Nimeamua kusimamisha masomo ya PhD nje ya nchi ili nijitayarishe kwaajili ya kugombea ubunge 2025 katika jimbo la Mbozi Mashariki

Habari za leo watanzania wenzangu,

Mimi rafiki yenu na kijana mwenzenu nilishafungua moyo wangu kuwatumikia watanzania katika kiti cha ubunge. Kama kuna wabunge humu naomba watanishauri zaidi ila ni jambo ambalo nalipenda na nina uzoefu nalo kidogo.

Muda wangu sahihi wa kujitokeza hadharani utakua 2025 ila bado sijaweka wazi nitagombea ubunge kupitia chama gani.

Hii ndio sababu kubwa iliyonifanya nisitishe masomo yangu haraka sana ili niweze kujipanga katika hili. Nilipata kuchaguliwa kuendelea na masomo ya PhD katika chuo kimoja huko nje ya nchi. Ilinipasa mwezi wa tisa mwaka jana niwe nimeshaingia chuoni na kuanza masomo yangu.

Naombeni kuungwa mkono katika hili. Najua muda ukiwadia ipo siku nitamalizia elimu yangu. Lakini kwasasa nijapange ili kutimiza adhima yangu.

Ahsanteni jamani.

View attachment 2495736

View attachment 2495735
Hongera na kila la kheri! Go go gooooo
 
Hatuna Jimbo linaloitwa Mbozi mashariki katika mkoa wa Songwe, masuala ya Mbozi mashariki na magharibi yalikwishaga na kuishia kwa akina Zambi na Silinde, ambapo Jimbo la Mbozi mashariki lilitoa Jimbo la Mbozi linaloongozwa kwa Sasa na mh GEORGE RAINWELL MWENISONGOLE pamoja na Jimbo la Vwawa linaloongozwa na mh Hasunga, wakati Mbozi magharibi lilitoa majimbo ya Tunduma ambalo kwa Sasa linaongozwa na mh Silinde, pamoja na la Momba.

Kutokujua tu majimbo katika eneo unapokwenda kugombea kunakuondolea sifa ya kupewa nafasi ya kugombea maana Kama hata majimbo huyajuwi bila Shaka hata kero za wananchi huwezi ukazijua iwe Ni kata ya Mlowo, Igamba, Shiwinga, Mahenje, Itaka, Bara, Nambizo, Magamba,n.k

Hata hivyo majimbo Yana watu tayari na kwa kanuni zetu wanaccm hupaswi kuanza vurugu za kampeni wakati huu bali unapaswa kumsaidia aliyopo labda Kama unagombea kupitia huko kwa wababaishaji wa chadema wasio na Sera Wala ajenda Wala Dira.

Pia kutokujuwa hata chama Cha kugombea pia huo Ni ubabaishaji mwingine maana huo Ni usaka tonge tu na kuangalia mahali kwenye fursa badala ya kuangalia itikadi ya chama.

Ushauri Wangu Ni kuwa Kama unataka kugombea kupitia chama changu Cha CCM nakushauri ungeendelea tu na masomo yako maana naona upo bado Sana kuiva kisiasa na badala yake ungejikita katika fani yako ya mafuta ili ulisaidie Taifa kuliko kuja kupoteza muda wako wakati hadi Sasa hujui hata chama kipi ugombee na Wala huna chama, Sasa Kama huna chama Ni mjinga gani atakupigia Kura wakati anaona wewe Ni msaka fursa?

Pili lazima uwe na misimamo katika maisha maana mpaka Sasa haieleweki unasimamia Nini na unataka Nini, pia wapiga kura ambao Ni wajumbe Ni waelewa Sana kwa Sasa hivyo usije kujipa majibu yako ya kubuni.
Kugombea ubunge ni uoga wa maisha.
 
PhD inasomwaje?! Maajabu ya Mataga
 
Napataje full funded scolarship na mimi niongezee masters
Unapenda nchi gani? Unapenda scholarship ipi kati ya hizi.
Commonwealth scholarship?
Chinese government scholarship?
Full Bright scholarship?
Swedish Scholarship?
Canadian scholarship?
 
Otherwise nakutakia kheri huko jimboni. Kama vipi gombea mbeya mjini against Tulia😂😂😂
😂😂😂dada yangu Dr. Tulia sitomweza amejipanga sana. Naangalia padhaifu panapoingilika. Napenda tuibadilishe Mbozi.
 
Hatuna Jimbo linaloitwa Mbozi mashariki katika mkoa wa Songwe, masuala ya Mbozi mashariki na magharibi yalikwishaga na kuishia kwa akina Zambi na Silinde, ambapo Jimbo la Mbozi mashariki lilitoa Jimbo la Mbozi linaloongozwa kwa Sasa na mh GEORGE RAINWELL MWENISONGOLE pamoja na Jimbo la Vwawa linaloongozwa na mh Hasunga, wakati Mbozi magharibi lilitoa majimbo ya Tunduma ambalo kwa Sasa linaongozwa na mh Silinde, pamoja na la Momba.

Kutokujua tu majimbo katika eneo unapokwenda kugombea kunakuondolea sifa ya kupewa nafasi ya kugombea maana Kama hata majimbo huyajuwi bila Shaka hata kero za wananchi huwezi ukazijua iwe Ni kata ya Mlowo, Igamba, Shiwinga, Mahenje, Itaka, Bara, Nambizo, Magamba,n.k

Hata hivyo majimbo Yana watu tayari na kwa kanuni zetu wanaccm hupaswi kuanza vurugu za kampeni wakati huu bali unapaswa kumsaidia aliyopo labda Kama unagombea kupitia huko kwa wababaishaji wa chadema wasio na Sera Wala ajenda Wala Dira.

Pia kutokujuwa hata chama Cha kugombea pia huo Ni ubabaishaji mwingine maana huo Ni usaka tonge tu na kuangalia mahali kwenye fursa badala ya kuangalia itikadi ya chama.

Ushauri Wangu Ni kuwa Kama unataka kugombea kupitia chama changu Cha CCM nakushauri ungeendelea tu na masomo yako maana naona upo bado Sana kuiva kisiasa na badala yake ungejikita katika fani yako ya mafuta ili ulisaidie Taifa kuliko kuja kupoteza muda wako wakati hadi Sasa hujui hata chama kipi ugombee na Wala huna chama, Sasa Kama huna chama Ni mjinga gani atakupigia Kura wakati anaona wewe Ni msaka fursa?

Pili lazima uwe na misimamo katika maisha maana mpaka Sasa haieleweki unasimamia Nini na unataka Nini, pia wapiga kura ambao Ni wajumbe Ni waelewa Sana kwa Sasa hivyo usije kujipa majibu yako ya kubuni.
Haya maneno kama yanatoka kwa mbunge aliyeko madarakani vile....
 
Umejipanga kwa masuala ya uganga na uchawi. Siasa ya Tanzania inategemea pesa na uwezo wako wa kuroga.
Angalau wakati wa Magufuli hakukuwa na uwezekano wa kupata Ubunge kwa pesa na ndumba ila kwa sasa tumerudi siasa za awamu ya nne. Wewe unadhani yule Mbunge alikuwa anaweza kumng'oa Chenge, hapana!
alipita kwa msuli wa Magufuli!

Ungeomba ushauri mapema, tungekushauri uende shule kuliko kugombea nafasi ambayo sharti ujue kusoma na kuandika!
Unafikiri ilikuwa sawa raisi kupanga safu ya wabunge anaowataka yeye ktk majimbo yote? Je, wangeweza kutekeleza majukumu ya kuihoji serikali? Yaani Wananchi wa masasi waseme huyu ndiye tunayemtaka, alafu raisi apindue meza awaletee chawa wake kwa kuwalazimishia?
 
Magufuli hakuwa perfect na moja ya makosa makubwa sana ya kumfanya yeye na Bashiru wachukiwe na vigogo wengi ndani ya CCM ni hilo kwenye kukata.

Magufuli kwangu atabaki shujaa no matter what.

Lakini kwenye kupindua meza za kura za maoni na jinsi alivyo deal na COVID alifanya maamuzi ya ovyo mno na yasiyo stahiki uvumilivu ata ningekuwa kuwa mimi naulizwa what to do ningependekeza lolote atolewe (hapo ndipo alipoanza kujiona mungu mtu) what a pity kwa sababu alikuwa na mengine mengi ya muhimu ambayo yeye tu angeweza fanya hizo reforms from evidence up to that point.
 
Back
Top Bottom