Nimeamua kusimamisha masomo ya PhD nje ya nchi ili nijitayarishe kwaajili ya kugombea ubunge 2025 katika jimbo la Mbozi Mashariki

Nimeamua kusimamisha masomo ya PhD nje ya nchi ili nijitayarishe kwaajili ya kugombea ubunge 2025 katika jimbo la Mbozi Mashariki

Magufuli hakuwa perfect na moja ya makosa makubwa sana na kumfanya yeye na Bashiru wachukiwe na vigogo wengi ndani ya CCM ni hilo kwenye kukata.

Magufuli kwangu atabaki shujaa no matter what, lakini kwenye kupindua meza za kura za maoni na jinsi alivyo deal na COVID alifanya maamuzi ya ovyo mno na yasiyo stahiki uvumilivu ata ningekuwa kuwa mimi naulizwa what to do ningependekeza lolote atolewe (hapo ndipo alipoanza kujiona mungu mtu) what a pity kwa sababu alikuwa na mengine mengi ya muhimu ambayo yeye tu angeweza fanya from evidence so far,
I salute ur comment mkuu
 
Habari za leo watanzania wenzangu,

Mimi rafiki yenu na kijana mwenzenu nilishafungua moyo wangu kuwatumikia watanzania katika kiti cha ubunge. Kama kuna wabunge humu naomba watanishauri zaidi ila ni jambo ambalo nalipenda na nina uzoefu nalo kidogo.

Muda wangu sahihi wa kujitokeza hadharani utakua 2025 ila bado sijaweka wazi nitagombea ubunge kupitia chama gani.

Hii ndio sababu kubwa iliyonifanya nisitishe masomo yangu haraka sana ili niweze kujipanga katika hili. Nilipata kuchaguliwa kuendelea na masomo ya PhD katika chuo kimoja huko nje ya nchi. Ilinipasa mwezi wa tisa mwaka jana niwe nimeshaingia chuoni na kuanza masomo yangu.

Naombeni kuungwa mkono katika hili. Najua muda ukiwadia ipo siku nitamalizia elimu yangu. Lakini kwasasa nijapange ili kutimiza adhima yangu.

Ahsanteni jamani.

View attachment 2495736

View attachment 2495735
Kwanini usifanye vyote viwili?
 
Labda kama una sababu nyingine ila naona umekosea sana kuacha PhD na full scholarship kwenda kugombea ubunge ambao ni miaka mitatu ijayo na huna uhakika utachaguliwa. Lazima kuna kitu kingine. Kama hujaacha tatadhali endelea na masomo!
 
Sema hiyo scholarship yako ya China haina Maslai nadhani ingekuwa ulaya nchi Kama UK sidhani Kama ungejiuliza mara mbili. Kugombea Ubunge Ni Hadi 2025 na mchakato unahitaji miez Kama mitatu tu ya kujiandaa so kuacha masomo yako yenye Maslai mapana kisa ubunge haupo sahihi maana huko unaenda kubeti.
 
Kwanza nikushukuru kwa ushauri mzuri pale mwisho. Nilijitahidi kuelekeza mawazo yangu shule, lakini wito wa kulifanya hili jambo uliishinda maamuzi ya moyo wangu.

Tutaogopa mpaka lini boss. Tumekuwa tukiambiwa kwamba kwenye mambo ya siasa bila uchawi hutoboi.

Ni kweli hata mimi hili nililishuhudia miaka ya nyuma. Lakini tumwamini Mungu zaidi na kujaribu ili na sisi tuushuhudie huo uchawi.

Mimi kiukweli nimejipanga katika hili na siwezi kuogopa, nimedhamiria haswa.

..Nakushauri umalize PhD yako.

..Au tafuta namna ya kufanya yote mawili yaani PhD na harakati za ubunge.

..kuna watu wako kwenye ubunge / siasa na wameweza kusoma Masters au PhD.
 
Nia yako ni njema ila endelea na masomo.
Siasa ya Tanzania ina "mtego wa panya"
Mtego wa kwanza ni mpaka upate "utezi wa chama chako kugombea" ndipo ugombee. Huo uhakika ni 50/50. Maana yake hii ni kamari.
Mtego wa pili unapogombea, kuchaguliwa na wapiga kura ni jambo moja na "kutanganzwa mshindi" ni jambo la pili. Hii nayo ni 50/50 kamari.

Kusoma PhD kuna certainty, chance za kuhitimu ni kubwa kuliko kuingia kwenye politics na hasa bongo politics.

Tungekuwa tuna mgombea binafsi na tuna tume ambayo majumuisho hayafanywi na ma-DED, ningekushauri njoo, otherwise, malizia uzamivu kwenye petrolium na gas. Ila kama unalenga kuja, usije sasa. 2023, 2024 ni muda mrefu sana. Utaishiwa pumzi mapema kabla ya game kuanza.
Acha kukatisha tamaa wenye mawazo tofauti na wewe? Au nawe ni mbunge wa eneo hilo?
 
Honesty doesn’t take people very far in life. But then if I am deemed a fool from the opinion of others why bother to air it. With that insight I might as well dish the nasty.

Hivi mtu ambae una promote biashara isiyo na maadili ya kusaidia watu kufaulu degrees zao unethically kwa ku assess kazi zao ili wafaulu (shida zaidi sio wewe) Ila hiyo serikali iliyokuwa kimya kuacha wapuuzi kama nyie ku advertise ujinga wenu.

Binafsi na kuona ni mtu ambae very unethical.

Na kuhusu Oil and Gas industry, ufahamu wako ni mdogo sana. As Plato put it in his ship leadership analogue, popularity wins.

Huko kwenye environmental issues ndio mweupe kabisa, but then with the Tanzania audience you don’t need much to get ahead.

Hivi unawezaje ku apply Phd, upate nafasi ambayo very competitive and then abandon the mission.

Common sense says Phd takes roughly about 2 years minimum to complete from your acceptance date. Should you have chosen to do it by then you would have graduated to pursue ya political ambitions.

Vilaza kama nyie uwongo wenu kuaminika ni kwa sababu ya audience ya J.F.

Binafsi sikatai unaweza kuwa.na ajira katika sector ya nishati, ila kwa kukusoma uelewa wako wa hiyo industry ni mdogo sana.

Sometimes I have to tell what it is. Don’t mind me, just remember Plato ship analogue.
 
Umeona JF Watu Wanavyolalama Kuhusu Tanzania
Nchi Inavyobolewa Ukipata Nafasi Usiende Kufanya Ujinga
Ukiingia Kwenye Kamati Hizo Ndiyo Force Account Zenu

Jimbo Nitakushauri Huko Unakogombea Ndiyo Wazazi Wangu Wametokea
 
Hiyo itakuwa PhD fake ya miaka 2.

Andika kwa kiswahili tu tutaelewa
Kwani we unadhani Phd ni kitu special sana?

That’s just a five chapter thesis same as in

First degree 10000 words
Masters 10000- 25000 words
Doctorate 50000+ words

All you need is to pick is a topic of Interest and extrapolate it following the rules required in writing the five chapters thesis.

Binafsi najiamini naweza fyatua any degree ambayo aihitaji complex mathematics nor laboratory researches.

Sitanii na huyu dada uelewa wake wa oil and gas ni very limited. Kwa mie ambae nimezifyatua hizo.

Mengine ni kupongezana ujinga kama ilivyo hada yenu watanzania.
 
Hatuna Jimbo linaloitwa Mbozi mashariki katika mkoa wa Songwe, masuala ya Mbozi mashariki na magharibi yalikwishaga na kuishia kwa akina Zambi na Silinde, ambapo Jimbo la Mbozi mashariki lilitoa Jimbo la Mbozi linaloongozwa kwa Sasa na mh GEORGE RAINWELL MWENISONGOLE pamoja na Jimbo la Vwawa linaloongozwa na mh Hasunga, wakati Mbozi magharibi lilitoa majimbo ya Tunduma ambalo kwa Sasa linaongozwa na mh Silinde, pamoja na la Momba.

Kutokujua tu majimbo katika eneo unapokwenda kugombea kunakuondolea sifa ya kupewa nafasi ya kugombea maana Kama hata majimbo huyajuwi bila Shaka hata kero za wananchi huwezi ukazijua iwe Ni kata ya Mlowo, Igamba, Shiwinga, Mahenje, Itaka, Bara, Nambizo, Magamba,n.k

Hata hivyo majimbo Yana watu tayari na kwa kanuni zetu wanaccm hupaswi kuanza vurugu za kampeni wakati huu bali unapaswa kumsaidia aliyopo labda Kama unagombea kupitia huko kwa wababaishaji wa chadema wasio na Sera Wala ajenda Wala Dira.

Pia kutokujuwa hata chama Cha kugombea pia huo Ni ubabaishaji mwingine maana huo Ni usaka tonge tu na kuangalia mahali kwenye fursa badala ya kuangalia itikadi ya chama.

Ushauri Wangu Ni kuwa Kama unataka kugombea kupitia chama changu Cha CCM nakushauri ungeendelea tu na masomo yako maana naona upo bado Sana kuiva kisiasa na badala yake ungejikita katika fani yako ya mafuta ili ulisaidie Taifa kuliko kuja kupoteza muda wako wakati hadi Sasa hujui hata chama kipi ugombee na Wala huna chama, Sasa Kama huna chama Ni mjinga gani atakupigia Kura wakati anaona wewe Ni msaka fursa?

Pili lazima uwe na misimamo katika maisha maana mpaka Sasa haieleweki unasimamia Nini na unataka Nini, pia wapiga kura ambao Ni wajumbe Ni waelewa Sana kwa Sasa hivyo usije kujipa majibu yako ya kubuni.

Kwahiyo mama kwenye uteuzi bado HAJAKUONA?

#YNWA
 
Hongera Mkuu kwa kusimama katika kile unachokiamini na kuifukuzia ndoto yako. Kwa kweli siasa za bongo ni ngumu na zinafigisu nyingi. Kujuana, rushwa, ushirikina n.k. Huenda ukawa vzr sana kwenye sera na mipango yako ya kuikomboa jamii lakini wapinzani wako wakawa vzr zaidi kwenye mipango ya nje ya uwanja ukajikuta unapata kura 6 kwa wajumbe halafu mwenzio kura 300. Ingawa kiuhalisia wewe unakuwa upo vizuri mno kuliko huyo mshindi.

Ushauri wangu kwako:
1. Kama ndio kwanza unakwenda kujihusisha na siasa actively and openly, nashauri hizo harakati uzianze mapema sana kujipitisha ujulikane. Ukichelewa sn kupita utaonekana ni msaka tonge tu. Pia lijue eneo lako kwa marefu na mapana. Vitongoji, kata na vijiji.

2. Pamoja na kutaka kujulikana, kuwa makini sana usijitangaze wazi kuwa unautaka ubunge ktk hatua hii. Watakula kichwa huko mbele kwa kujitangaza mapema na kukatisha ndoto yako. Ila Jitoe kama msamalia mwema kwenye mashule nunua hata madaftari ya bei poa peleka kama msaada, kwenye misiba jitokeze na sapoti unachoweza, michezo n.k

3. Wajue wajumbe wote wa chama chako wanaopiga kura za uteuzi wa wagombea na uwe nao karibu sn kwa namna unaweza. Jishushe sn. Sometimes siasa na unafki ni ndugu wa damu.
4. Fanya uchaguzi makini wa jimbo ambalo unaweza kummudu kiongozi aliyepo. Awe ni yule ambaye si waziri na hana jina wala mambo makubwa sn ameyafanya jimboni.

Alternatively:
Ni ngumu lakini inawezekana, kwa mtu anayejitokeza na kuingia kwenye siasa kwa mara ya kwanza tu na akapata ubunge. Hivyo, naweza pia kukushauri kutoacha shule hiyo kubwa huku ukizingatia umepata Full Scholarship na unalipiwa kila kitu; ada hadi kula na kulala.

Endapo ningelikuwa ni mimi, ningeendelee na masomo ila kipindi cha kuchukua fomu ama shortly before, ningeomba udhuru kdg chuoni na kuja japo kwa awamu hii kutest zari na kutanguliza jina kwa mipango ya mbele. Ukiipata fursa basi alhamdulillahi ila ukikosa fursa ya kupita basi, kule chuoni pia unakuwa hujapoteza unarudi na kuendelea. Uzuri haya majimbo na siasa zipo tu. Ukitanguliza jina na baadae ukapata hiyo PHD ktk chama tunaweza kukuangalia pia ktk eneo lingine. Wengi walio na elimu nzr na ambao wamejitokeza tu angalau hufikiliwa hata nafasi za Dc, Rc, Ded n.k

So, bro chakata bongo before muda wa hiyo fursa ya masomo haijakoma. Usije kosa kote. Nakutakia kila la Kheri.

Asante.

Nzwangendaba
 
Habari za leo watanzania wenzangu,

Mimi rafiki yenu na kijana mwenzenu nilishafungua moyo wangu kuwatumikia watanzania katika kiti cha ubunge. Kama kuna wabunge humu naomba watanishauri zaidi ila ni jambo ambalo nalipenda na nina uzoefu nalo kidogo.

Muda wangu sahihi wa kujitokeza hadharani utakua 2025 ila bado sijaweka wazi nitagombea ubunge kupitia chama gani.

Hii ndio sababu kubwa iliyonifanya nisitishe masomo yangu haraka sana ili niweze kujipanga katika hili. Nilipata kuchaguliwa kuendelea na masomo ya PhD katika chuo kimoja huko nje ya nchi. Ilinipasa mwezi wa tisa mwaka jana niwe nimeshaingia chuoni na kuanza masomo yangu.

Naombeni kuungwa mkono katika hili. Najua muda ukiwadia ipo siku nitamalizia elimu yangu. Lakini kwasasa nijapange ili kutimiza adhima yangu.

Ahsanteni jamani.

View attachment 2495736

View attachment 2495735
Aliyekwambia tunachagua Wasomi waganga njaa ni nani?
 
Ahsante sana kwa ushauri mzuri. Ushauri huu nitaanza kuufanyia kazi kwa uharaka sana rafiki.
Hawa nadhani ndiyo diaspora wa CHADEMA wanaoenda kupigana vita Ukraine ili watupatie tumehuru, wakiuliwa ndiyo wanamkumbuka Mama Tanzania waliyemkana. Elimu ni kitu cha kwanza; Mtume aliwaasa Waislamu wote waende China na kila mahali kujiongezea elimu, yeye huyu anataka aache shule abaki kipofu atuongoze vipofu wapi na wapi. Please ignore him.
 
Huyu ni mwanaccm tafadhali
 
Back
Top Bottom