab. Hii pia ilikuwa ni rai ya maulamaa wengine wote"

.

Ushahidi mkuu kuhusu masuala haya ni aya ambayo Allaah سبحانه وتعالى Anasema (Na imefasiriwa kuwa na maana):



((الْيَوْمَ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُواْ الْكِتَابَ حِلٌّ لَّكُمْ وَطَعَامُكُمْ حِلُّ لَّهُمْ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الْمُؤْمِنَاتِ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الَّذِينَ أُوتُواْ الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ إِذَا آتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ مُحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ وَلاَ مُتَّخِذِي أَخْدَانٍ وَمَن يَكْفُرْ بِالإِيمَانِ فَقَدْ حَبِطَ عَمَلُهُ وَهُوَ فِي الآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ))





((Leo mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri. (vitu vyote vilivyo halaal, katika chakula Allaah Alichokifanya halaal kama nyama iliyochinjwa, maziwa, mafuta, mboga, matunda) Na chakula (Wanyama waliochinjwa na wengine wanolika) cha walio pewa Kitabu (Mayahudi na Manaswara) ni halali kwenu, na chakula chenu ni halali kwao. Na pia wanawake wema miongoni mwa Waumini, na wanawake wema miongoni mwa waliopewa Kitabu (Mayahudi na Manaswara) kabla yenu, mtakapowapa mahari yao, mkafunga nao ndoa, bila ya kufanya uhasharati wala kuwaweka kinyumba. Na anayekataa kuamini (Tawhiyd ya Allaah na nguzo zote za Imani yaani kuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Yake, Siku ya kufufuliwa, na Qadhaa na Qadar) bila shaka amali yake imepotea, naye katika Akhera atakuwa miongoni mwa wenye khasara)) [Al-Maaidah:5:5]



Maana ya Muhswanaat (wanawake wema) ni wale ambao walio huru na walio katika stara. (Yaani katika heshima na aliye bikra, asiye mhuni) Ibn Kathiyr (Allaah Amrehemu) amesema katika Tafsiyr yake:

"Hii ni rai ya maulamaa wengi wao na hii ndivyo inavyoelekea kuwa hali yenyewe. Asije kuwa dhimiyah (mwanamke asiye Muislam aliye katika hifadhi ya Kiislam) lakini pia asiyekuwa katika stara (heshima, bikra). Ikiwa atakuwa katika hali hii atakuwa amepotoka na mwenye ufisadi, na mumewe atamalizikia kuwa kama inavyoeleza katika methali: "Amenunua tende mbaya na amekhiniwa katika uzito na mizani pia" .



Maana iliyo dhahiri katika aya ni vile ilivyomaanisha "al-Muhsnah"(mwanamke mwenye stara, (aliyekuwa bikra, asiyekuwa mhuni) naye ni mwanamke aliyejiepusha na zinaa kama Allaah سبحانه وتعالى anavyosema katika Aya nyingine:



((مُحْصَنَاتٍ غَيْرَ مُسَافِحَاتٍ وَلاَ مُتَّخِذَاتِ أَخْدَانٍ))



((….wawe wanawake wema, si makahaba wala si mahawara)) An-Nisaa: 4:21





Wakristo na Mayahudi ni Makafiri na washirikina, kutokana na Qur'aan, lakini wametolewa katika kuharamishwa kuolewa wanawake wao kwa sababu Allaah سبحانه وتعالىAnasema katika aya yenye maana:





((وَلاَ تَنكِحُواْ الْمُشْرِكَاتِ حَتَّى يُؤْمِنَّ وَلأَمَةٌ مُّؤْمِنَةٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكَةٍ وَلَوْ أَعْجَبَتْكُمْ وَلاَ تُنكِحُواْ الْمُشِرِكِينَ حَتَّى يُؤْمِنُواْ وَلَعَبْدٌ مُّؤْمِنٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكٍ وَلَوْ أَعْجَبَكُمْ أُوْلَئِكَ يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ وَاللّهُ يَدْعُوَ إِلَى الْجَنَّةِ وَالْمَغْفِرَةِ بِإِذْنِهِ وَيُبَيِّنُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ))



((Wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazi Muumini ni bora kuliko mshirikina hata akikupendezeni. Wala msiwaoze (binti zenu) wanaume washirikina mpaka waamini. Na mtumwa mwanamume Muumini ni bora kuliko mshirikina hata akikupendezeni. Hao wanaitia kwenye Moto, na Allaah Anaitia kwenye Pepo na magha**** kwa idhini Yake. Naye Huzibainisha Aya zake kwa watu ili wapate kukumbuka)) [Al-Baqarah: 2:221]





Hii ni njia ya dhahiri kabisa ya kuwafikiana baina ya aya mbili.





Allaah سبحانه وتعالى Amewaelezea kuwa ni washirikina kama Anavyosema:





((اتَّخَذُواْ أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللّهِ وَالْمَسِيحَ ابْنَ مَرْيَمَ وَمَا أُمِرُواْ إِلاَّ لِيَعْبُدُواْ إِلَهًا وَاحِدًا لاَّ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ سُبْحَانَهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ))





((Wamewafanya makuhani wao na wamonaki wao kuwa ni marabi badala ya Allaah, na pia Masihi bin Maryamu. Na wala hawakuamrishwa isipo kuwa wamuabudu Mungu Mmoja, hapana mungu ila Yeye. Subhanahu, Ametakasika na hayo wanayomshirikisha nayo)) [At-Tawbah: 9:31]



Kwa hiyo 'Watu wa Vitabu' ni makafiri na washirikina, lakini Allaah سبحانه وتعالى Ameturuhusu kula nyama zao na kuwaoa wanawake wao ikiwa watakuwa wenye stara (wenye heshima sio wahuni). Hii imeruhusiwa kutokana na maana ya aya iliyo katika Suratul-Baqarah 2:221 (tulioitaja hapo juu).





Lakini ifahamike kwamba ni bora na usalama kabisa kutokuoa wanawake wa Kitabu khaswa kwa siku hizi.



Ibn Qudaamah (Allaah سبحانه وتعالىAmerehemu) alisema: Kwa vile hali ni hii, ni bora kutokuoa mwanamke wa Kitabu kwa sababu 'Umar aliwaambia wale waliowaoa wanawake wa Kitabu "Waacheni (Wapeni talaka)" kwa hiyo wakawapa talaka isipokuwa Hudhayfah. 'Umar akamuambia: "Mpe talaka". (Hudhayfah) akasema: "Je, Unashuhudia kuwa yeye ni haraam?" Akasema: "Yeye ni mkaa wa moto wenye kuwaka mpe talaka". Akasema: "Je, Unashuhudia kuwa yeye ni haraam?" Akasema: "Yeye ni mkaa wa moto wenye kuwaka". Akasema: "Najua kuwa yeye ni mkaa wa moto wenye kuwaka lakini yeye ni halali kwangu". Baada ya muda akampa talaka na akaulizwa "Kwa nini hukumpa talaka alipokuamrisha 'Umar?" Akasema: "Sikutaka watu wafikiri kuwa nimefanya kosa (kwa kumuoa)".

Labda alikuwa akimpenda au labda kwa sababu walipata mtoto pamoja kwa hiyo alimpenda". [Al-Mughni 7/99]

Vile vile Hadiyth hii ifuatayo Sahiyh inasema:



Ibn 'Umar alipokuwa akiulizwa kuhusu kumuoa mwanamke Mkristo au Myahudi, alikuwa akisema: "Allaah Ameifanya kuwa ni Haraam kwa Muumini kuoa wanawake wanaomshrikisha Allaah katika ibada, na sijui lililo kubwa zaidi kuliko kumshirikisha Allaah katika ibada na kadhalika kama mwanamke kusema 'Iysa ni Mungu ingawa yeye ni mja tu wa Allaah" [Al-Bukhaariy]





Shaykh Ibn Baaz (Allaah Amrehemu) alisema: "Ikiwa mwanamke wa Kitabu anajulikana kuwa ni mwenye stara (sio muhuni) na kujiepusha na njia ambazo zinampeleka mtu katika uasharati, inaruhusiwa kwa sababu Allaah سبحانه وتعالى Ameruhusu hivyo na Ameturuhusu kuwaoa wanawake wao na kula nyama zao.



Lakini siku hizi kuna khofu kwamba wale wanaooa huenda wakakutana na uovu zaidi. Wanaweza kuwaita katika dini yao na wanaweza kuwalea watoto wao katika Ukristo. Kwa hiyo hatari ipo hakika na ni kubwa. Ili kuwa katika amani, Muumini ni bora asiwaoe. Na katika hali nyingi hakuna uhakika kama mwanamke hatofanya vitendo vya uasharati au hatowaleta watoto waliotoka katika uhusiano wa mwanzo. Lakini mwanamume akitaka kufanya hivyo basi hana dhambi kwake ili ajiweke katika stara na ainamishe macho yake kwa kumuoa. Ajitahidi kumuita katika Uislamu na awe na hadhari na uovu wake na hadhari ya kumruhusu asimvute yeye au watoto wake katika ukafiri". [Fataawa Islaamiyyah, 3/172]

Na Allaah Anajua zaidi
 
Chukulia katika mazingira ambayo ninauhuru (wa kikatiba) kuchagua dini yyte ile ninayoitaka. Na uhuru huu ninayo haki ya kuutekeleza wakati wowote ule. Sifungwi kubaki kwenye dini fulani.

Katika mazingira ya kuwa nimeoa mke kwa ndoa ya kikristo ambayo inaruhusu mke mmoja tu kwa mume mmoja na inatambulika hivyo kisheria. Nikiwa kwenye ndoa hiyo, kesho nikaamua kubadili dini na kuwa muislam na huko ninaruhusiwa kuwa na wake hadi wanne.

MASWALI:
1. Kwakua nitakua nimekana dini yangu ya awali, Je sheria itaendelea kumtambua huyu mke wa ndoa ya kikristo?

2. Hata kama tumeamua kuishi pamoja kama wanandoa (yeye abaki kuwa mkristo), je nitakua na uhuru kisheria kuongeza wake?

3. Hata kama tumeamua kuishi pamoja (na mke wangu naye abadili dini na kuwa muislam), je tutakuwa tumefunga ndoa au tutahitaji kuoana upya?

Nielewesheni kisheria na kwa imani ya kiislam pia.
kwa uelewa wangu mdogo hakuna ndoa itakayokuepo inatambulika kidin kama mkeo atabak kua mkristo....ukisema umekua muislam na ukaamua kuoa means unaemuoa ndio mke wakwanza unless aliyepo abadil dini muoane upya kiislam
 
1. Ndio sheria itaendelea kumtambua mke wa kikristo kwani mwanaume muislam anaweza kuwa na ndoa na mtu ambae ni ahlul kitab.
2. Ndio
3. Hakuna haja ya kufunga ndoa upya kwani Uislamu inatambua ndoa ilimradi iwe imefata taratibu za kidini.
Uislamu unatambua ndoa yoyote ilimradi iwe imefata taratibu za kidini, muislam mwanaume ameruhusiwa kuoa mwanamke asiekuwa muislam, pia kama akimsilimisha ni vizuri zaidi, lakini kama mlioana kwa dini nyongine baadae mkasilimu basi hakuna haja ya kuoana upya, na kama mwanamke akiamua kubaki kule kule kwenye dini yake basi haibatilishi ndoa. Na bado huyo mwanamke atatambulika kama mke wako.
Na je, ndoa za kiislam hua zinatoa hati (cheti) ya wanandoa? Inapotambua ndoa ya kikristo, uislam nafas yake inakua ni ipi hapo, au inatoa cheti cha utambuzi?
 
Ikiwa mlifunga ndoa ya kikristo,kisha nyote mkaingia kwenye uislam,basi ndoa yenu ya mwanza inahamishwa upande wa pili kama junsi mlivyohamia upande wa pili na maisha yanasonga.
 
Majibu!
1.Sheria ya kiislam itamtambua mkeo ikiwa na yeye amesilimu(amekuwa muislam)
2.Kama yeye akibaki kuwa mkristo ww utakuwa unazini (utapata dhambi) kwa mujibu wa sheria za kiislam kwa kuwa uislam haukubali ndoa ya muislam na asiye muislam(lazima mke &mume wawe wote waislam)
3.Wote mukibadili dini (mukiwa waislam)hamtatakiwa kufunga ndoa mpya ila ndoa yenu ile ile muliofunga mkiwa wakristo inatosha,Ispokuwa kama wakati mulipokuwa wakristo hamkufunga ndoa basi hapo ndio itawalazimu kufunga ndoa.
Mkuu hapo kwenye no2 ni papana sana...!
So wakati wa kutoa elimu hii adhimu unatakiwa kuwa mwangalifu sana,kumbuka wanawake wa Kitabu walioongelewa katika Qur'an sii waislam!!
 
Na je, ndoa za kiislam hua zinatoa hati (cheti) ya wanandoa? Inapotambua ndoa ya kikristo, uislam nafas yake inakua ni ipi hapo, au inatoa cheti cha utambuzi?
Ndoa za kiislamu zinatoa hati ya ndoa.
Na Uislamu unatambua ndoa iliyofungwa kidini, hata kama hati iliyotolewa ni ya kiserikali, ilimradi imefungwa kidini.
Inapotambua ndoa kikristo Uislamu hautenganishi watu waliooana kidini, bali hakuna hati ya ndoa hapo.

Nakuuliza swali na wewe sasa:
Kwani mtoto aliezaliwa wazee wakiwa wakristo na baadae wazee wakasilimu huyu mtoto anakuwa anaendelea kuwa mkristo au atakuwa muislam?
 
Na je, ndoa za kiislam hua zinatoa hati (cheti) ya wanandoa? Inapotambua ndoa ya kikristo, uislam nafas yake inakua ni ipi hapo, au inatoa cheti cha utambuzi?
Mkuu yes mnapofunga ndoa ya kiislam mnapewa hati ya ndoa,ingawa sii lazima kupewa,maana huwezi kusema hatufungishi ndoa eti kwasasabu vyeti vimeisha.Swali lako la pili sina elimu kubwa ya kukujibu hilo so ngoja wataalamu waje wakusaidie zaidi.
 
Back
Top Bottom