Hatuna Jimbo linaloitwa Mbozi mashariki katika mkoa wa Songwe, masuala ya Mbozi mashariki na magharibi yalikwishaga na kuishia kwa akina Zambi na Silinde, ambapo Jimbo la Mbozi mashariki lilitoa Jimbo la Mbozi linaloongozwa kwa Sasa na mh GEORGE RAINWELL MWENISONGOLE pamoja na Jimbo la Vwawa linaloongozwa na mh Hasunga, wakati Mbozi magharibi lilitoa majimbo ya Tunduma ambalo kwa Sasa linaongozwa na mh Silinde, pamoja na la Momba.
Kutokujua tu majimbo katika eneo unapokwenda kugombea kunakuondolea sifa ya kupewa nafasi ya kugombea maana Kama hata majimbo huyajuwi bila Shaka hata kero za wananchi huwezi ukazijua iwe Ni kata ya Mlowo, Igamba, Shiwinga, Mahenje, Itaka, Bara, Nambizo, Magamba,n.k
Hata hivyo majimbo Yana watu tayari na kwa kanuni zetu wanaccm hupaswi kuanza vurugu za kampeni wakati huu bali unapaswa kumsaidia aliyopo labda Kama unagombea kupitia huko kwa wababaishaji wa chadema wasio na Sera Wala ajenda Wala Dira.
Pia kutokujuwa hata chama Cha kugombea pia huo Ni ubabaishaji mwingine maana huo Ni usaka tonge tu na kuangalia mahali kwenye fursa badala ya kuangalia itikadi ya chama.
Ushauri Wangu Ni kuwa Kama unataka kugombea kupitia chama changu Cha CCM nakushauri ungeendelea tu na masomo yako maana naona upo bado Sana kuiva kisiasa na badala yake ungejikita katika fani yako ya mafuta ili ulisaidie Taifa kuliko kuja kupoteza muda wako wakati hadi Sasa hujui hata chama kipi ugombee na Wala huna chama, Sasa Kama huna chama Ni mjinga gani atakupigia Kura wakati anaona wewe Ni msaka fursa?
Pili lazima uwe na misimamo katika maisha maana mpaka Sasa haieleweki unasimamia Nini na unataka Nini, pia wapiga kura ambao Ni wajumbe Ni waelewa Sana kwa Sasa hivyo usije kujipa majibu yako ya kubuni.