HAbari zenu wakuu.
Binafsi nataka nimfungulie mama watoto biashara, basi nikatarget sehemu fulani kwa ajili ya biashara hiyo.
katika kufanya maulizo ya hapa na pale nikaambiwa natakiwa niwe na kama milioni nane(8) ili niweze kumvua mtu fremu, bado tra, pia kodi ya hiyo fremu ni 300k kwa mwezi.
Pia, bado jiji, usafi, fire, na tozo nyingine ambazo wafanyabiashara mnazifahamu, Figisu za washirikina, Bado kodi ya maskani tunapoishi.
Nikaona huu mziki siuwezi.
Nilichoamua kukifanya kwa sasa ni kukodi apartment ambayo nitakuwa nalipa 250k-300k per month kisha humo ndani nitenge chumba kimoja nikifanyie decoration muwe mwa kisasa, kisha nimuelekeze wife aanze kufanya biashara mtandaoni, maana hata hao wenye mafremu nao wanajitangaza humuhumu mitandaoni.
Kwa mtazamo wangu naona hapo nitakuwa nimeokoa gharama nyingi. Au wajuvi mnaushauri gani juu ya hili??
Jiji ni Mwanza