Tatizo kubwa kwa sisi wanavyuo hatuwazi nje ya box,kila mtu akipata vilaki kadhaa(mwanachuo) anakimbilia kufungua banda la chipsi.OK fine malengo yako baada ya hilo banda?.
OK Mimi ni mwanachuo wa mwaka wa pili,nimeamua kuja na ubunifu tofauti wa biashara yangu.Nimendunduliza nikafikisha laki sita na nusu na ninadream zakuja kuwa bakharesa hapo baadae.Unajua nimefanya nini?.
Nimetafuta vijana waaminifu wawili niliosoma nao wakafeli school.Mmoja yupo huko hom(mkoani) mwingine nimemtumia nauli elfu 50 aje dsm nikae nae geto(kashafika).
Nimechofanya yule wa mkoani(ninamuamini sana) nilimtumia laki nne na nusu,akanunua mchele kg 400.kilo kwa sasa mchele mpya ni 1000Tzsh.Kwahiyo apo ilienda sh laki nne.akabakiwa na sh elfu arobain,nmejumlisha na hela yakutoa mchele mashineni na magunia yakuuwekea.
Baada ya hapo akaenda tafuta usafili ambao kila kg 100,wamemtoza sh elfu 10000.kwahiyo kg 400 akawa kamaliza ela mpaka mzigo kufika dar.
Sasa unajua nmeamua kuifanya vipi hii biashara.Mimi nauza kuanzia Kg5. Kwa shilling 1800 kila kilo.Nmechukua oda ya mama ntilie wanao uza chakula chuo nacho somea,pia na baadhi ya mama ntilie wamtaani.
Pia nawauzia wanafunzi wanao jipikia kwenye magheto.Jambo la msingi nimelofanya nikuwa mtu akihitaji mchele ananipigia simu.nampelekea mchee mpaka mahali anapokaa.
Kama itakuwa mbali sana ambapo ntahitaji usafiri basi itabidi kg1 mteja ainunue kwa sh 1900.
Mchele naouza quality yake kwenye maduka ya mitaani ni sh 2200.
Sasa nmeanza na hizi kg 400,ambazo nikiziuza kwa kg1, sh 1800. Ntatoa sh 720000.Na hii nategemea ndani ya siku 10,mpaka 12 ntakuwa nmeshaipata.kwahiyo awamu ijayo ntatuma kg zaidi ya 580 km bei haitopanda
Tumekubaliana nahawa jamaa zangu wawili tutaanza kulipana japo ela ya sabuni baada ya miezi minne.Nahuku nikiwa nimesubili ela ya bum nitoe kama laki tatu niongezee ili mtaji ukue baada ya mauzo.
Pia nmekopwa mzani ntakuwa nalipa kidogo kidogo kadri mauzo yangu yatakavyokuwa.
Chakula ambacho nakula mie na huyu jamaa yangu kipo nje ya bajeti ya mtaji.
Nawewe mwanafunzi mahali ulipo/mtu mwenye mtaji mdogo waweza jaribu hii nahakika itakulipa.
Au kama mtu yeyote mwenye ushauli zaidi namna ntakavyoboresha zaidi anaweza nisaidia(tusaidia).
Sitaki kazi.