Nimeamua 'kusilimu' je, kisheria na kiimani nitaruhusiwa kuongeza wake nikihitaji?

Haya ndio majibu sahihi...kuna watu humu wanatoa majibu kwa hisia na bila kuwa na ilmu ya mada husika..jambo ambalo ni kosa kisheria.
 
Uwepo wao upo ndio maana wametajw katika kitabu tukufu ila kwa zama hizi sidhani, allah anajua zaidi, na kama watakuwepo watakuwepo kwa uchache mnoo, usikute ni mmoja katika watu milion 100... Kuwepo kwa madhehebu hakufanyia kukosekana kwa waislama wa ukweli, katika huko huko kugawanyika kuna wale waliothabiti.
 
Kutokana na mabadiliko ya kimapokeo hadi kufika sasa na kuendelea, katika ulimwengu huu watu wa kitabu hakuna, kwani kila utakayemgusa tayari ni mshirikina [thalithu thalatha]
Hiki ndio nikimaanishacho ndugu alibakari
 
Umebadilisha dini ilii Uongezee Wakeee...haa ha ha..
 
Kasome tena
Soma hapo, usijitie uhayawani.
 
kwa uelewa wangu mdogo hakuna ndoa itakayokuepo inatambulika kidin kama mkeo atabak kua mkristo....ukisema umekua muislam na ukaamua kuoa means unaemuoa ndio mke wakwanza unless aliyepo abadil dini muoane upya kiislam
 
Na je, ndoa za kiislam hua zinatoa hati (cheti) ya wanandoa? Inapotambua ndoa ya kikristo, uislam nafas yake inakua ni ipi hapo, au inatoa cheti cha utambuzi?
 
Ikiwa mlifunga ndoa ya kikristo,kisha nyote mkaingia kwenye uislam,basi ndoa yenu ya mwanza inahamishwa upande wa pili kama junsi mlivyohamia upande wa pili na maisha yanasonga.
 
Mkuu hapo kwenye no2 ni papana sana...!
So wakati wa kutoa elimu hii adhimu unatakiwa kuwa mwangalifu sana,kumbuka wanawake wa Kitabu walioongelewa katika Qur'an sii waislam!!
 
Na je, ndoa za kiislam hua zinatoa hati (cheti) ya wanandoa? Inapotambua ndoa ya kikristo, uislam nafas yake inakua ni ipi hapo, au inatoa cheti cha utambuzi?
Ndoa za kiislamu zinatoa hati ya ndoa.
Na Uislamu unatambua ndoa iliyofungwa kidini, hata kama hati iliyotolewa ni ya kiserikali, ilimradi imefungwa kidini.
Inapotambua ndoa kikristo Uislamu hautenganishi watu waliooana kidini, bali hakuna hati ya ndoa hapo.

Nakuuliza swali na wewe sasa:
Kwani mtoto aliezaliwa wazee wakiwa wakristo na baadae wazee wakasilimu huyu mtoto anakuwa anaendelea kuwa mkristo au atakuwa muislam?
 
Na je, ndoa za kiislam hua zinatoa hati (cheti) ya wanandoa? Inapotambua ndoa ya kikristo, uislam nafas yake inakua ni ipi hapo, au inatoa cheti cha utambuzi?
Mkuu yes mnapofunga ndoa ya kiislam mnapewa hati ya ndoa,ingawa sii lazima kupewa,maana huwezi kusema hatufungishi ndoa eti kwasasabu vyeti vimeisha.Swali lako la pili sina elimu kubwa ya kukujibu hilo so ngoja wataalamu waje wakusaidie zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…