Nimeamua kusimamisha masomo ya PhD nje ya nchi ili nijitayarishe kwaajili ya kugombea ubunge 2025 katika jimbo la Mbozi Mashariki

Kwanza nikushukuru kwa ushauri mzuri pale mwisho. Nilijitahidi kuelekeza mawazo yangu shule, lakini wito wa kulifanya hili jambo uliishinda maamuzi ya moyo wangu.

Tutaogopa mpaka lini boss. Tumekuwa tukiambiwa kwamba kwenye mambo ya siasa bila uchawi hutoboi.

Ni kweli hata mimi hili nililishuhudia miaka ya nyuma. Lakini tumwamini Mungu zaidi na kujaribu ili na sisi tuushuhudie huo uchawi.

Mimi kiukweli nimejipanga katika hili na siwezi kuogopa, nimedhamiria haswa.
 
Sasa unatangaza nia unajificha hivyo jiweke wazi tukujue ili tuamue ku kuunga mkono au upite kule
 
Sasa unatangaza nia unajificha hivyo jiweke wazi tukujue ili tuamue ku kuunga mkono au upite kule
Nitajitokeza hadharani boss ndio maana leo nimeamua kuweka wazi hapa ili mpate kujua mapema wanajamii forums wenzangu ikiwezekana tushikane mikono ili kutimiza adhima hii.
 
Unatangaza humu ili iweje? Fanya mambo yako kimya kimya. Unataka ujulikane umepata nafasi kwenye doctorate program lakini kiukweli huna maturity wala intellect ya kusoma PhD. Halafu "niahilishe" ndiyo nini?
 
Bora ungeenda shule,
 
Nia yako ni njema ila endelea na masomo.
Siasa ya Tanzania ina "mtego wa panya"
Mtego wa kwanza ni mpaka upate "utezi wa chama chako kugombea" ndipo ugombee. Huo uhakika ni 50/50. Maana yake hii ni kamari.

Mtego wa pili unapogombea, kuchaguliwa na wapiga kura ni jambo moja na "kutanganzwa mshindi" ni jambo la pili. Hii nayo ni 50/50 kamari.

Kusoma PhD kuna certainty, chance za kuhitimu ni kubwa kuliko kuingia kwenye politics na hasa bongo politics.

Tungekuwa tuna mgombea binafsi na tuna tume ambayo majumuisho hayafanywi na ma-DED, ningekushauri njoo, otherwise, malizia uzamivu kwenye petrolium na gas. Ila kama unalenga kuja, usije sasa. 2023, 2024 ni muda mrefu sana. Utaishiwa pumzi mapema kabla ya game kuanza.
 
Ila ubunge ulikua ni wa kuteuliwa make hakukuwa na uchaguzi
 

Kumbe PhD ya Kichina, in terms of rank if i will be asked, i will give it 10% Chinese PhD

Anyway kasome achana na kutafuta ubunge, utapotea milele, labda ww mgeni ktk viwanja vya siasa za kwenye field, uko kwenye siasa za online tu, achana na ubunge ukasome kwanza.
 
Elimu ni wewe mwenyewe boss.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…