Nimeamua nithubutu ingawa nina mtaji pungufu ya laki saba. Nawe waweza jaribu mahali unapoishi

Namshukuru Mungu kuendelea kunipa nguvu na afya.Naendelea kupumbana ingawa kuna changamoto za hapa na pale.Lakini ndio hivo yanipasa nipambane ili nijikwamue hapa nilipo.

Baada yawanafunzi wenzagu kuona nafanya hii mishe kuna baadhi yao nao wameamua kufanya(kuiga kila kitu),lakini sio jambo mbaya,hii itasaidia wateja kupata mchele mzuri.Na pia ubunifu zaidi ndio unahitajika ili niweze kustahimili.Kutoka kg 400 mpaka sasa nauwezo wakuagiza kg 1500.Hii pesa inayopatikana hapa sijawahi kula at a shilingi mpaka sasa.Faida yote inayopatikana hungeuka na kuwa sehemu ya mtaji.

Pia namshukuru Mungu sijawahi dhulumiwa tofauti na pale nilipoagiziwa vipande vya Michele(chenga).Endeleeni kunipa mawazo wakuu,nifanye nini ili kuweza kuwafikia wateja wengi zaidi.

Asante sana kwa mawazo yenu,nayafanyia kazi wakuu.
 
Hongera sana kwa kukomaa.. jee baada ya msimu wa mchele kuisha utabadilisha biashara au?
 

hii ni kiboko big up sana kaka
 
Hongera sana kwa kukomaa.. jee baada ya msimu wa mchele kuisha utabadilisha biashara au?
Mkuu mchele huwa hauishi msimu Ila kunakupanda na kushuka kwa bei.Kipindi mchele unapouzwa kg 1 sh 2500 hapa dar basi mikoani kilo moja ikipanda sana huwa ni sh 1700.Kwahiyo faida itaendelea kupatikana ingawa nitapata faida ndogo kwa sababu mtaji wangu unakuwa mdogo.Kwahiyo ntaendelea na hii biashara sema kuna deadline nimepanga itakapofikia ntaongeza biashara nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…